Kwanza napenda kuwapongeza wana Chipolopolo kwa ushindi.
Nimejaribu kufanya uchunguzi wa haraka haraka as of 2010, Tanzania is doing better economically compared to Zambia, Sasa naomba mnisaidie nikitu gani watanzania kinatufanya hata tusiweze kuqualify for the AFCON Finals!!!!!.
Hata Sudan jamani..with all due respect to Sudan , wana kila aina ya matatizo lakini wamequalify and played very well.
Kulikoni Tanzaniaaaaaa???????????????
Natoa Hoja..
Mdau
Tanzania
Nimejaribu kufanya uchunguzi wa haraka haraka as of 2010, Tanzania is doing better economically compared to Zambia, Sasa naomba mnisaidie nikitu gani watanzania kinatufanya hata tusiweze kuqualify for the AFCON Finals!!!!!.
Hata Sudan jamani..with all due respect to Sudan , wana kila aina ya matatizo lakini wamequalify and played very well.
Kulikoni Tanzaniaaaaaa???????????????
Natoa Hoja..
Mdau
Tanzania
Sisi hatuna kocha.alikuja mzushi Maximo tuliwekeza pesa nyingi lakini akawa mtu wa Majungu kuwachukia wachezaji wa Simba kama kina Boban ambao wangetufikisha huko walikofika Zambia.
ReplyDeleteZambia wana kocha makini alijua kuwa Ivory Coast ni warefu na wana maumbo basi soka likawa la chini chini.
Soka letu limefika hapa kuwa na watu kama maximo na viongozi wa TFF ambao si wapenzi wa mpira na hawajui kitu zaidi ya kula pesa.
mtu kama Katibu mkuu wa TFF hana vision wala mpango mkakati na si mtu wa Mpira so long anapata pesa basi.
Afisa Habari wa Tff sio mtu wa Mpira.hali hiyo hiyo nenda kwa Mwenyekiti wa Taswa na Katibu wake. mwenyekiti wa Taswa hana kitu kichwani na hana malengo zaidi ya kutumia platform hiyo kutengeneza deal za Mjini.
mfano kwenye fani ya habari kuna ripota ambaye kazi yake ni kuripoti tu na kuna Jounalist ambaye anachambua habari anafanya analysis.
sasa hao Maripota ndio wamejaa kwenye vyama vywetu vya michezo.ukija kwenye Club zetu wamejaa watu ambao si wa Mpira wanatumia vilabu kwa mambo yao.tunataka watu kama Mzee mangara Tabu,mohamed Kassanda alikuwa Simba na Mzee Bwamchawi walikuwa hawana shule ya darasani lakini walikuwa na informal education ambayo ni silaha kali kuliko Formal.
mdau Jongo wa Kisiju.
Yule namba tano wa Zambia aliyevaa jezi namba 13 kiboko sana.Drogba kwisha fitna yake atamroga Torres tu si Mwenee wa Zambia.pia kamati ya ufundi ya Zambia inabidi tukaitafute itudaidie maana hata uwe na kipa mpira unatoka.
ReplyDeleteMdau jongo wa Kisiju-Mtalaam wa soka.
MADA NZURI SANA MDOGO WANGU. KAMA MAENDELEO YA KIUCHUMI YANGEKUWA NDIYO MAFANIKIO YA MPIRA WA MIGUU, BASI MAREKANI INGECHUKUWA MAKOMBE YOTE YA DUNIA. KAMA IDADI KUBWA YA RAIA KATIKA NCHI INGEKUWA NDIYO KUJUA KUUCHEZA, BASI WACHINA WANGEFUNIKA.ETHIOPIA WANA UTAPIAMLO MKALI KWA KUKOSA CHAKULA NA BAADHI YAO WANAOMBA UKUMBIZI TANZANIA, LAKINI WANA MADEGE MAKUBWA YANAYORUKA DIRECTLY KUTOKA MAREKANI NA CHINA HADI ADIS-ABABA KILA SIKU. KAMA UTAJIRI WA MAFUTA NDIYO MPIRA WA MIGUU, BASI UAE WANGEENDA KUFANYIA MAZOEZI MWEZINI. MPIRA NI MAANDALIZI TANGU UTOTONI KWA-NADHARIA, VITENDO, NA BALANCED DIETY. NI HAYO TU MDOGO WANGU, SIYO UCHAWI, UTAJIRI, IDADI KUBWA, WALA SAYANSI YA MAROKETI.UKINDA VIJIWENI KESHO, WATANZANIA TUTASIMULIA MPIRA WA LEO KAMA VILE TULIKUWEPO UWANJANI. HIVYO NDIVYO TULIVYO. TUNAJUA KUUCHEZA KWA MIDOMO.
