Raia wa Ethiopia ,Daniel Chamiso Udude (25) akihojiwa na Mwendesha Mashitaka wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Morogoro, Helmina Foya, Desemba 29, mwaka huu nje ya Mahakama ya Mkoa , baada ya kuahirisha kesi kufutaka na kukosekana kwa mkalimali wa Lugha ya Kihabeshi ambapo kesi imehailishwa hadi Januari 11, 2012.
Raia 14 wa kutoka Ethiopia waliokamatwa katika msitu wa Bwawani,Wilaya ya Morogoro, Desemba 28,mwaka huu wakiwa Mahakamani wakisubiri kusomewa shitaka la kuungia nchini bila kibari wala hati za kusafiria , Raia hao awali , walidhaniwa ni kutoka Somalia , lakini walipohojiwa na Maofisa wa Idara ya Uhamiani Mkoani hapa waligundulika ni kutoka Ethiopia, kama walivyokuywa Mahakamani hapo.Picha zote na John Nditi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Wabongo wanakimbilia Ulaya wenzetu wanakimbilia Bongo.
    Tujihesabu tuna bahati sana ya kuwa watanzania.

    ReplyDelete
  2. Sio kwamba wanaipenda Bongo.wanakimbilia bongo kwa sababu ya kutafuta pasipoti ili waondoke na kwenda nayo nchi za nje kwani pasi za kwao si rahisi kupata visa zanje wameshaharibu sana.ndio maana wanaigeria,wakenya na nchi nyingi za africa wanaona bongo ni mahali rahisi kupata pasi.

    ReplyDelete
  3. Tuache mambo ya kuiga wazungu!
    Kuingia sisi sote ni Wana wa Africa
    Fungueni Mipaka hiyo aina maana yeyote.
    Viongozi wa Africa Amkeni kabisa.
    Kwa hiyo mtu wa Mwanza Asihamie Morogoro. Kama Mu-Ethiopia akija Tanzania na Kuchangia Kukuza Uchumi kwa kuripa kodi, Au Kuanzisha Biashara yake na Kutoa Ajira, Kuingia Mashambani na Kuotesha Mazao kuna Hasara gani??
    Hapa Mwanza watu wengi ni Wakimbizi kutoka Mikoa Mingi ya Tanzania na Wamechangia sana kukuza Uchumi wa Mwanza na Wameleta Maendeleo mengi sana.
    Wachagga, Waasia kutoka Dar es salaam na Tanga, Wapare na Wasomali wamejazana Mwanza. Tunapenda waje hapa.
    Viwanda vya Mwanza vinamilikiwa na Wahindi
    Maduka ya Wachaga na Miradi Mingine Mingi ya Uvuzi na Usafirishaji.

    Watanzania wezangu Msipitwe na Ulimwengu wa Kibiashara na Maendeleo ya Jamii( Globalization)
    Tusije kuwa kama North Korea

    ReplyDelete
  4. hawa wa ethiopia wasiruhusiwe kabisa kwao watu wabaya sana hawa tena wanaona muafrika mwingine sio mtu.

    ReplyDelete
  5. Hao jamaa wapewe tu msahamaha na waruhusiwe kukaa Bongo hata kama ni kwa masharti nafuu.

    Ukiwaangalia nyuso zao utaona tu ni kweli wana shida na wanahitaji msaada.

    ReplyDelete
  6. Wahamiaji haramu wafungwe KWA TIJA MAGEREZANI TANZANIA HUKU WAKITUMIKA KUZALISHA MALI BADALA YA KUTUGHARIMU KWA KULA BURE!

    (VIFUNGO VYA TIJA NA KAZI ZA UZALISHAJI)

    WAFANYIWE TAHTIMINI YA ''HUMAN RESORCE'' KUTAMBUA TAALUMA ZAO ILI WAZALISHE KWA TIJA WAKIWA KIFUNGONI NA KAMA HAWANA WABEBESHWE ZEGE KTK KAZI ZA UJENZI WA MIRADI YA BARABARA ,MABWAWA ,MAJENGO,KUFYATUA MATOFALI,KUVUNJA KOKOTO, KUFUGA NYUKI,KUPAKUA ASALI,KILIMO UFUGAJI NGÓMBE, NA KUCHANA MBAO!

