Mdhamini wa timu ya Yanga ya Jangwani jijini Dar es salaam Mama Fatma Karume akizungumza katika hafla ya timu hiyo kuimiza miaka 77 tangu kuanzishwa kwake iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Peacock na kuhudhuriwa na wanachama na wadau mbalimbali wa mpira wa miguu, huku mgeni rasmi akiwa Dk. Fenella Mkangara Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na michezo anayeonekana kulia katika picha kushoto ni baadhi ya wazee wa Yanga. Mama Fatma Karume alisema Yanga ni mzee wa miaka 77 lakini katika michezo anaweza kukimbia kwa kasi ileile ya kimichezo, hivyo akamuomba mola ili klabu hiyo izidi kupata mafanikio katika michezo.
Mgeni rasmi katika hafla ya timu ya Yanga kutimiza miaka 77 Dk Fenella Mkangara Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na michezo akizungumza katika hafla hiyo, huku Mwenyekiti wa Yanga Loyd Nchunga akifurahia jambo, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sadik Meck Sadik na kushoto ni mdhamini wa Yanga Mama Fatma Karume.
Katibu Mkuu wa Yanga Selestini Mwesigwa akipiga mamombi kabla ya kuanza kwa hafla hiyo kulia ni George Kavishe Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro na kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Yanga Loyd Nchunga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sadik Meck Sadik.
Wadau kutoka Peacock Hotel wakijadiliana jambo ili kuhakikisha sherehe hiyo inafana zaidi.
Ancle Hashim Lundenga kulia ndani kama unavyomuona akiwa ametulia kitiniKutoka kulia ni Kocha mkuu wa Yanga Kostadin Papic shabiki mkubwa wa Yanga Emmanuel Mpangala na Kocha msaidizi wa timu hiyo mwenye (Mzuka Mwingi) Fred Felix Minziro wakifuatilia mambo mbalimbali katika hafla hiyo.
Kulia ni wanachama wa Yanga Mh. Mudhihir Mudhihir kulia na Jaji Mkwawa wakiwa katika hafla hiyo jana uziku.
Mashabiki ha wa pia walikuwepo kuipa tafu klabu yao.
Kundi la THT likitumbuiza katika hafla hiyo
Hii ndiyo mandhari ya ukumbi inavyoonekana katika picha.
(KWA HISANI YA FULL SHANGWE BLOG)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. aIBU! Miaka 77 bila ya hata mara moja kutwaa kombe la Afrika!

    ReplyDelete
  2. Papic mbona kachukia anaona Yanga wanasherehekea nini?Uongozi bomu mambo hayaendi inavyotakiwa na ukijiuliza sherehe hii ni ya nini hupati jawabu.

    ReplyDelete
  3. Miaka 77 hakuna maendeleo kisoka halafu mnsherehekea nini. Hiyo ni mbinu ya kuidhinisha matumizi mabaya ya fedha za klabu. Viongozi wanachofikiria ni kula kile kinachopatikana na si vinginevyo.

    ReplyDelete
  4. wachezaje mbona hatujawaona katika sherehe au hawahusiki??

    ReplyDelete
  5. Ukweli ni kwamba Viongozi wetu kuanzia matawi mpaka taifa wamekosa uzalendo kwa Timu yetu. na pia ni dhahiri ya kuwa hauwajali wanachama na wapenzi wake! inatia aibu na inasikitisha sana miaka 77 wanaandaa sherehe kificho. katika hali ya kawaida wangetangaza hadharani utaratibu ambao unatumika kuandaa sherehehii. ili mwanachama au mpenzi wa Yanga aweze kuhudhuria kwa kuwa ni haki yake anatakiwa afanyeje au achangie nini! hata hivyo katika sherehe hiyo wametumia shilingi ngapi kwa kuwaalika wageni wangapi? na wamekusanya shilingi ngapi? je, wangetengeza T Shirt, khanga, vitenge, au vishika funguo hata 2,000 tu wangepata shilingi ngapi? je si njia mojawapo ya kupata mapato na kuwafanya wanachama na wapenzi kuwa pamoja? hawajajifunza kwa serikali ilivyoandaa miaka 50 ya Uhuru? nasikitika sana nilipiga kura lakini kura zangu zilipotea bure! wakati wengine wanasusa kupiga kura wakati wa Uchaguzi niliwaona wajinga, hawana akili na hawaitakii mema Yanga. kumbe mimi ndio bwege! Viongozi wetu Yanga ebu jitahidini kuleta mabadiliko yenye tija kwa wanachama. Uongozi wa kiujanja kama mtu fulani aliyefungwaga jela akatoka kwa msamaha anavyowaongoza wenye mikia. kiukweli tumechoka porojo na hii hali iliyopo. wakati mwingine unaweza kujuta kuwa mpenzi wa mpira lakini kwa kuwa Mungu kaleta neema kama hii ya kuwa na Timu nzuri kama Yanga unajipa moyo labda baadae itakuwa shwari! ukiangalia picha hao wageni walioalikwa unaweza kucheka kwa kweli! sijui wametumia vigezo gani! dah! NCHUNGA na wenzako iokoeni Yanga jamani. Umoja na Mshikamano wetu viko wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...