ReplyDeletekwetu bongo land ufisadi nambari one halafu ndiomengine kama mashindano ya ufisadi basi TZ Tutakua nambariwani duniani. lakini soka kalagabaho
ReplyDeleteHadi hapo udokozi na wizi wa pesa za kuendeleza vipaji vya soka nchini utakapo patiwa ufumbuzi. Nchi yetu ni kama imerogwa maana ni wizi mtupu kila sehemu. nasikia FIFA huwa wanawapa pesa TFF kila mwaka kwa ajili ya kuendeleza soka lakini waulize leo hii, chuo cha soka kwa vijana watakao kuwa akina Drogba wa kesho kiko wapi?!! Hamna! Wao mipango yao ni ya leo na kesho halafu na matumbo yao basi. Mie nilisha kata tamaa na Tanzania kwa kila jambo, hakuna tunaloliweza.
ReplyDeletejamani kweli hili jambo tusilifanyie mzaha, miaka takribani ishirini iliyopita wazambia walipoteza timu nzuri sana na hii leo wamedhihirisha makubwa na kikosi kingine kabisaa. Sasa tuangalie tatizo letu lipo wapi au ni nani anaesababisha hili tatizo la watanzania kuwa kichwa cha mwendawazimu.WATANZANIA NA VIONGOZI WETU TUTILIE MKAZO JAMANI MICHEZO sio tu mpira wa miguu tuweke mkazo katika michezo yote leo hii waarabu wanatimu za mashua mpaka wanawake wanashiriki sasa sie tatizo ni nini?Tumekalia POMBE TUU NA UZINZI KWENYE MAGESTI NA KUCHUKULIANA WAKE ZA WATU ebu tubadilike jamani.
ReplyDeletetumejifunza kuwa ipo haja ya kumrudisha Maxime Maximo!
ReplyDeleteHakuna chengine isipokua ufisadi na roho mbaya tu. Mchezo au michezo ni gharama. Ili kupata mafanikio lazima serikali ikubali kutumia pesa za kutosha juu ya michezo na vile vile wana michezo wathaminiwe kwa maneno na vitendo. Wakati wa michezo kua hobby umeshapitwa na wakati, sasa michezo ni carrer
ReplyDeleteMdau,
ReplyDeleteSoka si suala la kimaendeleo ya kiuchumi yanayofanya nchi ifanye vyema kwenye mashindano makubwa. Kama ingekuwa ni hivyo unavyoona kuwa Tanzania wapo kiuchumi vizuri kulikoni Zambia (japo mimi naona Tanzania tumechapika zaidi), basi nchi tajiri duniani kama vile Marekani na nyinginezo zinekuwa zinachukua kombe la dunia kila linapofanyika.
Jiulize nchi kama vile China yenye uchumi mzuri na idadi ya watu kama bilioni moja, haijawahi kuchukua kombe la dunia...iweje wao washindwe kuwa na wachezaji 11 wazuri kati ya watu bilioni moja? Hivyo fahamu mpira ni zaidi ya suala la uchumi, idadi ya watu nk
Ukiangali kwa upande wa Zambia, nidhamu na maamuzi yamewasaidia sana. Wachezaji wengi wa Kitanzania wanapokuwa kwenye mashindano ya kimataifa mfano timu ya taifa wengi wao hawana nidhamu ya kimpira, maamuzi ya msingi, kujua wanafanya nini pale kwa taifa lao nk. Kwenye hii miaka ya karibuni kuna kaunafuu kidogo, ila bado sana.
Soka la Tanzania ni la mdomoni mno na si la mipango ya kisayansi. Wachezaji wengi tangu wanaanza wadogo wanacheza hadi wanakuwa wakubwa hawajawahi kuwa na professional coach, hilo linawafanya wengi wao wanapofika timu kubwa hawaoni umuhimu wa kocha.
