Vijana waliomakatwa na meno ya Tembo waliokamatwa jana Mkoani Morogoro ambao walitambulikwa ka majina yao,Erick Kiari (kushoto) mwenye miaka 23, Abel Adrian (katikati) pia anamiaka 23 na Anaheri Mkindi ambaye umri wake ni miaka 17 wakiwa chini ya ulinzi katika kituo cha polisi mkoa wa Morogoro mara baada ya kukamatwa na meno ya tembo vipande 51 wakati wakisafiri kutoka mkoa wa Mbeya kwenda jijini Dar es Salaam kwa kutumia Gari yenye Namba DFP 3468 ambayo inadaiwa kuwa ilibandikwa tu na si Nambari zake za usajili na ilikuwa ni gari ya Mtu binafsi.Watuhumiwa hawa wanatarajiwa kupandishwa kizimbani kesho jumatatu ili kujibu mashtaka yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. No comment

    David V

    ReplyDelete
  2. Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya ITV jana , meno hayo yametoka wilaya ya Mbarali. Jamani vyombo vya usalama Fuatilieni kwa umakini sana Mbarali kuna ujangili wa chinichini unao watajirisha wageni. Hao vijana ni chambo tu, wahusika wenyewe wametulia tuli. Kaazi kwelikweli. Hata hiyo nalipongeza jeshi la polosi Morogoro, wamekuwa makini sana kipindi hiki.Huko mikoa mingine vitu vinapita tuu lakini vikifika Morogoro STOP.

    ReplyDelete
  3. Hao ni tembo wangapi waliouwawa?

    ReplyDelete
  4. a.alaikum kaka michuzi habari za mihangaiko? bro kwahisani yako naomba unitafute kupitia email hii alkharus@msn.com nina ujumbe nataka kukuuliza tafadhali ni muhimu sana

    ReplyDelete
  5. Fedha, zitatufikisha pabaya!

    Hii yote ndio ile haraka ya maisha na kuwa wengine ni Mafala.

    Matokeo yake ni kuaibika ,kupoteza muda bureee ,kudhalilika na kuozea Jela, hata kama walikuwa wanatumiwa na Watu.

    Hawa ni watoto sana angalia wana harakisha maisha kwa kukimbilia Utajiri kwa kazi hatarishi na Haramu kama hizi, badala ya kuzingatia masomo na shughuli za halali kufikia Mafanikio ya Kimaisha na huo Utajiri.

    ReplyDelete
  6. Watoto wa Kichagga wametumwa Pesa MBEE,

    Inaelekea hawa jamaa wamesha fanikisha mara kadhaa hapo kabla safari hii 'msala umeshika moto' imekuwa balaa.

    Matokeo yake wanazama Lupango!

    ReplyDelete
  7. mbona vitu vidogo tu hivyo jamani, ni kweli wanafanya makosa kwa kuwa majangili lakini mbona kuna wezi wakubwa kabisa wa rasilimali za nchi na hawakamatwi jamani?, eenh, hapa ndo mimi mara huanza kuamini kuwa hii nchi imeuzwa na ina wenyewe..wananchi wa chini tulie tu...JK mwogope muumba wako, utakwenda kujibu huko akhera

    ReplyDelete
  8. Anaheri Mkindi (Umri miaka 17)

    Masikini wee, aliyekaa kulia pembeni ya namba halisi za gari T 949 ameshika tama amefunga mikono yake, NDIO ANAZINDUKA USINGIZINI, ANAFUNGUKA, KUWA SASA ANAZAMA KABURINI.........JAMANI FEDHA FEDHEHA,

    SASA JAMANI VIFUNGO VYA UJANGILI MIAKA MICHACHE NI 30 JELA, HUKU UMRI WA MTANZANIA KUISHI NI MIAKA 56 TU.

    SASA (17+30=47) KWA HESABU ZA HARAKA HARAKA UKITOA KIFO KIFUNGONI DOGO ANABAKIWA NA (56-47=9) MIAKA 9 TU YA MAISHA!

    ZAIDI YA ROBO TATU 75% YA MAISHA YAKE ANATUMIA GEREZANI!

    JAMANI SI BALAA HILI?

    TUNATUMIA GHARAMA KUBWA KUWAZA UTAJIRI WA HARAKA HARAKA NA MAENDELEO BILA KUJALI UPANDE WA PILI KUWA KUNA MKONO MREFU WA SHERIA NA MAMLAKA!

    ReplyDelete
  9. Fanyeni umachinga, hamtaki mnaona ninyi Mastaa ma Tozi!

    Uzeni mifuko kwa jumla Masokoni,faida ya ku unga unga mnaona mnachelewa maisha!

    Fanyeni huduma za kibiashara kama kupiga photocopy na secretarial , ohhh kazi ni ya kike!

    Chagueni shughuli halali fanyeni hata kama faida ndogo, ohhh sisi ni Wachagga Christmass ya mwaka huu 2012 bado miezi 10 ipo karibu sana ikifika tutajieleza vipi Moshi?,,,sisi ni pasua kichwa Mtani kazi za Kiswahili hatuwezi!

    Jamani Vijana maisha yana njia ya Mkato?

    Jamani Vijana maisha yana njia ya Haraka?

    Haya sasa safari ya Lupango!

    ReplyDelete
  10. i hope watawafatilia wajue wahusika wenyewe na nani walikuwa wanapelekewa dar.

    inaweza kuwa walishapita bila kukamatwa before.

    ReplyDelete
  11. FEDHA ZA HARAKA:::kuliko M-PESA VODACOM!

    Ukisikia Fedha za haraka kuliko M-PESA VODACOM yenye uwezo na kasi ya ajabu kumfikishia Muhitaji fedha popote na saa yeyote ndio hizi!

    Matokeo yake inakuwa JELA-PESA VODACOM ambayo hawa watoto watatu wameghushi badala ya M-PESA VODACOM halisi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...