Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa, katika mkutano uliofanyika siku ya jumatano na kuhudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu, Asha-Rose Migiro, Katika Katibu Mkuu alianisha Mpango Kazi wa miaka mitano pamoja na vipaumbele vitano. baadhi ya vipaumbele hivyo, ni pamoja na uwezeshaji wa wanawake ili waweze kushika nafasi za uongozi za kisiasa halikadhalika kuwawezesha kiuchumi pamoja na kushughulika masuala ya vijana.Kuzihamasisha nchi kupinga kwa nguvu zote ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Kusimamia maendeleo endelevu na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia, mabadiliko ya tabia nchi, kuimarisha utoaji wa huduma za dharura na misaada ya kibinadamu, kuzisaidia nchi ambazo zimetoka katika migogoro na kusimamia suala zima la upokonyaji wa silaha. Mara baada ya mazungumzo yake na Mabalozi,Ban Ki Moon alikutana na waandishi wa Habari ambapo pia alielezea vipaumbele hivyo na pia kutangaza mabadiliko makubwa ya safu ya uongozi katika Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa. Akielezea mabadiliko hayo, Ban Ki Moom aliwaambia waandishi kwamba, Naibu Katibu Mkuu Migiro pamoja na Msimamizi Mkuu wa Ofisi yake Bw. Vijay Nambier wamewasilisha kwake ombi la kuachia nafasi zao ili kumpisha kuunda safu mpya ya wasaidizi wake. Katika mabadiliko hayo wapo pia maafisa waandamizi kutoka Idara na Mifuko ya Umoja wa Mataifa, ambao nao pia wataachia nafasi zao. wengi wao ni wale ambao wamefanya kazi na Katibu Mkuu katika miaka mitano ya kwanza ya uongozi wake.

Na Mwandishi Maalum

New York

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon ametangaza kuwapo kwa mabadiliko makubwa katika safu ya uongozi ndani ya Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya jumatano hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,mara baada ya kuainisha Mpango Kazi na Vipaumbele vya miaka mitano ya mwisho ya uongozi wake. Ban Ki Moon amethibitisha kwamba Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Asha- Rose Migiro atamaliza muda wake akiwamo pia Bw. Vijar Nambiar ambaye ni Mkuu wa Ofisi yake ( Chef de Cabinet).

“ Kama mlivyotangaziwa mwishoni mwa mwaka jana kuhusu mabadiliko yanayotarajiwa katika nafasi za watendaji waandamizi. Ningependa kuongezea na kuwajulisha kwamba, Naibu Katibu Mkuu, Bibi.Migiro na Bw. Vijar Nambiar wamewasilisha kwangu maombi yao ya kutaka kuachia nafasi zao , ili kuniruhusu kuunda timu mpya ya maafisa waandamizi nitakaofanya nao kazi katika awamu ya pili ya uongozi wangu” akasema Ban Ki Moon.

Na kuongeza “ Ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa Naibu Katibu Mkuu, Asha- Rozi Migiro, kwa uamuzi wake huo, na kwa kazi nzuri na ushirikiano mkubwa na usio na shaka wala doa alionipatia katika kipindi chote miaka mitano iliyopita akiwa msaidizi wangu wa karibu.

“ Amenipatia ushirikiano mzuri sana, alinishauri kwa busara na amejituma sana na kwa kuadilifu mkubwa katika kukabiliana na changamoto nyingi zilizoikabili Taasisi hii wakati wa awamu yangu ya kwanza ya uongozi” akasisitiza Ban Ki Moon.

Katibu Mkuu wa UM, akawaeleza waandishi wa habari kwamba, Naibu Katibu Mkuu, Migiro ataendelea kuwapo ofisini hadi mwezi wa sita mwaka huu ili kuratibu na kusimamia kipindi cha mpito pamoja na maandalizi ya Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo Endelevu (RIO+20).

Kwa mujibu wa Ban Ki Moon, pamoja na Migiro kuwasilisha ombi lake wapo pia baadhi ya watendaji waandamizi ambao nao wameonyesha nia ya kuachia nafasi zao ili kupisha menejimenti mpya.

Miongozi mwa maafisa hao ni pamoja na kama ilivyoelezwa awali ni Msimamizi Mkuu wa Ofisi yake Bw. Vijay Nambiar ambaye katika muda muafaka atapewa kazi ya kuwa mshauri wa Katibu Mkuu kuhusu Mynmar.

Watendaji wengine watakaondoka na ambao wengi wao walikuwa katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Ban Ki Moon ni kutoka Idara za Utawala, Maendeleo, Huduma za Mikutano, Habari, Ofisi ya Opokonyaji wa silaha, na Mshauri wa Masuala ya Afrika.

Wengine ni wasimamizi wa Idara za Uchumi za Afrika na Ulaya, waratibu wa mifuko ya maendeleo na Idadi ya watu UNDP na UNFPA. Aidha wamo pia wawakilishi maalum wa Katibu Mkuu wanaohusika na masuala ya watoto katika migogoro ya kivita, na uzuiaji wa mauaji ya kimbali, ambao wanatarajiwa kuachia nafasi zao kati kati ya mwaka huu.

Akaeleza pia kwamba mchakato wa kujaza nafasi Nane zitakazoachwa wazi katika ngazi za ukatibu mkuu msaidizi (Under-Secretary General) umekwisha anza .