Wachezaji wengi wafahamu mpira ni ajira yao. Hivyo ni jukumu lao wenyewe kwenda gym, kufanya mazoezi binafsi, kujipanga ipasavyo kabla ya kuambiwa na kocha...hiyo ndio siri ya mpira wa sasa na si uchawi na longolongo
MAKULILO
Ni kweli kabisa, hili swali ni zuri na muhimu kujiuliza.
ReplyDeleteKuna mambo mawili,mosi, Tanzania zaidi tunapenda ushindi wa magazetini na pili, kuna tatizo la wadau vigogo kuwapotosha makocha kwa kutaka kuchagua wachezaji wanaowapenda wao sio kwa kiwango bali asilimia kubwa huwa kuna ka'ugonjwa cha Uyanga na Usimba ndani yake!
Kwa ushindi wa magazetini, ninamaanisha jinsi tunavyopenda kuongea bila matendo na kuwafagilia wachezaji hadi wao wenyewe wanaona ndio basi tena wameshakuwa mastaa!! Hii inawapotosha wachezaji na inajenga udhaifu katika mlolongo mzima wa kuchagua wachezaji kwani kuna wengine huwa wakichaguliwa, kutokana na kujiona tayari wamekuwa mastaa basi hata mazoezini inakuwa "ishyu" kwenda. Wakati ukizingatia hali halisi, ni asilimia ndogo ya wachezaji hao wameshafanikiwa kwenda nje japo kuonyesha uwezo wao.
Kuhusu wadau vigogo kuwapotosha makocha, sio tu Tanzania bali nchi za Afrika huwa tuna tatizo hili. Zambia hao hao ni mfano mzuri, kwani tayari kuna wadau walikuwa wanalalamika kuwa kocha anakosea kupanga wachezaji. Ni kweli, wadau ndio wenye uwezo wa kumpa mwangaza kocha lakini usiwe wa kumpotosha bali uwe mwangaza wa kweli na sio kwa upendeleo. Kocha wa Zambia amekuwa na msimamo thabiti na ndio maana hakutetereka na hao vigogo. Aliwajibu kuwa atachagua mchezaji ambae yupo fiti mazoezini na si vinginevyo, kwani tayari lawama za kwa nini hawapangi wachezaji maarufu zilikuwa zinamuandama. Sisi Tanzania, zaidi inaonekana wazi kabisa, asilimia kubwa ya wachezaji ni Simba ama Yanga, na kwa kiwango kikubwa hutokana na shinikizo la wadau vigogo. Wachache sana hutokea timu nyingine, kwa hiyo sana sana inakuwa kama kuunga timu moja ya mafahari hao wawili, ambao mara kwa mara tumekuwa tukiwaona hawafurkuti katika mashindano ya klabu Afrika, mara nyingi hatua ya kujidai ni mzunguko wa pili!!
Itambulike Taifa Stars inapofungwa, wapenzi wa soka tunapata uchungu sana moyoni, ukizingatia kuna timu zilizofuzu kama mdau ameitaja Sudan, mimi naongeza Niger (ambayo inasemekana ni nchi ya kwanza ama ya pili kwa umasikini duniani).
Timu ichaguliwe kwa kuangalia viwango bila upendeleo na wadau vigogo wajue wanawakilisha Taifa na sio kuwakilisha ushabiki wao binafsi!!!
Hongera sana Chipolopolo!!! Mmetutoa Afrika Mashariki kidedea!!!
mpira wetu tunacheza kwa mdomo zaidi. hakuna mtu aliye serious labda Kikwete peke yake. tubadilike tuwajali wachezaji wote bila ubaguzi tutafanikiwa.
ReplyDeleteWenzetu wameamua kuacha longolongo, wamewekeza kwa madogo! sisi kwetu imeabaki maneno! Huyo Tenga kabaki kuwa mwanasiasa. Imenifanya kweli kuamini kasoma lakini hana tunu ya uongozi na ndio maana hata kule kampuni ya Landrover aliyokuwa akiiongoza haikufanya vema!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteTulichojifunza Tanzania:
ReplyDeleteKwanza HONGERA SANA KWA JIRANI ZETU ZAMBIA!
Wametutoa Kimasomaso kwa kutupa muamko ya kuwa inawezekana!
Ugonjwa mkubwa unaokabili maendeleo na mafanikio ya Soka Tanzania licha ya nafuu ya kiuchumi kama Mdau unavyonukuu ni ,ugonjwa wa SIASA zaidi kuliko SAYANSI hadi kwenye Soka!