    ReplyDelete
  7. Mimi nafikiri kuna haja mahakama kutoka usingizini, maana miaka nenda rudi watu hawa wamekuwa wanakamatwa na kuletwa mahakamani, na kumekuwa na tatizo sana la wakarimani wa lugha ya kihabeshi, inafikia muda mwingine kesi zinahairishwa kwa sababu hiyo. Hivi kesi hizi zikiendedlea hakimu atawezaje kufanya rekodi ya ushahidi kama hajui lugha husika na hakuna mkarimani anyeielewa lugha hii!! Hivi mahakama inashindwa nini kuwapeleka kozi ya lugha ya kihabeshi baadhi ya mahakimu ili kwamba haki iweze kutendeka kwa hawa ndugu??. Tukumbuke "haki iliyocheleweshwa..."

    katerero73@gmail.com

    ReplyDelete
  8. Hawa wazamiaji WAHABESHI, WASOMALI NA WENGINEO inatakiwa

    WATANDIKWE ''NYUNDO'' VIFUNGO VYA DHABU KALI SANA ILI IWE FUNDISHO WASIPITIE HAPA TZ TENA!

    Hawa Wahabeshi wanapita huku rahisi sahisi TZ kunako hongeka!

    WAHABESHI wanaijua sana ZIMBABWE HAWAKANYAGI KABISAAA HUKO KWA VILE INA HISTORIA YA KUWAADHIBU VIKALI!

    ReplyDelete
  9. Asante sana Anonym wa Fri Dec 30 05:33 AM.Kwanza kabisa Waethiopia ni watu huru sana,sio kama wale wenzetu wa Somalia.Tafadhali waachieni wakae Tanzania.For all Ethiopians we say to you..Welcome to Tanzania,we love you as our brothers and sisters.Jah liveth.
    Kwezai Pitah.

    ReplyDelete
  10. MDau wa Pili umeongea Point wapo kutafuta Passport na Mdau wa 3 Point, Africa lazima tujue kushirikiana na kujuwa tatizo ni kitu gani tuwe na umoja wakutatuwa matatizo yetu sio kuiga WEST au kufuata West nini wanataka Mdau unayesema Ethiopia waruhusiwe Somalia wasiruhusiwe unaonesha kabisa ujinga wako. Kuhusu Somalia kama hatutosaidia kwa nia nzuri ya wenyewe sie wa Africa basi wataendelea kuwa Maadui sababu na sie tunawafanyia uwadui kwa visivyotuhusu kisa American na Euro wanatuambia tupeleke majeshi kwani sie Watumwa wao? John Mangi

    ReplyDelete
  11. Wanapelekwa mahakamani kufanya nini tena? wao ni wahamiaji haramu kutoka Ethiopia, warudishwe kwao Ethiopia mara moja badala ya kuiingiza gharama serikali, kuendesha kesi, kuwalisha na kuwahudumia.Huu uungwana wetu ndio unaotuponza. Ona wenzetu Kenya, hawa wahamiaji wanapita huko Kenya kutoka kaskakzini ya Kenya hadi kusini ya Kenya na kuingia TZ, wenzetu Wakenya wanawaachia na kuwaruhusu waendelee na safari kuja TZ kutupa mzigo kwa kuwa tutawakamata na kuwahoji na kuendesha kesi kwa kuwa wanajua sisi ni waungwana tunafuata sheria. Lazima tulingalie suala hili kwa umakini, tujiulize kwa nini wamepitishwa Kenya wasiwakamate koote huko?!! haiwezekani kusema kuwa mamlaka za usalama za Kenya haziko makini kuliko zetu zikashindwa kuwaona.Ni kwamba wanawaachia waje huku, lazima nasi tukatae kubeba mizigo ya kutupiwa.

    By MZALENDO

    ReplyDelete
  12. waachiwe waishi huru africa kwa nini hatupendani mbona wazungu wenzetu wanapendana wamejiunga wametengeneza EU sisi hatuwezi kuwa huru bila umoja na free of movement.

    ReplyDelete
  13. We umekutana na waethiopia ukiwa nje ya bara la Africa walivyo na dharau kwa Waafrica wengine. Vile nywele zao zinateleza tu wanajiona wao ni juu kuliko wenzao wanakudharau kuliko hata mzungu anavyokudharau. Warudisheni kwao.

    ReplyDelete
  14. HUU NI UPUUZI. MWAFRIKA SIJUI LINI ATAAMKA. UNAWAKATAA NDUGU ZAKO????
    MBONA TUNAWAPAPATIA WAZUNGU??? HALAFU SISI KWA SISI TUNAKATALIANA??
    HAPA ULAYA WALIOKO EU WANA FREE MOVEMENT NA WANMAPENA KAZI WAO KWANZA KABLA YA KUMPA MTU MWEUSI,
    HIVI NI NINI LAKINI? HII NI LAANA??

