Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe. Gaudentia Kabaka kulia, akiongea jambo na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira, Bibi Edine Mangesho (mwenye miwani) wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipokuwa akiaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa utumishi wa umma (kustaafu), anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira, Bw. Eric Shitindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Bi Mkubwa pamoja na kuwa amestaafu lakini isiwe kumtupa Jongoo na mti wake.

    Hakuna ajuaye Jungu kuu halikosi ukoko, hata akiwa nje anaweza toa mchango kutokana na uzoefu wake.

    Angalau hata katika hadhara na sherehe mbalimbali za Ofisi licha ya Kustaafu kwake aalikwe na ajisikie bado ni sehemu ya Utumishi!

    ReplyDelete
  2. KUSTAAFU:

    Kutokana na mipango ilivyo mibovu kwa Wastaafu, watu huomba waendelee na kazi hadi kifo,,,angalia Bi Mkubwa masikini weee usoni anaonekana bado anatamani awe kazini!

    Kwa Tanzania yetu ni mwiba mchungu suala la ''Kustaafu'' kwa vile unaenda iona joto ya jiwe tofauti na nchi za Wenzetu watu huomba muda ufike wakapumzike na kula raha ya Utumishi wao uliotukuka!

    ReplyDelete
  3. Kwa mazingira ya Tanzania, suala la Kustaafu likimfikia mtu anakuwa kama Mtu aneyesomewa hukumu ya kifo Mahakakani!

    Ushahidi, hebu angalia huyo mama Mstaafu anavyotizama kana kwamba haamini macho yake kuwa Kengele imelia, KIZA KIMETANDA, Bundi anaunguruma na Matumaini ya Maisha yanapotea, na kuwa sasa anarudi Mtaani!

    ReplyDelete
  4. Mungu akubariki Mama Mangesho, its time to go na kuwaachia vijana hapo juu wanufaike pia...

    ReplyDelete
  5. Kweli kustaafu ni tatizo Tanzania lakinikwa mtazamo wangu wa haraka haraka huyu mama anonekana hana shida yoyote, angalia ngozi yake ya mwili it tells you everything!

    ReplyDelete
  6. Wewe Mdau Anonymous wa Wed Jan 25,01:16:00 PM 2012

    Kweli kustaafu ni tatizo Tanzania...anaonekana hana shida yoyote, angalia ngozi yake ya mwili it tells you everything!

    Ahhh acha weee hayo ni matarajio ya muda tu usisikie!,,,tafuta mtu aliyestaafu miaka mitano tu iliyopita muulize usikie!

    Mimi binafsi nimeshaonyeshwa mtu alikuwa Afisa wa Ngazi za Juu (Mwandamizi) Wizara ya Fedha miaka ya Awamu ya Pili, masikini weee Mzee amepigika hata nguo zake pasi hajapiga!

    TATIZO LILE FUNGU LA MAFAO HUWA LINAKWISHA, ILE YA MWEZI HADI MWEZI (Nusu ya uliokuwa Mshahara wako) HAIPANDI TENA,,,WAKATI KAZINI UKIWEPO PANA MFEREJI WA NEEMA ZIKIMIMINIKA!,,,SASA KAMA HATMA YAKE INA UHAKIKA KWA NINI USO WAKE UNAELEZA KILE KITU KILICHO MOYONI?...NI DHAHIRI HATMAA YAKE BAADA YA KUSTAAFU ANAIOGOPA!

    ReplyDelete
  7. Ahhh acheni Wadau,,,Pamoja na ngozi ya mwili wake kung'ara mama anaonyesha wazi kabisa uso wa kupoteza matumaini kwa vile anaelewa wazi kuwa sasa anaelekea kwenye Mlima wa matatizo ya Dunia!

    ReplyDelete
  8. Maazimio ya Utawala (Administrative Policies) hayana maumivu unapokuwa katika Utawala, lakini pindi baada ya Kustaafu machungu ya Sera mtu alizoweka yeye mwenyewe akiwa Kazini yanaanza kujitokeza katika Maisha yake na ndugu zake wakiwa Uraiani!

    Juzi tu, Waziri Mkuu Mstaafu alipelekwa ktk matibabu MOI (Taasisi ya Mifupa) hali aliyoiona kwa Wakata manyasi ingawa yeye alikuwa VIP aliomba Huduma za Afya ziboreshwe!

    Watu wakauliza kwa nini asitoe msisitizo huo wakati bado yupo Ofisini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...