MARA ZOTE SIASA NI TAALUMA YA MASLAHI ZAIDI KULIKO MAENDELEO, KITU AMBACHO KINAANZIA KUTOKA KWENYE SHIRIKISHO LETU TFF HADI KATIKA VILABU VYA TIMU NA TASNIA YA SOKA KIUJUMLA!
WEWE ANGALIA DIRA,SERA, NA MWELEKEO WA MIPANGO MINGI YA TFF, VILABU VYA TIMU ZIPO KTK MASLAHI ZAIDI KULIKO MAENDELEO!
MARA ZOTE SIASA HUZAA UBABAISHAJI IKIINGIZWA POPOTE HATA MSIBANI!
Unaposema "doing better economically" inaelekea unatumia vigezo vya makaratasi vilivyojaa upotoshaji tofauti na hali halisi. Suala moja kubwa lenye tofauti kati ya TZ na nchi nyingine ni ukosefu wa uzalendo kwa viongozi wetu tangu alipoondoka baba wa taifa.Ukijiuliza kwa nini hali ya umaskini TZ bado ni mbaya nadhani jibu utalipata maana viongozi wana fedha nyingi kuliko serikali.
ReplyDeleteSiasa..... shida ni pale siasa inapotaka kutumiwa kila mahali, hata penye uhitaji wa kitaalamu....
ReplyDeleterushwa, kusajili vijana wa wazee tunaowajuwa.
ReplyDeleteMdau wa kwanza hana akili timamu kwani asili mia 99.9 ya wachezaji wa Simba na Yanga si wachezaji kweli Bali ni wachawi wa ukweli wako benchi. Maximo Kama kocha hushinda na wachezaji uwanjani kupanga formation na mbinu za ulinzi ila wale wachezaji hawafundishiki kutokana na kutokuwa na vipaji vya ukweli. Mpira wa TZ so mpira wa mtu mwenye akili timamu kufuatilia, angalieni tu jinsi Simba na Yanga wachezavyo, si ujinga tu ule? Sasa kwa mtaji huu nyie mnadhani tutafika wapi, wenzetu wanapiga hatua sie bado tunakalia Simba na yangu timu zinazoua mpira wa Bongo. Tuachane na ushirikina tukuze vipaji vya ukweli tusipoangalia tutabaki na mambilikimo Kama kina Ngassa wasiofundishika, wakati ndiyo huu.
ReplyDeleteKwa kweli wengi tumegusia tatizo la soka letu lakini mimi naona kwanza tutafute sababu za kisayansi za kukosa mafanikio upande wa soka na si kutooa sababu za juu juu
ReplyDeletemfano:
1. Awali tuliambiwa tatizo ni kina Alhaji Ndolanga na wenzake ambao sio watu wa mpira ndio maana soka halikuwi wakaja Tenga na hao 'watu wa mpira' lakini naona hamna jipya
2. Tukasema wanaacha makocha wa nyumbani wanakumbatiwa wakigeni, challenge wakapewa Mkwasa na Jamhuri - mambo yakawa yale yale.
4. Tuasema bila kina Boban hatuwezi kushindwa , Boban akaitwa na kilichotokea sina haka ya kukirudia
3. Kwa saa simsikii hata mmoja akizungumzia soka la wanawake , je mafanikio ya timu ya soka ya wanawake ni kutokana na maandalizi mazuri au ni bahati tu , nani anatafakari namna bora ya kupata timu nyingine baada ya hii , jibu hakuna na hata TFF najua hawajishughulishi kutafuta jibu .Sie ni hodari wa kusifia mavuno mazuri ya matunda pori yaliyojiotea na kukua yenyewe kwa kudura za mungu .Huu ni ushuhuda mwingine wa jinsi tunavvyoshangilia tusichoapanda .
wadau mnaweza kuendelea
Wasiwasi
Dsm
Nina hakika tatizo lipo na hatulijui na hili ni hata kwa viongozi wetu wa kitaifa , wanadhani shule ni majengo na idadi kubwa katika udahili si vifaa ba walimu bora na wenye ari
Jongo wa Kisiju ni mnafiki na asiyefahamu swali la mdau!
ReplyDeleteUnaanza kuchambua mtu na mtu ili iweje? Pia si vyema ukaichambua taaluma ya mwenzako bila kujua unachokisema eti kuhusu reporter ba journalist! Inaonekana unafanyia kazi sana stories za vijiweni mtu kama wewe yaonekana hata familia yako inakushinda kuiongoza!
