Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa, akitowa nasaha zake kwa Wanachama wa CCM wa Jimbo la Uzini katika Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni katika viwanja vya Skuli ya Uzini. 
 Katibu Mkuu wa CCM Mkama, akiwahutubia  Wanaccm wa Jimbo la Uzini katika Mkutano wa Kampeni.  
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, akitowa maelezo ya Uzinduzi wa Kampeni ya Jimbo la Uzini.
 Mbunge wa Jimbo la Uzini Mohammed Seif Khatib, akiwahamasisha Wananchi wa Jimbo lake katika Mkutano wa Kampeni uiliofanyika katika Viwanja vya Skuli ya Uzini. 
Rais Mstaafu Wa Zanzibar na Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume akimnadi mgombea wa Kiti cha Uwakilishi jimbo la Uzini ndugu Mohd Raza Huko katika kiwanja cha Mpira Uzini hapo jana
Mgombea wa Uwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohd Raza akihutubia wananchi pamoja na wanachama wa chama cha Mapinduzi baada ya kutambulishwa rasmi kwa wanachama hao hapo jana Kuliani kwake ni Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume
Rais Mstaafu Wa Zanzibar na Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume akibadilishana mawazo na Makamo Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Pius Msekwa huko katika kiwanja cha mpira Uzini wakati wa kuzinduakampeni ya kugombea Uwakilishi wa jimbo hilo.
Kijana wa chipukizi Zawadi Mbaraka akimvisha Skafu Rais Mstaafu Wa Zanzibar na Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Amani Karume baada ya kuingia katika Uwanja wa Mkutano wa CCM kwa ajili ya kuzindua kampeni ya chama hucho huko Uzini wilaya ya kati Unguja.
Vijana wa umoja wa waendeshaji mapikipiki wa chama cha Mapinduzi wakimsindikiza mgombea wa Uwakilishi wa chama hicho junbo la Uzini Mohamed Raza katika uzinduzi wa kampeni wa kuwania kiti cha Uwakilishi Jimbo hilo hapo jana.
Wananchi mbalimbali pamoja na wakereketwa wa chama cha CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika huko katika kiwanja cha Uzini Zanzibar kwa ajili ya kumnadi mgombea wa Uwakilishi wa jimbo hilo ndugu Mohd Raza.Picha na Yussuf Simai-Maelezo-Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Magambaz in action!

    ReplyDelete
  2. Hawa watu sidhani kama wanafikiria au wanakubali kwamba siku moja nchi itakuwa chini ya chama kingine. Kwa sababu hiyo watahakikisha kwa nguvu zote hasa za dola jambo hilo halitokei!!!

    ReplyDelete
  3. Jamani jamani jamani, hizi khanga, kofia, T-shirt na vilemba ndivyo vimetufikisha hapa leo. Hivi ni lini ulienda dukani ukapunguziwa bei kwa ajili ya khanga, au tshirt uliyovaa??? Watanzania tuache kuuza utu wetu kwa vitu vya kitoto. Mtu kama hafai usimchague kisa kakupa khanga au pilau.Nawatakieni kampeni za amani na utulivu.

    ReplyDelete
  4. jaribu kuedit kabla hujachapisha spelling za botswana ni hizi

    ReplyDelete
  5. haya majina mengine. kidogo nidhani tupo Congo-kinshasa.
    Jimbo la uzini, skuli ya uzini,wilaya ya mchamba wima.Zanzibar mpo juu.hahahahaha.

    ReplyDelete
  6. hiki ndio chama

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...