    ReplyDelete
  15. lakini hawa waabesh wanaonewa bure si wangepewa haki ya ukimbizi? Labda idara ya uhamiaji wangepitia tena kwa makini kutupia macho vibali vya wahamiaji kutoka nchi kama DRC,Burundi,Rwanda ambao wameingia nchini ki aina aina na kujichukulia uraia au pengine ajira,pia wapo wanamuziki ambao kuwepo kwao nchini waliingia kiujanja ujanja,pia kuna makasisi wa dini kutoka nigeria nao wachunguzwe na vibali vyao vifutwe

    ReplyDelete
  16. wauawe tu kutopoteza muda

    ReplyDelete
  17. Iweni watu wa Mungu, Msimuonee mgeni' Hawa ndugu wanahitaji chakula na s magereza, halafu magereza ya Tz ilivyochoka ndo watakufa. Mbona huku hata watz wanajiita wasomali, wakenya na wanapata misaada? msiwape tu passport zetu maana immigration ya Tz kupata passport kwa wazamiaji ni kama kupata mbege moshi ila kupata passport kwa Mtz ni sawa na kupata mbege huku kwa malkia.Waacheni wapige box Tz,

    ReplyDelete
  18. Waethiopia,

    1.Wafanyiwe tathmini hawa watu ni mojawapo ya jamii iliyo kiasili talented sana ktk Afrika wapo, mafundi wazuri wa kazi za ubunifu ktk sekta zote mavazi, majengo na Ufundi Mchundo (Ufuaji Vyuma) kwa waliosoma Historia wanajua hili au Hata ktk vitabu vya Dini Taurati, Quran ,Biblia.
    Wao unaweza kukuta mtu hana Shahada ya Chuo Kikuu lakini kazi yake aifanyayo kwa mkono ipo juu sana.

    2.Wakiwa hawana tija kitaaluma wapelekwe wakachunge ngo'mbe Arusha na Dodoma pia ndio fani yao!

    ReplyDelete
  19. Ninakuunga mkono anony wa kumina tatu kutoka juu. Waethiopia sio watu wenye kuthamini waafrika wenzao. Kweli kabisa wanadharau sana, wanajiona wao wako mbele kama tai. Lakini tatizo hili sio lao hawa walioko nchi za magharibi wakitafuta maisha au sio tatizo la hawa wakimbizi, ila ni la viongozi wao ambao wameruhusu nchi yao kujichanganya sana na nchi za magharibi na kwa hiyo hawana ubinadamu tena. Maana nchi za magharibi hazitaki mtu mweusi amfikilie mweusi mwenzake, furaha yao wao waone: wakimbizi, vita vya wenyewe kwa wenyewe, njaa nk. Kwa maana nyingine marezi ya kitaifa ya kiethiopia huwezi kuyalinganisha kabisa na malezi ya kitaifa ya Ki-TZ. Wa-TZ tusipoteze dira! Tumefundishwa uungwana toka mwanzo: Afrika ni moja na waafrika wote ni ndugu zangu. hili ni jambo kuu sana na tulio wengi kulielewa ni ndoto ya mchana, na kwa kuwa hatulielewi hili basi Afrika tutaendelea kuchukiana na kuwa na matatizo kila kukicha. Mwenyedharau muonyeshe upendo na umsaidie ili umrejeshe katika hali ya utu.
    Anony wa kumi na nne toka juu pia unesema jambo jema. Watu weupe wameturithisha sheria zao kama hizi za uhamiaji lakini wao kwa wao hawazichukulii serious na kuumizana kama sisi weusi tunavyozichukulia. Inawezakana kama anony alivyogusia watu weusi tuna laana na ndiyo hata tukawauza ndugu zetu kama watumwa!Moyo huo bado tunao.AIBU SANA.
    Bloger tafadhali sana kapuni usiniweke.

    ReplyDelete
  20. nendeni kwao mkasikie jinsi weusi halisi mnavyoitwa, (tinkruh balyah).

    ReplyDelete
  21. waachiwe huru kwani maisha popote.. Wakongo, warundi, wanyarwanda, wasomali, wahabeshi. Wote ni watu 2wapeni h4fadhi.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 01, 2012

    Ahmed
    Huu unaweza kuwa ni ubaguzi hali ya juu kwa watanzania,na sikuhizi kuitwa racist ni sawa na kuitwa nguruwe, watu hawapendi jina hilo. lakini Tanzania ndio wanaanza wakati wazungu wanaacha. waethiopia na wasomali wanaopoingia tanzania wanabaguliwa kutokana chuki walionayo kwa wasomali na waethiopia bila ya kosa. juweni kuwa sasa hali inabadilika Somalia na Ethiopia ndia future richest in the world kutokana na mafuta yao na nyinyi mtakuja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...