HEE HEE...KABLA YA KUANDIKA MAONI YANGU NIMEPITIA MAONI YOOTE NENO MOJA BAADA YA JINGIGINE..UJUMBE MKUBWA AMBAO UNAJIRUDIARUDIA NI KWAMBA KUMBE UWEZO TUNAO ILA TU MANENO/SIASA ZINAKUWA NYINGI KULIKO VITENDO?UFISADI HUMO TFF
ReplyDeleteMIMI NILIDHANI KWA SABABU WACHEZAJI WETU WANA MAUMBO MADOGO-SI KWELI HATA KIDOGO BAADA YA KUANGALIA MPAMBANO WA FAINALI HII YA ZAMBIA NA IVORY C HILO SASA NIMELIWEKA PEMBENI.
SUALA LA SIMBA NA YANGA SIYO TATIZO KUBWA KWANI HATA TIMU YA ZAMBIA KARIBU 80% WANACHEZEA TP MAZEMBE;TIMU ISIBADILISHWE MARA KWA MARA?JANA KOCHA WA ZAMBIA KAMA MLISIKIA VIZURI WAKATI WANAENDA KUPIGA PENAT ALIWAMBIA WACHEZAJI'DONT FORGET 2006
DAVID V
SASA UTAFANYAJE VIZURI KITU AMBACHO HUKIPENDI?? TANZANIA HATUPENDI MPIRA!! NI KELELE TU NA MAJUNGU!! HATA WEBSITE ZA MAGAZETI TANZANIA HAYAJAWEKA MATOKEO NA HIGHLIGHTS ZA FAINALI YENYEWE MPAKA DAKIKA HII, HATA WEBSITE YA TFF HAKUNA CHOCHOTE. HATA BLOG HII HAIJAWEKA HIGHLIGHTS MUHIMU!! NI WIVU??
ReplyDeleteTAFAKARI!!
IMAGINE! And still compared to other nations, Tanzania is having two teams which are all allowed to join the AFCON tournaments (Taifa Stars & Zanzibar Heroes) and we still messing up with opportunities. WE SHOULD WAKE UP!
ReplyDeletemimi nashauri kwanza tuwapandishe ndege mbovu hii timu ya taifa na ianguke wachezaji wote wafe.....halafu na sisi tutafute wachezaji wapya kama zambia pengine itakuwa dawa na sisi baada ya miaka 19 twaweza kufanya kitu ......
ReplyDeleteSasa huyo anayesema hatuko serious labda kikwete pekeyake,mpelekeni basi yeye kikwete achezi mpira..shida yetu sie watanzania ni uchawi na sio mpira na ujanja tuu wa kuongea...wachezaji wapunguze ngono na ulevi..na wawe serious na kazi yao
ReplyDeleteUkomandoo kuanzia uongozi wa vilabu,shirikisho hadi wafadhili uchwara.Iundwe idara ya uhasibu kwenye vilabu na TFF zitapatikana tu pesa za kulea vipaji mbona vipo tu lukuki?
ReplyDelete...hata website ya Mwanaspoti hakuna chochote kuhusu fainali, daily news no, The Citizen no, lakini kwa watani wa jadi (daily Nation) kuna taarifa ya zambia! hapa tofauti ni kubwa!! Walau mdau Shaffi Dauda amejitahidi!!
ReplyDeleteSisi tunaweza siasa, ndio maana website za karibu magazeti yote hutakosa ngua za kijani na politiki, maisha yote utafikiri ni mwaka wa uchanguzi!!
Work ethics: zero, trust: zero, discipline: zero. na Soccer inahitaji sifa zote hizo!! kwa kweli kazi yoyote ionahitaji kuwa na hivyo vitu!!
tukiondoa ubishoo, tukiondoa ubinafsi na tukiweka mambo mengine sawa kama vile vyombo vya michezo basi tunaweza kufanikiwa.
ReplyDeleteUkiangalia wenzetu, jamani hata sudani wanatushinda!!
Yaani nilivyoangalia wazambia jana nikaona vibwana mdogo vingine vimekaa kama wamachinga wa pale kariakoo, lakini mpira vinapiga ile mbaya.
