Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) kila Jumatatu kuanzia saa 4 Asubuhi limekuwa likiendesha ‘Jukwaa la Sanaa’ kwenye ukumbi wake ulioko makao makuu ya Baraza Ilala Sharif Shamba.Katika jukwaa hilo linalohusisha wadau wote wa sanaa, hoja nzito na motomoto kuhusu tasnia ya Sanaa na Utamaduni zimekuwa zikijadiliwa na kujibiwa.
Katika Jukwaa la Sanaa Jumatatu ijayo ya Tarehe 20, Februari 2012, Kamati ya Vazi la Taifa itawapa fursa ya kukaa na wasanii, wadau wa sanaa na wananchi kwa ujumla nafasi ya kufahamu hatua na mikakati iliyofikiwa katika mchakato mzima wa kupata vazi la taifa na kutoa maoni yao.
Wasanii na Wadau wa Sanaa na wananchi hawana budi kuja kwa wingi Kuanzia saa 4 Asubuhi kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko Ilala Sharif Shamba ili kupata fursa ya kukutana na Kamati ya Vazi la taifa
WOTE MNAKARIBISHWA
Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI, BASATA
Ntashangaa sana kama Wtza. watashindwa kubuni aina ya vazi la taifa kisilokua na bendera.
ReplyDeleteHivi sisi jamani tuna laana gani ya kushindwa kufikiri sawa sawa?
Yaani, badala ya kujikita kubuni aina ya mshono, tunakimbilia bendera na ml. kilimanjaro.
Mh. mudhihiri ana mawazo mazuri ktk hili lkn naona hakuteuliwa ktk watu 'makini'
HAPA TATIZO NI KWAMBA HATA WAKIFANYA HUO MKUTANO HAUTASAIDIA KWANI WAMESHAAMUA KUCHAKACHUA BASI WAMALIZIE WATOE HILO WATAKALOLITOA.WATU WAMESHAPIGA KELELE KUHUSU SWALA HILI LAKINI HAKUNA BADILIKO LOLOTE LILILOTOKEA.HAPO UAMUZI UPO KWA NCHIMBI NA KUSAGA WENGINE WOTE BENDERA FATA UPEPO
ReplyDelete