Inasikitisha kwamba Bunge laweza kukaa wiki nzima na kujadili masuala mbalimbali bila kutoa muda kujadili suala la mtikisiko katika sekta ya Afya.
Siku ya kwanza ya Bunge nilisimama kutaka taarifa ya serikali kuhusu mgomo wa madaktari na taarifa hiyo ijadiliwe na Bunge. Spika akalojulisha Bunge kwamba Serikali imempa taarifa na itawasilishwa.
Bunge likaahirishwa siku bila kurejea. Kamati ya Uongozi ya Bunge ilipohitaji taarifa ya Serikali, Serikali haikuwa na taarifa. Kwa hiyo walifanya ujanja ujanja kuzuia mjadala wa mgomo wa madaktari.
Jana wabunge kwa mara nyingine wamesimama kutaka mjadala huu wa dharura. Naibu Spika wa Bunge akatumia sababu za kiufundi kuzuia mjadala. Inawezekana wabunge hawakuwaandaa wabunge kusimama kuunga mkono hoja, lakini ni jukumu la Kiti kuona umuhimu na udharura wa mijadala.
Hii inadhihirisha kwamba sasa Bunge kama Mbunge mmoja mmoja au kwa ujumla wake na Taasisi ya Bunge imekosa mguso na Hali ya wananchi (out of touch).
Hali hii ni hatari sana. Wananchi wanapoona chombo kinachowawakilisha hakitoi nafasi kwa masuala yanayowagusa, watachukua hatua zao wao wenyewe na hivyo kuhatarisha utulivu wa nchi.
Bunge liache shughuli nyingine zote na kutoa fursa ya kupokea taarifa ya serikali kuhusu madai ya Madaktari,kuijadili na kuazimia kwa kuelekeza hatua za kutekelezwa na serikali.
JK vunja Bunge hilo ili tuchague wapya waliopo they arecompletely out of touch. Wengi ni ma Professa etc hawajui umasikini. Good on you Zitto.
ReplyDeleteTuumeshukuru kama mmeliona na nyie, sisi wananchi tulishaliona siku nyingi tunawasubiri 2015
ReplyDeleteMadaktari wanadai miposho kama ninyi wabunge mlivyojiongezea. Tatizo wao hawana mamlaka ya kujiongezea miposho kama ilivyokuwa kwa Wabunge! Na likimalizika la madaktari, kuna walimu na wanafanyakazi wengine. Serikali ya haiwezi kuzuia matakwa ya Bunge, vinginevyo itakuwa ni ya kidikteta. The way foward, badala ya kuitupia serikali lawama, anzeni kwanza kufuta posho mlizojipitishia, au pitisheni sheria ya Bunge kusimamia maslahi ya wafanyakazi wa serikali!
ReplyDeleteBig up, up stairs yako iko sawa zitto,ndio tujue kwamba role na responsilities za wabunge wengi hawazifahamu hawa walio bungeni kwamba ni wawakilishi wa wananchi, hivyo sisi wananchi tunawaomna jinsi wasivyo yuwakilisha vema, but don't worry finally 2015
ReplyDeleteTatizo la wabunge wetu hasa wa CCM lilianza kwa njia walizotumia kuingia bungeni kwa hiyo yanayotokea leo yalitarajiwa.
ReplyDeletekwa viongozi wetu na wabunge hili suali la mgomo wa madaktari halina umiimu sana kwani haliawagusi wao. infact posho zao ni muhimu zaidi kwani hilo linawagusa wao binafsi.
ReplyDeletewabunge na familia zao wakiumwa wanauwezo wa kulipia matibabu yao nchini na nje ya nchi kwa hivyo hakuna sababu ya wao kupoteza pumzi zao kwa huduma ambayo haina umuhimu wowote kwao. IDUME SERIKALI YA UDANGANYIFU
INAFURAHISHA KUONA KUNA BAADHI YA WABUNGE WENYE AKILI NA UCHUNGU NA NCHI HII. NAKUPONGEZA SANA NDUGU YANGU ZITTO KWA KUONA HILO. NI KWELI LIMEKOSA MGUSO (OUT OF TOUCH) KWA WANANCHI WENGI.
