Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Allan Mlulla (kushoto aliyesimama) akisoma hotuba ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( wa kwanza kulia walioketi) kufungua semina ya Uhamasishaji na Uelimishaji kwa wadau katika Mkoa wa Morogoro kuhusu masuala ya ushindani , kumlinda mlaji na mapambano dhidi ya bidhaa bandia, iliyofanyika Desemba 15,mwaka huu.
Baadhi ya wadau kutoka Taasisi mbalimbali pamoja na wa Idara za Serikali Mkoani Morogoro wakisikiliza kwa makini mada ya Sheria ya ushindani na Utekelezaji wa Masuala ya Ushindani na Kumlinda Mlaji,ambayo ilitolewa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Allan Mlulla ( hayupo pichani) Desemba 15, mwaka huu mjini hapa wakati wa semina ya Uhamasishaji na Uelimishaji wa wadau katika Mkoa wa Morogoro kuhusu masuala ya ushindani , kumlinda mlaji na mapambano dhidi ya bidhaa bandia.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , Joel Bendera ( aliyekaa katikati ) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa kutoka Taasisi mbalimbali na Idara za Serikali za Mkoa wa Morogoro, jana mjini hapa mara baada ya kufungua semina ya Uhamasishaji na Uelimishaji wa wadau katika Mkoa wa Morogoro kuhusu masuala ya ushindani , kumlinda mlaji na mapambano dhidi ya bidhaa bandia,( wa kwanza kushoto waliokaa ) ni wakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Allan Mlulla, semina hiyo ilifanyika Desemba 15, mwaka huu.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...