Mh. Balozi Dkt Batilda S. Burian, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya, amewasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mh. Mwai Kibaki, Rais wa Jamhuri ya Kenya tarehe 28 Machi, 2012. Hafla hiyo fupi iliandaliwa IKULU, Nairobi. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mh. Prof. Sam Ongeri, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na viongozi wengine wa Serikali. Pichani juu Mh. Balozi Dkt Batilda S. Burian akisoma hotuba fupi ya kuwasilisha rasmi Hati zake za Utambulisho kwa Mh. Rais Mwai Kibaki.
 Mh. Balozi Dkt Batilda S. Burian akikabidhi rasmi Hati zake za Utambulisho kwa Mh. Rais Mwai Kibaki.
 Mh. Balozi Dkt Batilda S. Burian akitambulisha rasmi ujumbe wake aliombatana nao. 
 Mh. Rais Mwai Kibaki akiteta jambo na Maafisa wa Ubalozi alioambatana nae.  Kutoka kushoto kwa Mh. Rais ni Bw. Innocent Eugene Shiyo, Mkuu wa Utawala na Fedha ambaye pia anasimamia Masuala ya Uchumi na EAC, Brig Gen Edwin Victor Millinga, Mwambata Jeshi, Bi Grace Mgovano, Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Bibi Kemilembe Mutasa, Mwambata Mazingira.

Mh. Rais Mwai Kibaki akiteta jambo na Mh. Balozi Dkt Burian kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na Mh. Rais kwa ajili  ya Mabalozi waliowasilisha Hati zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hongera Dkt Batilda, unaaminika.

    ReplyDelete
  2. Kila la kheri Dkt Batilda

    ReplyDelete
  3. Maskini mh Rais hajui hata kushika glass..jamani..haigi hata wenzake walioko pembeni

    ReplyDelete
  4. Dkt Batilda, utatuwakilisha vyema tunakuaminia

    ReplyDelete
  5. Bongo tupo juu:

    Jamani Wadau Kenya choka mbaya, angalieni,

    Wakenya mabahili sana,

    1.Picha ya kwanza juu kiti cha Raisi nyuma yek kina Nembo ni kama cha meza ya Chakula, hako kameza kenyewe kwa kumpokelea utambulishi duh kana Kitambaa cheupe cha kufuma kwa mkono na pembeni mauwa ya Plastiki !

    2.Angalia picha ya chini Ikulu imepigwa Chupingi wakati sisi Bongo Ikulu yetu ni Hekalu la maana !

    ReplyDelete
  6. wacha upuuzi wako glasi ndio jambo ulililiona tuuuuuu. acha ufinyu wa mawazo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...