Baadhi ya watumishi wa Idara mbalimbali za Serikali ya Mkoa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, wakisukuma gari lililonasa kwenye tope katika barabara ya Lumuma – Kidete, wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa huo, Joel Bendera (hayupo pichani) mwanzoni mwa wiki, alipokwenda kukagua ujenzi wa Bwawa la Kidete.
Baadhi ya watumishi wa Idara mbalimbali za Serikali ya Mkoa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, wakihangaika kubeba mawe ili kulinasua gari lililonasa kwenye tope katika barabara ya Lumuma – Kidete, wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa huo, Joel Bendera (hayupo pichani) mwanzoni mwa wiki, alipokwenda kukagua ujenzi wa Bwawa la Kidete.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mbona Vumbi linatimuka,imekwama kwenye vumbi au?.Hizo gari(Lancruiser 70 series) nzuri kwa barabara za aina hizo tatizo tu tairi zake nyembamba,ikianza kuchimba inakuwa kama wembe.

    David V

    ReplyDelete
  2. Landcruiser HardTop inakwama....basi dereva ana matatizo au hiyo gari ni kanyaboya.
    Na ziara ya mkuu wa mkoa msafara mkubwa hivyo wa nini. Uchezeaji wa fedha za walipakodi tuu. alitakiwa awe na wajumbe wasiozidi watatu. yeye, dereva na masaidizi/mtaalamu wake.
    angalia mafuta, perdiem nk

    ReplyDelete
  3. Hii ndiyo shida ya nchi yetu , tunanunua magari tu, lakini kujenga barabara aaaah hatutaki.

    ReplyDelete
  4. Hapo dereva tu ndio mwenye tatizo, hiyo gari ni kosa la jinai kukwama sehemu kama hiyo!!!!

    Itakuwa dereva lazima kabebwa na jamaa yake yupo serikalini. Kazi za kupeana hizo, mwisho anataka kuwalaza pori!!

    Halafu hizo gari nyingine hata kamba ya kuvutia hamna au ndio mabosi hao wamebeba kalamu na laptop tu!!!

    ReplyDelete
  5. Maajabu ya mwaka huu. Hiyo L/Cruiser si ya kukwama mahali hapo, kwa kuwa ina 4WD. Dereva kazoea kuendesha gari zisizo na 4WD

    ReplyDelete
  6. mbona barabara kaiacha pembeni huko alikuwa anaenda wapi wacha akwame,huyo kweli ni dereva ?

    ReplyDelete
  7. Huyu dereva alipelekewa leseni nyumbani na kuna ndugu yake alimsaidia kupata ajira. Hapo siyo mahali pa kukwama gari kama hiyo. Halafu msafara mzima hawana hata kamba ya kuvutia. Hayo ni mambo ya kupeana kazi kwa kujuanan na siyo kufuata sifa za mwombaji.

    ReplyDelete
  8. Imekuwa ni vuzuri Waheshimiwa wakashuhudia ubovu wa barabara na miundo mbinu hafifu kwa macho yao na vitendo badala ya kupokea taarifa wakiwa Maofisini Mjini kwa njia ya simu.

    ReplyDelete
  9. aaah jamani msimlaumu dereva kwa sana maana yeye alikwepa hicho kitope pembeni maana kuosha gari nako kazi kila saa, bora gari iwe safi lakini inase kwenye mtaro..ebo!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...