Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Assah Mwambene akiwa kapiga chunlai yenye rangi ya bendera ya Taifa. Bila shaka vazi hilo ni juhudi binafsi za wabunifu katika kuendeleza libeneke la msako wa Vazi la Taifa ambao mchakato wake umeanza
Home
Unlabelled
vazi la taifa: hapa vipi?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ubunifu mzuri, ila kwanini watanzania hatujui mpangilio wa rangi za bendera ya taifa letu?
ReplyDeleteHapo sawa ila amekosea blue kuiweka juu, nashauri blue iwekwe chini badala ya yellow
ReplyDeleteHii ni nzuri, lakini wasiwasi wangu ni kuwa, hizo rangi zilizo tumika zimekuwa na mrengo wa chama fulani, na kwa mujibu wa waraka wa umma kuhusu mavazi yanayo takiwa kuvaliwa kunako sehemu za kazi, ni vizuri yasiegemee kwenye mrengo wa Chama chochote cha Siasa.
ReplyDeleteUshauri wangu vema yakafanyika marekebisho ili yaweze kuvaliwa sehemu za Kazi kama ofisi za Serikali.
Uchafu mtupu...
ReplyDeletebayaa kwani lazima liwe na bendera ya taifa walau mngechukua rangi mbili hapo blue na kijani. sasa mambo ya kuvaa bendera hapana kwa kweli... na wee mzee wa kubana na koleo hamna kubana hii meseji, huu ni mtazamo wangu.
ReplyDeleteHILI NI VAZI LA CCM SIO TAIFA.... MAIN COLOR KABADILISHE...THAT GREEN STINKS
ReplyDeletenzuri lakini nadhani blue iwe chini ya ufito wa njano na sio kama hivyo ilivyo sasa
ReplyDeletehebu ngoja niwaulize, kwani vazi la taifa lazima liwe na rangi za bendera? mbona nikiwaangalia Wajapan, wa Ghana, Waganda wana mavazi yao ya taifa lakini hayana marangi ya bendera zao? wabunifu hebu kuweni wabunifu bila kuweka hizo rangi please
ReplyDeleteKAMA VILE UMEIBA BENDERA NA KUISHONA SHATI HAIFAI HATA KIDOGO. HAPA UBUNIFU BADO.
ReplyDeleteVazi la taifa ni vizuri liwe zuri na linalopendwa na wavaaji. La sivyo mnapoteza muda bure. Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
ReplyDeleteWanaotafuta vazi watumie ubunifu, akili, maarifa.
Akili za kijasiri amali ndio zitumike siyo za kijamaa
Kazi kwelikweli kama vazi la Taifa ndio hili au liwe bendera. Kunahatari hata kukosekana kwa heshima ya bendera au kuabudiwa kwa vazi hilo.Ubunifu huu haufai endeleeni kuumiza vichwa kwanza sio kukurupuka.
ReplyDeletekwa nini wa2 sio wabunifu?kwani lazima vazi la taifa liwe na bendera ya taifa hebu wa2 wajitahidi kufikiri zaidi.
ReplyDeleteNational dress:
ReplyDeleteWhat is a national dress? http://en.wikipedia.org/wiki/Folk_costume
Reading wikipedia and some other sites the only conclusion I can come to is maybe the committee should be concentrating on more pressing issues like finding ways to raise funds within our society for projects such as clean water in the villages, affordable housing for the masses, dispersing management knowledge for small scale business. I can go on and on with areas such committee (which will take up the tax payers’ money) can be of service.
The issue I have with the traditional dress is vast because I don’t have answers to the following:
Who is a Tanzania?
What is the cultural make up of Tanzania and will it be reflected in the traditional dress??
Looking at Wikipedia, Kanzu is considered a traditional dress; well I wonder what we wore before the Arabs came to town.
What impact, if any, will this traditional dress play in the future for our nation?
Will it be ‘ooooh okay’ and life moves on?
50 years have gone and we are still stuck up in committees that don’t solve the everyday problems our people are facing!!
Does a mother who has to walk 10kms to fetch water from well give a hoot if there is a national dress or not?? Give her running water near her house and she will push the wheel of development even further than she has so far!
We need to change the way we do things and its only ourselves who can do it. When we as individuals can galvanize creativity, the Government will take us more serious and respect our vote and taxes!
CCM TUPU
ReplyDeleteHiyo mbona ni vazi la timu ya yanga. Wanasimba hatuwezi nunua ng'o!
ReplyDeleteNaungana na anony Wed Dec 14, 10:11:00 AM 2011. Kwani vazi la taifa mpaka liwe rangi za bendera ya taifa? Halafu vazi la taifa linapaswa kuwa 'full', yaana juu mpaka chini, sio shati au suruali pekee. Tujitahidi kuwa wabunifu zaidi ya hapa.
ReplyDeleteHaya mambo ya vazi la taifa tumeshachelewa sana. Ilibidi vazi la taifa libuniwe mara tu baada ya kupata uhuru sio kusuburi miaka 50 baadae. Ilikuwa rahisi kufanya hivyo enzi ya chamna kimoja kwani vazi lingebuniwa na chama kingeamua kuwa hilo ndilo liwe vazi la taifa. Hakuna mtu angebisha au kuleta malumbano. Hili sidhani kama linawezekana enzi hizi za utandawazi na uhuru wa kuchagua.
