Kimara
Ubungo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Hii ilikuwa ni siku gani ya wiki...mbona sioni mnyororo?

    ReplyDelete
  2. Hivi huu ujengaji wa mabarabara na ma mifereji mikubwa ya maji (tena iliyowazi)ndio ujenzi gani huu?

    ReplyDelete
  3. Aisee Tanzania imejengeka banaaa, ona hilo jiji utafikiri Loss Angeles marekani!!!! Nafiri hapa kuna kapolitiks ndani yake nimekushtukia ankal, tuletee picha ya manzese basi tuonishe! Hapo barabara bado inaonekana very finyu kunatakiwa kuwe na high ways na undergraound kama kuna hiyo jeuri! Pamoja na vikwangua anga vinavyokua kwa kasi lakini wananchi wanaendelea kuishi katika hali ya umaskini! less than a $$ per day! Bongo ni nzuri kuangalia kwa macho lakini wachache ndo wanafaidi!

    ReplyDelete
  4. kuanzishwe sheria ya wapi magari makubwa yanatakiwa kupita na wapi hayapi.. ili kuongeza taswrira nzuri ya jiji pamoja na kupunguza foleni pia kuimarisha barabara.

    ReplyDelete
  5. siku hiziz asubuhi hamna nyororo,ngoma zinateleza kama vile hazipo DAR.

    ReplyDelete
  6. tehe tehe!!!!!!!! haijawahi tokea mdau wa kwanza always ni mnyororo tu. Au kuna msafara wa mkuu ulikuwa umepita ndio maana picha ikawa hivyo.

    ReplyDelete
  7. Hii itakuwa katikati ya wiki, tuna mwezi sasa hakuna foleni kabisa si asb wala jioni na kama ikiwepo ni kidogo sana na inatembea jeshi la polisi wanasitahili pongezi sana hasa ma traffic kama ni mafunzo yamewaingia vizuri sna, tunaomba waendelee hivyo hivyo.

    ReplyDelete
  8. safi sana sema chonde chonde wajemeni hiyo mitaro ya maji machafu serikali ifanyieni mpango wa kuiziba kwa juu itasababisha ajali nyingi sana

    ReplyDelete
  9. sasa gari hii inatafuta nini kwenye njia za watembea kwa miguu ndiyo maana sheria za barabarani hazifuatwi madreva wanaendesha magari ovyo ovyo

    ReplyDelete
  10. miji yetu imekaa vizuri sana na serikali imejitahidi kuipanga vizuri, lakini tatizo lipo kwa wanainchi kutunza mazingira yake, kama hapo ukiangalia taswira kwa mbali utaona unavutia, ila kwa karibu unaweza ukakasirika jinsi mazingira yalivyo machafu na hayana mvuto kabisa. wanainchi tujitahidi kurekebisha tatizo hilo, bila ya sisi hata mji uweje hautovutia kamwe.

    ReplyDelete
  11. Mdau uliyesema kulikuwa kuna msafara wala haujakosea. Picha zote zinaonyesha kuna matrafiki, angalia vizuri picha ya KIMARA, mbele ya shangingi leupe kuna landrover ya MATRAFIKI wa2 wamesimama, kulia kuna pikipiki ya ya trafiki imezuiwa na shangingi leusi, na upande huo huo mbele kuna landrover ya kina RAS Makunja!!

    Tukirudi kwenye picha ya ubungo ndio hivyo hivyo, angalia kwa makini upande wa kushoto kuna trafiki wamesimama nyuma ya landrover, shangingi leupe nyuma yao na pikipiki mbele yao.

    Ni kosa la jinai hiyo sehemu ikose foleni kihivyo. Hii CHANGA la MACHO!!!

    ReplyDelete
  12. Hali ngumu ya kiuchumi no money wese inapanda kila siku magari yameegeshwa majumbani! Hadi hapo hali ya kiuchumi itakapokuwa shwari nchini. Hapo bwana hakuna cha trafiki wala nini.Tunapanda dala dala kwa kwenda mbele na nauli itapanda hivi karibuni.

    ReplyDelete
  13. Watu wamepaki magari....maisha magumu kumudu gharama ya mafuta si mchezo ndio maana siku hizi hakuna foleni. Mkisikia watu wanalalamika maisha maugumu mnafikiri uongo????

    ReplyDelete
  14. Si rahisi kukosa foleni.Hapa ukiangalia taswira zote 2 utaona mpiga picha yuko katika msafara ambao una ving'ora na unaongozwa na pikipiki za Polisi, Pickup na Landcruiser ya Polisi. Hivyo Polisi walikuwa wanasafisha njia ndio maana hakuna magari mengi na kuonesha foleni

    ReplyDelete
  15. Wewe anomy Fri Feb 17, 09:17:00 PM 2012,kama ulipita sekondari nadhani ulikuwa mzuri sana kwenye somo la Jiografia upande wa picha..Uko sawa aliyepiga picha alikuwa kwenye msafara,mimi mwenyewe nilikimbilia kuangalia magorofa kwenye 'Background' sikuweza kuziangalia kwa umakini hizi picha hadi ulipobnishtua.Asante sana mdau kwa uchunguzi wako-nimeupenda

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...