Kidebe kama kawa kama dawa,sasa kwa wale wanaosema ni bongo pekee ndio kuna zengwe la kiwese basi mjue mmenoa. 
 Jamaa akiwahi zake sheli.
Kipini cha nguvu kuelekea sheli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Huo unasema zengwe la mafita haliko bongo sio kweli kwani nipo hapa uingereza kwa muda wa miaka kumi na tano na sijawahi kuona hali hii hata siku moja hii ni mara ya kwanza kuona hali hii na hii yote inasababishwa huenda kukawa na mgomo wa madereva wa malori ya kukubebea mafuta,kwa hiyo muandishi au mpiga picha za matukio haya ungeelza hali yenyewe inatokana na sababu gani na sio kupotosha umma.

    ReplyDelete
  2. Kaka zengwe la huko sio ukosefu wa mafuta bali madereva wanaondesha matanki ya mafuta ndio wametishia kugoma japokuwa wamesema hawatagoma tena.

    ReplyDelete
  3. Hongera kwa kuwaonyesha wadau wa hii blog kuwa hata ughaibuni mambo ni kama Bongo tu. Isipokuwa wao waliwahi kuwa wajanja. Tunasoma nao hapa wanadesa kama kawa.

    ReplyDelete
  4. kweli........lakini ni nadra sana kutokea!

    ReplyDelete
  5. SAFARIHII SIJUI WATAINGIA NCHI GANI LABDA KENYA TEHTEHTEH, SYRIA WAMEDINDA! VENEZUELA MSAHAU KUGUSA OIL.

    ReplyDelete
  6. michuzi acha kupotosha umma. ni kweli tatizo ni moja - upatikanaji wa mafuta.

    lakini ambacho hukiweki wazi ni sababu za mafuta kukosekana Uingereza ukalinganisha na yanayotokea hapa nyumbani.

    ReplyDelete
  7. hapa ni uk ....na sisi tumerithi kwao kila kitu

    ReplyDelete
  8. Huu ndio upumbavu unaotutia umaskini, kwanini umeficha namba za gari kwenye hiyo picha ya chini. Hukuhitaji sisi kutambua ni nchi gani katika nchi za dunia ya tatu. Hao watu wajuu unaosema wapo wakikusanya mafuta kwenye madumu hawako kwenye foleni na ni picha zinazoonyesha mtu mmoja mmoja kitu ambacho kinawezekana kufanyika popote pale endapo utakuwa unahitaji mafuta kwa shughuli nyingine... Tunapenda umasikini kwa sababu jirani maskini, unakuta mtu haendi shule sababu rafiki yake haendi shule na ndio huku mleta mada alipofikia kulazimisha kupenda umaskini kwa kutaka kujilinganisha kwanjia yoyote ile na mtu wa nchi zilizoendelea

    ReplyDelete
  9. Picha tatu za watu wajuu zinaonyesha wapo kazini, kwenye mambo ya ujenzi/ukarabati au usafi. Hii ni kutokana na aina ya mavazi yao hasa upande wa viatu vyao vinayofanana.. Haitoshangaza sana kwa wao kutumia madumu kuchukulia mafuta kama moja ya njia ya ubebaji wa nishati hiyo kuelekea kwenye matumizi yake, Picha ya mwisho inahitaji kufikiria kidogo japokuwa ninaharaka nikirudi nitakufafanulia vizuri...

    "Tupende kujiringanisha na mazuri na si mabaya"

    ReplyDelete
  10. Usitudanganye ndugu,!!!!

    ReplyDelete
  11. UNGETUELEZA HAPA NI MJI AU NCHI GANI

    ReplyDelete
  12. Hahahahaha,

    Duhhh ama kweli Dunia imefilisika !
    Yaani hata Uingereza kwa werevu kuna Foleni ya mafuta ?

    Kuanzia sasa tafadhali ninaomba msimsumbue Raisi wangu Mpendwa JK masuala ya shida ya Mafuta muanze kumuuliza David Cameron wa UK maana wao walitutawala sisi na Uhuru tumepata kutoka kwao !

    ReplyDelete
  13. Shida ya Mafuta Uingereza hadi foleni?

    Ahhh stop muache mara moja kumsumbua JK kwa suala la uhaba wa mafuta mwacheni mwana wa mwenzenu !

    ReplyDelete
  14. Shida ya Mafuta kwa Uingereza ?,,,afadhali sisi Tanzania ni nchi ndogo tunajitahidi wao ni aibu wana jina kubwa !