Ni hayo tu
Mwendawazimu hana la kujifunza katika chochote, wacha watu wenye mikakati na dhamira za kweli wafanye maajabu ya kuishangaza dunia, wakati Tanzania inaushangaza ulimwengu kwa mambo mengine adimu kv tiba za Liliondo, mauaji ya maalbino, ufisadi, fitna, siasa chafu nk.
ReplyDeletetz tumeng'ang'nia akina nsajigwa wakati tallent wapo hadi vijijini tena waliokuwa wanamtoa jasho Drogba ni vijana wadogo sana HONGERA CHIPOLOPOLO, TZ mkiomba mechi ya kirafiki na hao jamaa mtakula tano. kwani tunaweza mpira wa mezani tu.
ReplyDeletenyie angalieni english premier league tu ndo inafurahisha, mpira bongo? hakunaga timu
ReplyDeleteMada nzuru sana kaka Michuzi.Kwanza mfumo mzima wa soka hapa nchini,haujakaa katika hali ya kutaka kuinua soka la nchi yetu,badala yake umetawaliwa na wajanjawajanja fulani ambao wako pale kujitajirisha wao na familia zao including nyumba ndogo zao,inauma sana ndugu michuzi,kuona watanzania zaidi ya 30million wenye kiu ya kweli na uhitaji wa kweli wa kuona mafanikio ya timu zetu,potelea mbali Taifa stars,japoza club basi.Wachache hao wasio na ufahamu wowote kuhusu soka zaidi ya vijielimu vyao vya kuungaunga na ujanjaujanja mwingi na maneno tele,bado wanaendelea kuidhurumu furaha ya wengi.Ni hivi,kuanza upya si ujinga,Zambia wameweza wana nini na sisi tushindwe,tuna nini.Hapa cha msingi ni kuua na kuuzika uongozi wote wa Tff na vyama vingine vya Club hapa nchini,na tuchague watu wenye uweledi wa soka.suala la kocha halihusiki hapo,either awe mzawa au foreigner,kama team mbovu ni mbovu tu.Naililia Tanzania,inajengwa na wenye Moyo na kuliwa na wenye Choyo.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRICA.
ReplyDeleteMaximo hatufai kurudi na huyu Mdenishi aondoke apewe JULIO.
ReplyDeletemdau Jongo wa Kisiju.
Hivi we Jongo una akili kweli? Julio kocha? Yule hata aliyokuwa mchezaji hakuwa mchezaji wa kimataifa bali ni wa kawaida tu japo wengi mtabisha lakini ukweli ndo huo. Katika miaka yake yote ya ukocha amefanya nini cha hajabu, jibu ni hakuna. Julio ni sawa tu wapenzi Wa soka bongo, kuongea sana na porojo za hapa na pale. Julio ni mtu wa majungu na hafai kuwa kocha kamwe.
DeleteWatanzania tumechoka kusubiri lini tutashiriki African cup??? Ili toondoe hili neno KICHWA CHA MWENDA WAZIMU!!!!!.fanyeni kweli sio ubishooo tuuu!!!!.utaona tunaitatana majina makubwa kumbe miyayusho tuu!!!.
ReplyDeleteHuwezi kuwekeza katika Siasa kwa kuelekeza Mabilioni ya Shilingi za Walipa Kodi,,,halafu ukavuna Mafanikio ya Soka na Huduma Bora za Afya!
ReplyDeleteUkiwekeza katika Siasa mavuno ni Ujenzi wa Mabaa,Pubs,Ununuzi wa Magari ya anasa,Magari kwa Nyumba ndogo zao,Ujenzi wa Mahoteli na Majumba ya Wanasiasa na Familia zao!
Huwezi kuwekeza katika Siasa kwa kuelekeza Mabilioni ya Shilingi za Walipa Kodi,,,halafu ukavuna Mafanikio ya Soka na Huduma Bora za Afya!
ReplyDeleteUkiwekeza katika Siasa mavuno ni Ujenzi wa Mabaa,Pubs,Ununuzi wa Magari ya anasa,Magari kwa Nyumba ndogo zao,Ujenzi wa Mahoteli na Majumba ya Wanasiasa na Familia zao!
Tanzania kote kote hakuna la kufurahisha wapenda Tanzania ni ufisadi na uzembe, roho mbaya na kubwa zaidi ni ubnafsi wa viongozi wote.
ReplyDeletelabda kije kizazi kingine iki labda iwe kwa mtutu wa bunduki.
