Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Issa Machibya (wa pili kushoto) na RPC wa mkoa huo wakiwasili eneo la tukio, ambapo kwa mujibu wa habari toka huko moto huo mkubwa umezuka katika mojawapo ya maduka na juhudi za kuuzima zinaendelea
Asskari wa Faya wakiwasili sokoni hapo tayari kuanza kazi. 


Na Pardon Mbwete na Anna Msika wa Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limefanikiwa  kuzuia na kuokoa  mali na kudhiti moto kwa kushirikiana na askari zima Moto wa kikosi cha zimamoto Halmashauri ya Kigoma Ujiji na Kikosi cha zimamoto viwanja vya Ndege na baadhi ya vitu vimeokolewa na vingine kuungua bado thamani yake haijajulikana
 
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Kihenya Kihenya  amemtaja mmiliki wa duka hilo kuwa ni Faustine  Samweli 39, Mfanyabiashara wa Lumumba  Road chumba NO.16 kiliungua moto.
 
Kaimu Kamanda  amesema kuwa  Chanzo cha moto huo ni Freezer iliyokuwa imeachwa ikiwaka usiku mzima bila kuzimwa hivyo kusababisha chanzo cha moto huo
 
Kamanda huyo amesema kuwa Thamani halisi ya mali iliyoteketea bado haijajulikana  na uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado unaendelea.
 
 Freezer linalodhaniwa ndiyo chanzo cha moto huo

 
Hata hivyo kamanda kihenya amewataka wafanya biashara wa eneo hilo kuhakikisha usalama wa mali zao kabla na baada ya kufanya shughuli zao kuwa waangalifu wakati wa ufungaji wa maduka yao ili kuzuia tukio la aina hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ndio madude ya kichina yanavyokuwa unalinunuwa rahisi ila hasara yake inakuwa kubwa sana....tokea lini freezer kuwa chanzo cha moto

    jamani tununuwe vitu japo second hand vilivyotengenezwa na hao wachina ila linalotoka ulaya tusivamie vitu vipya vinavyotoka moja kwa moja kutoka china

    mimi nishakula hasara sana kwa vitu kama hivi ila tokea nichukuwe toka ulaya nimeshatatuwa matatizo haya

    ReplyDelete
  2. Chanzo cha moto inasemekana ni FRIZA iliyoachwa bila kuzimwa!!! Huyo ni kaimu kamanda wa Mkoa!!! Lol! Nani kakwambia kuwa friji au friza vinatakiwa kuzimwa, kabla ya kufunga duka. Vifaa hivyo kitaalam vinapowashwa kwa mara ya kwanza baada ya kutoka dukani, havitakiwi kuzimwa, labda wakati tu wa kuvifanyia service ya kawaida. Kama vile, kuondoa misosi na vinywaji vyote, anglau mara moja kwa mwezi kwa ajili ya kusafisha, na service nyinginezo.

    Kwa hiyo viongozi msiwe waropokaji. Tukio kama hilo linapotokea, acha idara husika ndiyo itoe taarifa.

    Mdau-Mtaalam wa masuala ya umeme.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...