Akasema ujazaji wa nafasi hizo ambao utakuwa wa uwazi utazingatia sana sifa na uwezo wa mtu, uwiano wa kikanda na jinsia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Hatujaelezwa vizuri kuhusu kuondoka kwa Dr Migiro katika kazi yake, huenda tutahitaji kufanya nae mahojiano ya kina hasa ili kuweze kupata udani wa nini hasa kimemuondoa! Huenda kulikuwa na sintofahamu kati yake na Ban Ki Moon. Makelele ya kwamba anakuja kujiandaa kwa ajili ya kugombea urais 2015 siyatilii maanani sana!!!!

    ReplyDelete
  2. HONGERA MAMA MIGIRO KWA KUTUWAKILISHA VYEMA KATIKA UN NA DUNIA KWA UJUMLA,NINGEPENDA KUTOA WITO KWA PRESIDENT KIKWETE KUMTUMIA VIZURI KATIKA SAFU ZA DIPLOMA MAMA HUYU.TILISHAONYESHA UDHAIFU WETU WA KUTOMTOMIA BI GETRUDE MONGELA KWA SABABU ZA KISIASA,NA SASA TUTUMIE HII FURSA VIZURI.

    ReplyDelete
  3. Mimi Sijaelewa. Kwa nini Ban Kin Moon naye hakuwasilisha barua ya kuachia ngazi ili kupisha management mpya. I smell a rat!

    ReplyDelete
  4. Inatosha!

    TENDA WEMA WENDE ZAKO USINGOJE SHUKURANI!

    Ni busara kwa mwenye akili timamu kufanya kitu kwa muda maalum na akang'atuka kufanya mambo mwngine!

    ReplyDelete
  5. wewe mchangiaji wa kwanza naye,sasa hapo huelewi nini,kipindi cha uongozi ni miaka mitano,miaka mitano imepita,kwahiyo kunahitajika mabadiliko ya uongozi,kwahiyo mama migiro kwa uadilifu wake tu ameomba aachie ngazi ili kuwapa nafasi wengine,lkn hiyo haizuii kuteuliwa tena kushika wadhifa huo au hata mwingine. Hivyo ndo kiongozi anatakiwa awe,mtu hutakiwi kuwa na uchu wa madaraka.

    ReplyDelete
  6. EHHEHHE
    ANARUDI BONGO RAIS MTARAJIWA HUYO
    WANAUME WA CCM WANAOWANIA URAIS MMEULA NA CHUYA YALE YALE YA MAKINDA

    ReplyDelete
  7. BAN MOON kwa nini asiseme tu kwamba hamekataa kumuongezea Mrs Migoro new contract for next five years. Tuliokua karibu na office hizo tunajua mama alifanya kampeni nza kufa mtu ili kuendelea na term nyingine. But utendaji wake hukukulidhisha.

    ReplyDelete
  8. nyie pigeni kelele tu ati raisi mtarajiwa mara lowassa sijui membe nasema hiviiii rais mtarajiwa ni waziri wa ulinzi hussein mwinyi piga ua huyo ndo atakuwa mgombea wa ccm, ndo mana yuko kimyaaa anabehave kama rais mtarajiwa.

    ReplyDelete
  9. ha haa, jamani sie huku tutamaliza maneno yoooote wenyewe kimyaaa wanatuchora tu. hebu tuangalie maisha yetu na sisi

    ReplyDelete
  10. Mmmmmmh!! nyie naona wengi mnasema Mh. Mwinyi, Mh. Migiro, Mh. Lowassa au Membe ndiyo maraisi watarajiwa. Mi naona kama Mh. Bilal ndiye anayetayarishwa kuwa rais, maana akosi kuuza sura kwenye media, iwe bala au visiwani. Mala utasikia anazindua iki au anakutana na balozi fulani.

    ReplyDelete
  11. Mdau wa 8 hapo juu Fri Jan 27,01:27:00PM 2012

    Naungana na wewe wengine wanahangaika buree tu ,wa mwachie mwenyewe aje Mtoto wa Mzee Ruksa Alhaj ili NEEMA IRUDI TENA!

    ReplyDelete
  12. Mdau wa nane hapo juu Anonymous Fri Jan 27, 01:27:00 PM 2012

    Dunia inashangaza sana, Marekani alitawala GEORGE FITZGERALD BUSH (Baba) akafuatia BILL CLINTON akaja GEORGE WALKER BUSH (Mtoto) watu wa Dunia hawakusema!

    Sasa angalia Syria anatawala BASHAR ASSAD(Mtoto) baada ya HAFEZZ ASSAD(Baba), Marekani na Dunia hawataki, na vivyo hivyo baada ya ALI HASSAN MWINYI akitaka HUSEEIN MWINYI,,,itakuwa kazi WATAKATAA TU!

    ReplyDelete
  13. Kuitumikia kazi sio lazima mpaka ufukuzwe!

    Uwezo na ufanisi wa Uongozi unategemeana na Umri pia kama mjuavyo kadri umri unavyosonga ndio uwezo wa kufikiri na kumbukumbu unapungua, mpo hapo?

    Haya mambo ya kuzeekea na kufia katika Madaraka ni utamaduni wa Afrika, na kwa watu wasio na akili timamu!

    ReplyDelete
  14. Naibu katibu mkuu nakupongeza sana. Nimdpenda sana huu mtandao www.mytodaytv.com kwa video mbali mbali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...