Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) kila Jumatatu kuanzia saa 4 Asubuhi limekuwa likiendesha ‘Jukwaa la Sanaa’ kwenye ukumbi wake ulioko makao makuu ya Baraza Ilala Sharif Shamba.Katika jukwaa hilo linalohusisha wadau wote wa sanaa, hoja nzito na motomoto kuhusu tasnia ya Sanaa na Utamaduni zimekuwa zikijadiliwa na kujibiwa.

Katika Jukwaa la Sanaa Jumatatu ijayo ya Tarehe 20, Februari 2012, Kamati ya Vazi la Taifa itawapa fursa ya kukaa na wasanii, wadau wa sanaa na wananchi kwa ujumla nafasi ya kufahamu hatua na mikakati iliyofikiwa katika mchakato mzima wa kupata vazi la taifa na kutoa maoni yao.

Wasanii na Wadau wa Sanaa na wananchi hawana budi kuja kwa wingi Kuanzia saa 4 Asubuhi kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko Ilala Sharif Shamba ili kupata fursa ya kukutana na Kamati ya Vazi la taifa
WOTE MNAKARIBISHWA
Ghonche Materego

KATIBU MTENDAJI, BASATA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ntashangaa sana kama Wtza. watashindwa kubuni aina ya vazi la taifa kisilokua na bendera.

    Hivi sisi jamani tuna laana gani ya kushindwa kufikiri sawa sawa?

    Yaani, badala ya kujikita kubuni aina ya mshono, tunakimbilia bendera na ml. kilimanjaro.

    Mh. mudhihiri ana mawazo mazuri ktk hili lkn naona hakuteuliwa ktk watu 'makini'

    ReplyDelete
  2. HAPA TATIZO NI KWAMBA HATA WAKIFANYA HUO MKUTANO HAUTASAIDIA KWANI WAMESHAAMUA KUCHAKACHUA BASI WAMALIZIE WATOE HILO WATAKALOLITOA.WATU WAMESHAPIGA KELELE KUHUSU SWALA HILI LAKINI HAKUNA BADILIKO LOLOTE LILILOTOKEA.HAPO UAMUZI UPO KWA NCHIMBI NA KUSAGA WENGINE WOTE BENDERA FATA UPEPO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...