
FRANCO CHARLES MWEKWALUMA
Kesho Jumamosi Februari 4, 2012 inatimia miaka 15 tangu mpendwa wetu ututoke. Ingawa kimwili umetutoka lakini kiroho utadumu kuwa katika mioyo yetu, na pengo lako halitazibika kamwe.
Tunakukumbuka na tunapungukiwa sana na ule upendo wako kwetu,ucheshi na mshikamano katika familia.
Mwanao Grace anakupenda na anakuombea. Unakumbukwa na familia yote hasa kaka na dada zako. Ndugu, jamaa na marafiki wanakukumbuka pia.
Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi.
AMINA
AMINA
Ankal
ReplyDeleteNimeumia sana kuona picha hii hapa. Huyu Franco hata sikujua siku zote hizi kuwa amekwenda, duh! Yaani huyu alikuwa Kaka yangu alinitangulia Tambaza Sekondari, tukaja onana IFM, lakini zaidi alikuwa mwanasoka mzuri na pia mtu wa watu wote. Franco aliishi katika jamii ya watu wenye tabia tofauti naye na wala hakuwaiga. Bila shaka wengi watakubaliana nami hasa pale BOT kuwa ilikuwa vigumu sana kuamini kuwa Franco kasoma Tambaza lakini ana nidhamu kiasi kile. RIP Franco wenzako hatuna la kusema bali kumshukuru Mungu kwa umri aliokupa kuishi duniani na kuondoka.
Hi Bro Kausioooo nitakukumbuka daima hasa kwa ucheshi na makeke yako uliyokuwa unafanya ,RIP Man!!!!
ReplyDeleteMungu awape moyo mkuu wakati wa kumbukumbu hii ngumu. Bwana alitoa Bwana akatwaa jina lake libarikiwe.
ReplyDeleteInfact it is just very sad to remember our beloved relatives and friends who have passed but let just depend on our God to give us strength.
Rest In Peace Franco, we miss you so much!
ReplyDeleteFranco Kausio winga machachari nimekumbuka mbali sana kuona hii picha nakumbuka safu ya nkoma Abdalah madenge Dan jose mpelwa oscar nyanda mlekwa.wengine HUKU NJE RAFIKI ZAKO BACHALA BOY MZUNGU WAKIKUIMBIA. MWENYEZI MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA PEPONI AMEEN
ReplyDeleteUncle Mithupu,leo umenikumbusha
ReplyDeleterafiki yangu wa siku nyingi,he was a nice man,mcheshi kwa watu wa rika lote,mungu amlaze mahali pema peponi.RIP Franco,mungu alikupenda zaidi.Adam
RIP Franco tunakumiss sana BOT na magomeni
ReplyDeleteUtakumbukwa daima JOJIS kwa Nguma Ilala....RIP
ReplyDeletetunakukumbuka sana franco, upendo na kutokuwa na majigambo. Pole tena dada yake franco uliekuwa pale chuo kikuu UDSM miaka ile, na marafiki zako wa BOT.
ReplyDeletedaH, nimekumbuka sana mitaa ya ilala na enzi za benk club kule temeke
Buriani ndugu yetu mpendwa Franco Mwekalumwa !
ReplyDelete