    Akijamba mtoto sio tatizo sana wanasema 'amepumua'!,,,ila akijamba Mkubwa ohhh watasema 'kaharisha' kabisaaaaa !

    ReplyDelete
  15. Hizo picha ni Ukerewe,huna haja ya kujua ni mji gani kwani shida hiyo ipo miji yote kwa sasa kwa vilingo mbali mbali.Kuna waziri aliyekosea na kuwaambia watu wajiwekee weso nyumbani, basi ndiyo kaanza vugo la panick hiyo. Kuna sheria hapa inayokataza mtu kuweka petroli zaidi ya kiasi fulani nyumbani, lakini jamaa hawasikii la mtu. Jana mama mmoja kawaka moto alipokuwa akigeda petroli kutoka one container to another, jikoni kwake. Masikin hali yake taaban.Jamaa waliona tanki likipeleka wese basi wakalifuata mpaka huko liendapo.Its just panick buying.

    ReplyDelete
  16. KWA HIYO UNATAKA KUSEMA NI SAWA KUKIWA NA MATATIZO YA MAFUTA TANZANIA KWA SABABU HATA UINGEREZA MATATIZO YAPO?

    FUNGUKA KICHWA MTOA PICHA!!

    ReplyDelete
  17. Mbona annony wa kwana na wapili wepesi kuhalalisha hali ngumu hiyo huko Ulaya bali wa kwanaza kubeza hali kama hiyo nyumbani kwao? Kwani kukaa Uingereza mika kumi na tano inatueleza nini kama si ujinga tu. Kwani nasi hali ya foleni ya mafuta ilivyojitokea si ilikuwa kwa sababu ya waagizaji wakubwa kuhodhi mafuta? Mbona hili hawakuliona? Wenzetu wamekaa nje hata kujusahau kwao na sasa wamekuwa makuwadi ya huko walipofikia ambapo bado wanadharauliwa na kujiona wajanja kukosoa wanapotoka! Bahati mbaya hii ndiyo akili ya maskini aliyegandamizwa kwa miaka mingi!!

    ReplyDelete
  18. Mdau unaempinga ndugu yetu wa uingereza aliesema ameishi huko miaka15 yuko sawa usimshutumu Kama kuwadi yeye macho yameshatoka vumbi,haijui tena malaria,Jikoni kalala paka.mimi na wewe tofauti na yeye usiwe na wivu kuifagilia bongo ni kuwafanya Viongozi wetu wajipweteke badala ya kutafuta maendeleo na wao watatueleza hivyo hivyo Uk wese foleni wacha ujinga wako wewe unatoka kijiji gani?Katika akili yako unafikiri Uk wakose wese upate wewe huko mwanarumango!!!subutuuuu!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  19. Jamani muwe basi mnaangalia hata taarifa za habari za Kimataifa! Mtu anakaa anabisha eti sio Uingereza hapo? Angalia Skynews hiyo habari ya ukosefu wa mafuta wanairudia rudia sana.

    ReplyDelete
  20. Wanaobisha kuwa si Uingereza ni vipofu. Hata hauwezi kusoma, vibao. Na kuona 'co.uk' kwenye information za 'site' zao. Lakini pia haiwezekani kama wewe ni baba mzuri, kuiambia familia yako kuwa watakula maharage na ugali maisha yote, maana umetembelea nyumba ya tajiri fulani ukakuta wanakula maharage kwa ugali tu. Ni jukumu la kiongozi kuweka mazingira mazuri wakati wote, bila kulinganisha ubovu wa nchi yake na nchi tajiri. Hapo kutakuwa hakuna kuendelea

    ReplyDelete
  21. Anachosema ndugu yetu aliyekaa uingereza kwa muda wa miaka kumi na tano ni kweli sio ukuwadi,ila wewendugu yetu inaonekana una husda na roho mbaya,yeye kasema kuwa hakuna uhaba wa mafuta tatizo ilikuwa madereva wa malori ya kubebea mafuta walikuwa wanataka kufanya mgomo hata hivyo huo mgomo hauko tena sasa kusea ukweli sio utumwa na ndiyo maan sisi hapa bongo hatuendelei kwa kusema uongo na kulindana.

    ReplyDelete
  22. UINGEREZA SIO PARADISO AU PEPONI!

    Shida haichagui wa kumfika, cha msingi tusijenge hoja kuwa kwa sababu imejiri huko huko kwa Wajanja wetu basi sisi iwe ndio kuwa imekuwa muafaka, hapana inabidi tijikakamue tuweke mipango endelevu na ya uhakika kwa upande wetu !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...