Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Viongozi wa Kampuni ya Star Times ya China baada ya makabidhiano ya Leseni kwa Kampuni hiyo katika sherehe zilizofanyika leo Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
 Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Joseph Kilange akimkabidhi Mwenyekiti wa Kampuni ya Star Times ya China Pang Xin Xing Leseni Kampuni hiyo kufanya kazi zake rasmi Zanzibar  katika sherehe iliyofanyika leo Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
 Mwenyekiti wa Kampuni ya Star Times ya China Pang Xin Xing akitoa hotuba  ndogo katika Sherehe ya kukabidhiwa Leseni Kampuni hiyo kufanya kazi Zanzibar iliyofanyika leo Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa akitoa hotuba katika Sherehe ya kukabidhiwa Leseni Kampuni ya Star Times ya China kufanya kazi Zanzibar iliyofanyika leo Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akitia saini Kitabu cha Wageni kabla ya tukio la kukabidhi Leseni Kampuni ya Star Times ya China leo katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort kulia ni Naibu Waziri wa Redio, Televisheni na Filamu wa China  Li Wei.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa na mazungumzo na Naibu Waziri wa Redio Televisheni na Filamu wa China  Li Wei wa mwisho kuliani kwake kabla ya Sherehe ya kukabidhiwa Leseni Kampuni ya Star Times ya China kufanya kazi Zanzibar iliyofanyika leo Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.PICHA ZOTE NA Hamad Hijja - Maelezo Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Finally! Zanzibar Cable wamepata wapinzani!

    ReplyDelete
  2. Hao wachina wezi tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...