ReplyDeleteHapo umenena mbunge wangu,watu badala ya kutilia mkazo vipaumbele, siasa ndo zinashika kasi.Hatufiki kwa kaweli.Kwa mwendo huu!!!
ReplyDeleteDuh!Taarifa fupi sana lakini imebeba ujumbe mrefu na mzito kweli.Kweli wewe Zitto unatisha.
ReplyDeleteWewe Ndugai bado kijana mdogo lakini ndiyo umeiga tabia za wazee wa CCM..unahitaji kuombewa.
WABUNGE:Hata suala la mgomo wa Madaktari mnaliwekea ???Linagusa karibu kila mtanzania bila kujali itikadi za chama,dini,rangi,kabila nk.Inabidi mtuombe radhi sisi wananchi.Mnajiona miungu hey?Subirini 2015, mmeamsha hasira zetu.
David V
Ingawaje simjui huyu jamaa, anaonekana ni kati ya Wanasiasa wachache kama si pekee wanaofanya kazi zilizowapeleka Bungeni. He always on point. The rest are there to collect the money.
ReplyDeleteNafikiri sasa wakati umefika ubunge uwe ni wa kujitolea.
ReplyDeleteKAMA KAZI ZITTO HAPO HAKUNA ANAEMJALI BINADAMU ILA NI MALIPO YAO TU YA NYONGEZA KAMA NINI SIJUI WEWE BASI UWE WA MBELE SIKU ZOTE TAIFA LINAKUSAIDIA WEWE NA WANA CHADEMA WENGINE ILI TUNUSURIKE
ReplyDeletewABUNGE WENGI WAMEINGIA BUNGENI KWA NJIA YA PESA NA HIVYO HAWAWEZI FANYA CHOCHOTE CHA KUWASAIDIA WAPIGAKURA WAO. BADALA YAKE WANAZIDI KUJIONGEZEA POSHO KUCOVER PART YA PESA WALIZOTUMIA KUJIWEKA MADFARAKANI. WAMESAHAU KUA WAO NDIO WANAOTAKIWA KUSIMAMA KIDETE KUTOA MAAMUZI YA NINI KIFANYIKE KUNUSURU MAISHA YA WAPIGAKURA WAO.BIG UP ZITTO.
ReplyDeleteTATIZO NI MFUMO MZIMA WA UCHAGUZI..KIUKWELI KABISA..WABUNGE WETU WENGI NI WATU BOGUS KABISA..TUNAWACHAGUA TU KWA MAZOEA YA CHAMA..KWAMBA AKISHINDA KULA ZA MAONI KWENYE CHAMA BASI HANA MPINZANI TENA..NIMEKUWA ELECTION OBSERVER MARA KADHAA, YANI KUNA NGOMA HATA KUJIELEZA ZENYEWE HAZIWEZI, LET ALONE NATIONAL ISSUES..I ESPECTED THIS..NA MLIOPIGA KULA KWA SABABU YA CHAMA NA SIO MTU MSILALAMIKE..PIGA KIMYA..2015 KITU GANI?.MTAHESABU CHAGUZI NA CHAGUZI MPAKA LINI?
ReplyDeletezitto, siku zote mimi husema...hakuan kwa sasa ama anaejua kazi yake au anaejali na mwenye huruma hapo bungeni zaidi yako zitto..wanakigoma kaskazini siku mtakapomnyima kura zenu huyu kijana, ploeni na aje singida magharibi atachukua ubunge kama inakubalika kisheria...mohamed misanga sioni kazi yake bungeni zaidi ya kula na kuongeza tumbo lake tu...hongera kaka zitto.
ReplyDeleteahsante
hsm