Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa wamesimama mara baada ya Naibu Spika wa Bunge Job Ndugay Kuahirisha kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.Pamoja na mambo mengine yaliyojitokeza wakati wa kuahirisha kikao hicho ni hoja ya Mgomo wa madaktari ambayo iliibuliwa na mbunge wa Kigoma mjini Peter Selukamba ambaye aliitaka serikali kutoa tamko la hatma ya mgomo huo ambapo Naibu spika Job Ndugay aliwataka wabunge kuwa na subira ili Ofisi ya spika ikutane na kamati ya uongozi ya bunge ili kutoa maamuzi hapo kesho kabla ya kuahirisha mkutano huo wa sita.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugay akitekeleza majukumu yake wakati wa Kipindi cha maswali na majibu leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (katikati)akifurahia jambo na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (kulia) maarufu kwa jina la Sugu (CHADEMA) na mbunge wa Kigoma mjini Peter Selukamba (kushoto) nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Edward Lowasa (kushoto) akijadili jambo na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Stephen Wasira (katikati) na mbunge wa viti maalum CHADEMA Leticia Nyerere leo mjini Dodoma.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.


.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Jamani Michuzi toka lini Lowassa akawa mbunge wa Longido??????Au mimi cjui??/
ReplyDeletebunge linashauri serikali au linaisimamia serikali? kamati ya bunge ya kuongea na madaktari ni wazo zuri, lakini haikupewa time frame ya kufikia muafaka, ndio maana hoja ya kujadili mustakabari wa mgomo na kuahirishwa kwa bunge, haikomi.
ReplyDeleteNi bora bunge hili likaahirishwa hadi pale mgomo wa madaktari utakapo tafutiwa ufumbuzi. Hivi hamjiulizi, ni watanzania gani mnao wawakilisha bungeni ambao maisha yao yapo ktk risk kubwa? Wnakufa, ndugu zao wagonjwa na hawajui wafanyaje ktk kunusuru maiasha yao?
Kibanga Msese
YAANGALIE MAFISADI....Siku moja watasema....Muulizeni MOBUTU!
ReplyDeleteEL kanifurahisha juzi kamtuma Mwanri kumwakilisha kwenye harambee kanisani. Mara likaibuka dudu snake meza kuu...wacha Mwanri atimue mbio...Sasa najiuliza;inawezekana EL aliyajua mapema ndo maana akamwagiza Mwanri amwakilishe?...Just thinking noisily
ReplyDeleteTumeiona Louis Vuitton.
ReplyDelete