ReplyDeleteKazi kweli kweli! Mbona wabongo tunakuwa wavivu wa kubuni? Suala hili linakuwa gumu kutokana na kupoteza Utamaduni wetu na kuiga utamaduni wa Kimagharibi.Wakiona Mmasai amevaa vazi lake la asili wanakebehi au Mzaramo akicheza Ngoma anaonekana amepitwa na wakati!Lakini mwana Hip hop akipanda Jukwaani huku akifuata sauti yake kutoka ktk CD na kuwaambia watu "PIGA KELELEEEEE!" Watu wanatoa 20,000 fasta kusikiliza "PIGA KELELEEEEE" Mwanzo mwisho.
ReplyDeleteVAZI LA TAIFA SI KITU CHA MPAKA COMMITTEE IKAE BALI NI KITU KINACHOKUJA AUTOMATICALLY KWA WATU WENGI KUPENDELEA KUVAA NGUO ZA AINA FLANI (KAMA UTAMADUNI FLANI HIVI YAANI TUNAKUWA KAMA VILE WAMASAI WANAVYOVAA BASI NA SIE KTK WINGI WETU TUNAKUWA TUNA MAVAZI FLNI). NI NGUMU KWA TAIFA LA VIJANA WENGI WANAVAA MILEGEZO NA SKINI JEANS ALAFU TUSEME TUNALETA VAZI LA TAIFA, HAPA NAONA NI KAZI NZITI MFANO MZURI ONA VIJANA WANAVYOVAA HASA VYUONI ALAFU NDIO UTAPATA JIBU MAANA KAMA VYUONI WANAVAA HIVYO MAANA YAKE KWA ALIE MTAANI ATATEMBEA UCHI KABISA MAANA ROLE MODEL AMBAO NI WANAVYUO WANAVAA KIHASARAHASARA
ReplyDeleteAaaghhhhh huo mrangi wa KIJANI ndo soo lenyewe,SIVAI hata kwa MIKWAJU,hii rangi nikiiona tu basi mie nageuka ghafla,kama nilikua naangalia tv basi hujikuta tu nisha bonya kitufe.
ReplyDeleteWABUNIFU NA WAVAAJI WOTE VIPOFU.
ReplyDeleteVAZI LA TAIFA::::
ReplyDeleteWengi wamefurukuta lakini wazo la kuingiza angalau vionjo vya Mgolole na Lubega havipo kabisa kwa Wabunifu wa vazi la taifa!
Ingawa picha nyingi za historia ya watu wa zamani zimeonyesha wakiwa ktk vazi hilo ,ingefaa wabunifu waanzie hapo na kuendela mbele ili kupata kitu sahihi.
Hilo lirangi la kijani hakifai, HILO NI VAZI LA CCM. AGGRRR!!!
ReplyDeleteKwani vipi?
ReplyDeletePana tofauti gani kubwa ya rangi za Bendera ya CCM na rangi za Bendera ya TAIFA?
HEBU TUBISHANE KWA HOJA ZA KISAYANSI KAMA HAPA CHINI:
___________________________________
(Experiment)
___________________________________
BENDERA YA TAIFA:-
-Nyeusi
-Bluu
-Kijani
-Njano
-Nyeupe(ktk fito)
BENDERA YA CCM:-
-Kijani
-Njano
___________________________________
(Results)
___________________________________
Rangi za CCM zimezaliwa kutokea Bendera ya Taifa!
Mtu unaweza kuthubutu,kujaribu kumkana baba mzazi, lakini mama mzazi hakuna wa kusingiziwa!
Sasa mnabisha nini?, mna akili kweli?...hamjui kuwa CCM ndio SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA?
Wajameni kutokana na Experiment nzito ya Kisayansi na ulinganishi iliyoshushwa na Profesa wa Vitendo hapo juu Mdau wa 24, Kuhusu rangi za nchi kwa kweli asiyeamini jarobio hilo la Sayansi na matokeo hayo ya Sayansi atakuwa si mwenzetu na atakuwa ni mchawi!
ReplyDeletehilo alilovaa jamaa ni vazi la ccm lenye bendera PINDU ya taifa. yaani ameitukana bendera ya Tanzania kwa kuigeuza chini-juu!
ReplyDeleteVAZI LA TAIFA??? RIDICULOUS....!!! LET US THINK TWICE...!!!
ReplyDeleteNashauri wabunifu wapewe nafasi ya kutoa mishono ambayo itawakilisha vazi la taifa.Watu hawataki kuchaguliwa rangi za kuvaa,kinachotakiwa ni mshono tu tofauti na hapo tutavaa uniform nchi nzima.
ReplyDeleteNashauri wabunifu wapewe nafasi ya kutoa mishono ambayo itawakilisha vazi la taifa.Watu hawataki kuchaguliwa rangi za kuvaa,kinachotakiwa ni mshono tu tofauti na hapo tutavaa uniform nchi nzima.
ReplyDelete