Mh. Balozi Dkt Batilda S. Burian, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya, amewasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mh. Mwai Kibaki, Rais wa Jamhuri ya Kenya tarehe 28 Machi, 2012. Hafla hiyo fupi iliandaliwa IKULU, Nairobi. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mh. Prof. Sam Ongeri, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na viongozi wengine wa Serikali. Pichani juu Mh. Balozi Dkt Batilda S. Burian akisoma hotuba fupi ya kuwasilisha rasmi Hati zake za Utambulisho kwa Mh. Rais Mwai Kibaki.
Mh. Balozi Dkt Batilda S. Burian akikabidhi rasmi Hati zake za Utambulisho kwa Mh. Rais Mwai Kibaki.
Mh. Balozi Dkt Batilda S. Burian akitambulisha rasmi ujumbe wake aliombatana nao.
Mh. Rais Mwai Kibaki akiteta jambo na Maafisa wa Ubalozi alioambatana nae. Kutoka kushoto kwa Mh. Rais ni Bw. Innocent Eugene Shiyo, Mkuu wa Utawala na Fedha ambaye pia anasimamia Masuala ya Uchumi na EAC, Brig Gen Edwin Victor Millinga, Mwambata Jeshi, Bi Grace Mgovano, Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Bibi Kemilembe Mutasa, Mwambata Mazingira.
Mh. Rais Mwai Kibaki akiteta jambo na Mh. Balozi Dkt Burian kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na Mh. Rais kwa ajili ya Mabalozi waliowasilisha Hati zao.
Hongera Dkt Batilda, unaaminika.
ReplyDeleteKila la kheri Dkt Batilda
ReplyDeleteMaskini mh Rais hajui hata kushika glass..jamani..haigi hata wenzake walioko pembeni
ReplyDeleteDkt Batilda, utatuwakilisha vyema tunakuaminia
ReplyDeleteBongo tupo juu:
ReplyDeleteJamani Wadau Kenya choka mbaya, angalieni,
Wakenya mabahili sana,
1.Picha ya kwanza juu kiti cha Raisi nyuma yek kina Nembo ni kama cha meza ya Chakula, hako kameza kenyewe kwa kumpokelea utambulishi duh kana Kitambaa cheupe cha kufuma kwa mkono na pembeni mauwa ya Plastiki !
2.Angalia picha ya chini Ikulu imepigwa Chupingi wakati sisi Bongo Ikulu yetu ni Hekalu la maana !
wacha upuuzi wako glasi ndio jambo ulililiona tuuuuuu. acha ufinyu wa mawazo.
ReplyDelete