MUNGU ibariki Tanzania
Ukweli unaogopwa, ndio maana hatutafanya chochote, hata blogu hii inajua!! Jipu lisipopasuliwa madhara yake mwayajua!!
ReplyDeleteMaoni mengi mazuri humu. Lakini ukweli ni kuwa, tukipata kocha mzuri tutafika mbali. lakini si Mbrazili au Mwingereza, tafadhali. Tutafute Mjerumani au mholanzi. Wana rekdi nzuri Afrika hawa.
ReplyDeleteKweli suala la soka limewakuna wengi maana wachangiaji ni wengi mno.Hapatoshi.
ReplyDeleteNaomba niungane na wenzangu kuwa kwa Tanzania kupotea maboya katika soka inauma saaaaaaana.Huko nyuma tulikuwa bora mno lakini siku hizi siasa katika mpira kibao.
Hata tukileta kocha gani kwa mwendo huu hatutafikapopote.Maamuzi yote hata ya utaalamu wa mpira yanatoka TFF.
Kila kocha aliyewahi kuletwa TZ,iwe kwa club ,au taifa lazima aondoke anadai.
Maandalizi maalumu ya timu zetu au mikakati ya kudumu sijui kama ipo.TUNAKAZANA SANA IKIBAKI WEEK MBILI AU MWEZI HALAFU TUKASHINDANE NA WENZETU WALIOJIANDAA MWAKA.
Zamani,kila shule ya msingi ,kila shule ya secondary,kitongoji kulikuwa na viwanja.Sasa hivi hata maeneo ya wazi yamejengwa.Hata huko mikoani viwanja hivyo havipo tena.Viwanja vya mashirika ya umma viko wapi leo.
Mpira si utajiri au ukubwa wanchi au uwingi wa watu kama wenzangu walivyosema bali ni maandalizi na mikakati ya michezo.Kutafuta masoko ya wachezaji wetu nje badala ya vikwazo.
Hata michezo mingine yote iwe hivyo.Wakina Filbert,Mwinga Mwanjala wa siku hizi wako wapi. Kwani wale tuliwaazima kutoka nchi zingine!
Mkazo wa kujenga viwanja au kutenga viwanja vya michezo uko wapi.Vijini,wilayani,mikoani mkazo uko wapi?Badala yake hata maeneo yaliyokuwepo tunajenga.Si lazima academy kama za ulaya,maeneo hayo yakitengwa na mkazo ukawepo vijana wataanzia huko.Tumeshindwa hata viwanja vya tennis,Golf.Ukitaka michezo hiyo lazima uishi Dar au Arusha.
Naye anyeongelea kuwa tumazidi ngono,hizo ni hoja za kiwenda wazimu.Wapi hakuna ngono au hujatembea wewe ,na hata kuosoma mambo mablimbali husomi wewe.Ngono kuwepo au kutokuwepo inahusianaje na mpira.Wewe ukiibiwa mkeo unaleta hoja hizo kwenye mjadala wa mpira.
Hivi unajua ngono ilivyo Brazil,Spain,Ufaransa,Italy,au unaona TZ tu.Hiyo ya TZ cha mtoto.Hao Zambia waliposikia timu ya imeshinda unasikia walicho fanya wanawake wengi!Wamesema zawadi yetu ni ngono.Hivyo,usichanganye mambo wewe ongelea tufanyeje katika soka na michezo mingine acha kutuletea yaliyokusibu.
Kwa kweli katika soka tufanye kitu.Sudani,Angola,Bukinafaso,Malawi wanatuacha kweli.Tusilaumu wachezaji wal makocha bure tuone sisi tufanyeje katika sekta ya michezo.Unataka siku hizi wa TZ kweli hawezi kukimbia mbio.
Hata waheshimiwa wabunge katika maeneo yenu tusaidieni.Hamkuenda huko kuongelea barabara,maji,umeme,na madaraja tu.Hata michezo ni kazi yenu,vyote vinahusu wanachi.
Sababu nime compare economical ranks kati ya TZ na Zambia ni kutoa sababu ya kutokuwa na resources, kila mchezo ni lazima uwe na funds za maandalizi ya muda mrefu sio miezi sio mwak amoja au mitano, it is a long term strategy..nashukuru wadau kwa kutoa mifano ya US,China etc..
