Kipa wa Zimbabwe, Chigova George akiruka juu kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake huku mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars, Hussein Javu akiwania mpira huo.
Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars, Mrisho Ngasa akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Zimbabwe, Eric Mudzingwa katika mchezo wa Kombe la Chalenji uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Zimbabwe imeshinda 2-1. (Picha na Francis Dande).
Shabiki wa kujitolea wa Timu ya Zimbabwe akishangilia kwa furaha baada ya timu ta Taifa ya Kilimanjaro kufungwa leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Makelele ya Julio Kihwelo yako wapi sasa?

    ReplyDelete
  2. Ni matokeo niliyoyatarajia kabisa kutoka na aina ya wachezaji wa kibongo pamoja na akili zao na kutokujitambua kwao.Mwaka huu kombe la kagame litampata bingwa wa halali mwaka jana lilikosea njia.
    Mike

    ReplyDelete
  3. Hii timu yetu ni mshipi usiobebeka. Nashauri, tukampigie magoti macimo arudi. Hii ni AIBUUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  4. Mike nimekupata. Kwani akina samata mbona wakiwa kwenye timu zao huko nje wanafanya vizuri sana, na inakuwaje wakiwa kwenye timu ya taifa hawaonekani? Tatizo liko wapi? Imefika wakati sasa timu ya Taifa ikitoka uwanjani imefungwa au imetoa sare ipelekwe kwa wale wanaume wajulikanao kwa jina la MPs,hiyo itawafanya wakiwa uwanjani wajitume na kuwa na uchungu na Nchi yao TANZANIA

    ReplyDelete
  5. duh tunafungwa na zimbabwe nchi ilikuwa chini kabisa kiuchumi duniani hivi sisi tutamfunga nani?

    ReplyDelete
  6. Wabongo na kubeza tu hawajambo! Leo imekuwa bora maximo.mbona kpnd kile yupo mltaka kumponda mawe? Wabongo hawanaga jema..mnataka nan afngwe?

    ReplyDelete
  7. hao si mashabiki wa kujitolea bali ni wazimbabwe halisi. waandishi mmekuwa wavivu kama wachezaji wa kilimanjaro stars!!? fanyeni utafiti japo mngewahoji kidogo tu, ukweli mngeupata.

    ReplyDelete
  8. Jamani hii mipira ya kutegemea BAHATI hadi lini?...angalia tumecheza na CHAD utmepita na kufuzu kwa bahati licha ya kufungwa, tumecheza tena na hii Zimbabwe tumepita na kufuzu kwa bahati!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...