Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa, akitowa nasaha zake kwa Wanachama wa CCM wa Jimbo la Uzini katika Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni katika viwanja vya Skuli ya Uzini.
Katibu Mkuu wa CCM Mkama, akiwahutubia Wanaccm wa Jimbo la Uzini katika Mkutano wa Kampeni.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, akitowa maelezo ya Uzinduzi wa Kampeni ya Jimbo la Uzini.
Mbunge wa Jimbo la Uzini Mohammed Seif Khatib, akiwahamasisha Wananchi wa Jimbo lake katika Mkutano wa Kampeni uiliofanyika katika Viwanja vya Skuli ya Uzini.

Rais Mstaafu Wa Zanzibar na Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume akimnadi mgombea wa Kiti cha Uwakilishi jimbo la Uzini ndugu Mohd Raza Huko katika kiwanja cha Mpira Uzini hapo jana

Mgombea wa Uwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohd Raza akihutubia wananchi pamoja na wanachama wa chama cha Mapinduzi baada ya kutambulishwa rasmi kwa wanachama hao hapo jana Kuliani kwake ni Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume

Rais Mstaafu Wa Zanzibar na Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume akibadilishana mawazo na Makamo Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Pius Msekwa huko katika kiwanja cha mpira Uzini wakati wa kuzinduakampeni ya kugombea Uwakilishi wa jimbo hilo.

Kijana wa chipukizi Zawadi Mbaraka akimvisha Skafu Rais Mstaafu Wa Zanzibar na Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Amani Karume baada ya kuingia katika Uwanja wa Mkutano wa CCM kwa ajili ya kuzindua kampeni ya chama hucho huko Uzini wilaya ya kati Unguja.

Vijana wa umoja wa waendeshaji mapikipiki wa chama cha Mapinduzi wakimsindikiza mgombea wa Uwakilishi wa chama hicho junbo la Uzini Mohamed Raza katika uzinduzi wa kampeni wa kuwania kiti cha Uwakilishi Jimbo hilo hapo jana.

Wananchi mbalimbali pamoja na wakereketwa wa chama cha CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika huko katika kiwanja cha Uzini Zanzibar kwa ajili ya kumnadi mgombea wa Uwakilishi wa jimbo hilo ndugu Mohd Raza.Picha na Yussuf Simai-Maelezo-Zanzibar
Magambaz in action!
ReplyDeleteHawa watu sidhani kama wanafikiria au wanakubali kwamba siku moja nchi itakuwa chini ya chama kingine. Kwa sababu hiyo watahakikisha kwa nguvu zote hasa za dola jambo hilo halitokei!!!
ReplyDeleteJamani jamani jamani, hizi khanga, kofia, T-shirt na vilemba ndivyo vimetufikisha hapa leo. Hivi ni lini ulienda dukani ukapunguziwa bei kwa ajili ya khanga, au tshirt uliyovaa??? Watanzania tuache kuuza utu wetu kwa vitu vya kitoto. Mtu kama hafai usimchague kisa kakupa khanga au pilau.Nawatakieni kampeni za amani na utulivu.
ReplyDeletejaribu kuedit kabla hujachapisha spelling za botswana ni hizi
ReplyDeletehaya majina mengine. kidogo nidhani tupo Congo-kinshasa.
ReplyDeleteJimbo la uzini, skuli ya uzini,wilaya ya mchamba wima.Zanzibar mpo juu.hahahahaha.
hiki ndio chama
ReplyDelete