Vijana waliomakatwa na meno ya Tembo waliokamatwa jana Mkoani Morogoro ambao walitambulikwa ka majina yao,Erick Kiari (kushoto) mwenye miaka 23, Abel Adrian (katikati) pia anamiaka 23 na Anaheri Mkindi ambaye umri wake ni miaka 17 wakiwa chini ya ulinzi katika kituo cha polisi mkoa wa Morogoro mara baada ya kukamatwa na meno ya tembo vipande 51 wakati wakisafiri kutoka mkoa wa Mbeya kwenda jijini Dar es Salaam kwa kutumia Gari yenye Namba DFP 3468 ambayo inadaiwa kuwa ilibandikwa tu na si Nambari zake za usajili na ilikuwa ni gari ya Mtu binafsi.Watuhumiwa hawa wanatarajiwa kupandishwa kizimbani kesho jumatatu ili kujibu mashtaka yao.
Home
Unlabelled
Wadakwa na Meno ya Tembo vipande 51 mkoani morogoro
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comment
ReplyDeleteDavid V
Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya ITV jana , meno hayo yametoka wilaya ya Mbarali. Jamani vyombo vya usalama Fuatilieni kwa umakini sana Mbarali kuna ujangili wa chinichini unao watajirisha wageni. Hao vijana ni chambo tu, wahusika wenyewe wametulia tuli. Kaazi kwelikweli. Hata hiyo nalipongeza jeshi la polosi Morogoro, wamekuwa makini sana kipindi hiki.Huko mikoa mingine vitu vinapita tuu lakini vikifika Morogoro STOP.
ReplyDeleteHao ni tembo wangapi waliouwawa?
ReplyDeletea.alaikum kaka michuzi habari za mihangaiko? bro kwahisani yako naomba unitafute kupitia email hii alkharus@msn.com nina ujumbe nataka kukuuliza tafadhali ni muhimu sana
ReplyDeleteFedha, zitatufikisha pabaya!
ReplyDeleteHii yote ndio ile haraka ya maisha na kuwa wengine ni Mafala.
Matokeo yake ni kuaibika ,kupoteza muda bureee ,kudhalilika na kuozea Jela, hata kama walikuwa wanatumiwa na Watu.
Hawa ni watoto sana angalia wana harakisha maisha kwa kukimbilia Utajiri kwa kazi hatarishi na Haramu kama hizi, badala ya kuzingatia masomo na shughuli za halali kufikia Mafanikio ya Kimaisha na huo Utajiri.
Watoto wa Kichagga wametumwa Pesa MBEE,
ReplyDeleteInaelekea hawa jamaa wamesha fanikisha mara kadhaa hapo kabla safari hii 'msala umeshika moto' imekuwa balaa.
Matokeo yake wanazama Lupango!
mbona vitu vidogo tu hivyo jamani, ni kweli wanafanya makosa kwa kuwa majangili lakini mbona kuna wezi wakubwa kabisa wa rasilimali za nchi na hawakamatwi jamani?, eenh, hapa ndo mimi mara huanza kuamini kuwa hii nchi imeuzwa na ina wenyewe..wananchi wa chini tulie tu...JK mwogope muumba wako, utakwenda kujibu huko akhera
ReplyDeleteAnaheri Mkindi (Umri miaka 17)
ReplyDeleteMasikini wee, aliyekaa kulia pembeni ya namba halisi za gari T 949 ameshika tama amefunga mikono yake, NDIO ANAZINDUKA USINGIZINI, ANAFUNGUKA, KUWA SASA ANAZAMA KABURINI.........JAMANI FEDHA FEDHEHA,
SASA JAMANI VIFUNGO VYA UJANGILI MIAKA MICHACHE NI 30 JELA, HUKU UMRI WA MTANZANIA KUISHI NI MIAKA 56 TU.
SASA (17+30=47) KWA HESABU ZA HARAKA HARAKA UKITOA KIFO KIFUNGONI DOGO ANABAKIWA NA (56-47=9) MIAKA 9 TU YA MAISHA!
ZAIDI YA ROBO TATU 75% YA MAISHA YAKE ANATUMIA GEREZANI!
JAMANI SI BALAA HILI?
TUNATUMIA GHARAMA KUBWA KUWAZA UTAJIRI WA HARAKA HARAKA NA MAENDELEO BILA KUJALI UPANDE WA PILI KUWA KUNA MKONO MREFU WA SHERIA NA MAMLAKA!
Fanyeni umachinga, hamtaki mnaona ninyi Mastaa ma Tozi!
ReplyDeleteUzeni mifuko kwa jumla Masokoni,faida ya ku unga unga mnaona mnachelewa maisha!
Fanyeni huduma za kibiashara kama kupiga photocopy na secretarial , ohhh kazi ni ya kike!
Chagueni shughuli halali fanyeni hata kama faida ndogo, ohhh sisi ni Wachagga Christmass ya mwaka huu 2012 bado miezi 10 ipo karibu sana ikifika tutajieleza vipi Moshi?,,,sisi ni pasua kichwa Mtani kazi za Kiswahili hatuwezi!
Jamani Vijana maisha yana njia ya Mkato?
Jamani Vijana maisha yana njia ya Haraka?
Haya sasa safari ya Lupango!
i hope watawafatilia wajue wahusika wenyewe na nani walikuwa wanapelekewa dar.
ReplyDeleteinaweza kuwa walishapita bila kukamatwa before.
FEDHA ZA HARAKA:::kuliko M-PESA VODACOM!
ReplyDeleteUkisikia Fedha za haraka kuliko M-PESA VODACOM yenye uwezo na kasi ya ajabu kumfikishia Muhitaji fedha popote na saa yeyote ndio hizi!
Matokeo yake inakuwa JELA-PESA VODACOM ambayo hawa watoto watatu wameghushi badala ya M-PESA VODACOM halisi!