ReplyDeleteUSA soccer sio their main sports,angalia jinsi wanavyo fanya vizuri kwenye basketball, Tennis na Boxing etc. sita mention mchezo wao wa mikono wanaouita foot ball kwa kuwa niwenyewe tu ndio wanaoucheza.
China the same thing soccer is not their primary sports angalia wanvyo fanya vizuri on gymnastics, tennis, basket ball etc..nafikiri mmenilielewa kwa nini nimeanza na swala na uchumi.uchumi mzuri means better resources...shida yetu kubwa ni uongozi..kama ilivyo kwenye issues nyingine za Afya, Umeme etc.
Cha kwanza ningependa viongozi wa soccer kuanzia ngazi ya mikoa wawe ni wachezaji wa zamani ambao wameshacheza huu soccer.
tuna wachezaji wengi tu wazuri ambao wakiwekwa kama viongozi watamake a big difference.
Vipaji tunavyo..maandalizi yanatakiwa kuanzia shule za msingi,umitashumta, umisseta..wakina Nteze, Lunyamila,Fumo wote hawa walianza kuoneka kwenye Umisetta.
ila tatizo kuwa kama wadau woote wanavyo sema ni UONGOZI UONGOZI UONGOZI...
Mimi jamani yangu macho kumanina anzia kufukuza huyo Tenga , Rage, na wote hao, ambao hawakucheza hata mpira, Eti NI KIT MANAGER WA National Team. kweli Tutafika?
ReplyDeleteNa kujuana tu, wakati wacheza wazuri mmewapuuzia watoto under 17 walioshinda coca cola cup, mpaka brazil. Wako vijana chipukizi wazuri Huko Kigoma eti mmekalia wachezaji wa simba na yanga shenzi taip.
mdau kigoma Rangers
Tenga ni mbabaishaji tu, japo alichezea Pan lakini kimpira sidhani kama kweli alikuwa mchezaji mzuri maana hajuwi lolote lile. Binafsi, nafikiri yupo pale kimaslahi zaidi. We umeona wapi mtu anakuwa rais lakini hajuwi kanuni za soka ama uongozi?
ReplyDeleteHapa tatizo ni Tenga na wachezaji wetu wachawi. Mpira ni kipaji na si uchawi kama kina Ngassa wanavyodhani.
ReplyDeleteJamani KIPA WA Zambia alikuwa na NDUMBA.Harry REDNAPP WA Totenham juzi mechi na NEWCASTLE alikuja njiwa kukaa golini.siku na LIVERPOOL alikuja paka.uchawi upo mpirani.
ReplyDeleteTumejifunza kuwa kipaji na uchawi ni vitu viwili tofauti.
ReplyDeleteMdau Anonymous wa Mon Feb 13, 12:28:00 PM 2012
ReplyDelete-----------------------------------
''Tuwapandishe Ndege mbovu Taifa Stars wafe...baada ya miaka 19 na sisi tuwe na mafanikio kama Zambia!''
-----------------------------------
HAHAHAHAHAHA,,,,!!!!!
Mdau kwa kweli nimecheka sana kwa Maoni yako, sasa hapo si ndio tutapelekwa Mahakama kwa Makosa ya uhalifu dhidi ya Ubinaadamu The HAGUE?
Amenifurahisha mdau aliyesema tatizo ni kuwa tulimleta mzushi Maximo ambaye alikuwa mtu wa majungu na chuki kwa wachezaji wa Simba kama Boban ambao wangetufikisha huko.
ReplyDeleteKweli kabisa mdau. Sasa hivi tunaye Poulsen ambaye naye "ameendekeza majungu" na kutomchukua Boban. Kweli mdau. Katika Watanzania milioni 40, bila Boban hatuna timu. Hata ukipekua historia yetu ya ushiriki wa kombe la mataifa huru ya Afrika utaona kwamba mara zote timu ilipokuwa inamtumia Boban ilikuwa inashiriki kwenye hizo fainali.
Nimerudi tena TFF.mnachekesha kweli,kujifanya mnajua kitu,huyu kocha wa Zambia alikuja hapo kuomba kazi mkamnyima eti hana uzoefu wa kutosha.Mkamchukua mwenye uzoefu...haya yako wapi sasa.Haya maoni yalivyo mengi yanaashiria ni jinsi gani tunavyougua na timmu yetu ya Taifa ya mpira wa miguu.Jitahidi twende Africa ya kusini 2013,msiangalie viingilio tu milangoni.
ReplyDeleteDavid V