Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa wamesimama mara baada ya Naibu Spika wa Bunge Job Ndugay Kuahirisha kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.Pamoja na mambo mengine yaliyojitokeza wakati wa kuahirisha kikao hicho ni hoja ya Mgomo wa madaktari ambayo iliibuliwa na mbunge wa Kigoma mjini Peter Selukamba ambaye aliitaka serikali kutoa tamko la hatma ya mgomo huo ambapo Naibu spika Job Ndugay aliwataka wabunge kuwa na subira ili Ofisi ya spika ikutane na kamati ya uongozi ya bunge ili kutoa maamuzi hapo kesho kabla ya kuahirisha mkutano huo wa sita.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugay akitekeleza majukumu yake wakati wa Kipindi cha maswali na majibu leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (katikati)akifurahia jambo na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (kulia) maarufu kwa jina la Sugu (CHADEMA) na mbunge wa Kigoma mjini Peter Selukamba (kushoto) nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Edward Lowasa (kushoto) akijadili jambo na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Stephen Wasira (katikati) na mbunge wa viti maalum CHADEMA Leticia Nyerere leo mjini Dodoma.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Jamani Michuzi toka lini Lowassa akawa mbunge wa Longido??????Au mimi cjui??/

    ReplyDelete
  2. bunge linashauri serikali au linaisimamia serikali? kamati ya bunge ya kuongea na madaktari ni wazo zuri, lakini haikupewa time frame ya kufikia muafaka, ndio maana hoja ya kujadili mustakabari wa mgomo na kuahirishwa kwa bunge, haikomi.

    Ni bora bunge hili likaahirishwa hadi pale mgomo wa madaktari utakapo tafutiwa ufumbuzi. Hivi hamjiulizi, ni watanzania gani mnao wawakilisha bungeni ambao maisha yao yapo ktk risk kubwa? Wnakufa, ndugu zao wagonjwa na hawajui wafanyaje ktk kunusuru maiasha yao?

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  3. YAANGALIE MAFISADI....Siku moja watasema....Muulizeni MOBUTU!

    ReplyDelete
  4. EL kanifurahisha juzi kamtuma Mwanri kumwakilisha kwenye harambee kanisani. Mara likaibuka dudu snake meza kuu...wacha Mwanri atimue mbio...Sasa najiuliza;inawezekana EL aliyajua mapema ndo maana akamwagiza Mwanri amwakilishe?...Just thinking noisily

    ReplyDelete
  5. Tumeiona Louis Vuitton.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...