Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde,Inaeleza kuwa Boss wa zamani wa TBC (Tanzania Broadcasting),Tido Mhando (pichani) amekuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Uchapishaji wa Magazeti ya kila siku hapa nchini ya Mwananchi Communication Limited,kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mkurugenzi Mtendaji wa Zamani wa Kampuni hiyo,Sam Shollei.
Globu ya Jamii inatoa pongezi kwa Bw. Tido Mhando kwa kupata nafasi hiyo na kumtakia kila la kheri katika utendaji wa kazi yake hiyo mpya.
BRAVO TIDO, FANYA KAZI KWA MOYO! SAHAU YALIYOPITA.
ReplyDeleteLETA MAENDELEO KWA UWEZO WA ELIMU YAKO NA WAPE ELIMU ULIOTOKA NAYO HUKU UK. TANZANIA DEMOKRASIASASA.
Hongera sana Mwananch Communications kwa kupata mtendaji mahiri kabisaaaaaaaa!
ReplyDeleteHeeeeeeeeeee Hurray!! MCL mmeokota kifaa, hongera sana. Ila muepukane na uandishi wa kishabiki ila fuateni misingi ya uandishi bora wa ukweli na uwazi kwa kupata taarifa ya pande zote zinazohusika. In other words try as much as possible to be objective observing all the journalistic ethical principles without being intimitaded. Through this path you will continue to be respected, and hopefully with Tido you will ascend higher and higher.
ReplyDeleteKumekucha, sasa nanga zitapaa!
ReplyDeleteBravo mwananchi communication for to have Mr Tido at the helm.
ReplyDeleteTanzania tuna tatizo sana la kutokuwa na watu wavumilivu wanaoweza kutulia kwenye taaluma zao kiuadilifu wakaendeleza career zao hadi kiasi cha kuwa ma-Executives. Tido ni mfano wa wa-Tz wachache walioonyesha kuwa uadilifu na uvumilivu katika taaluma ni jambo muhimu sana. Pamoja na kumpa hongera Tido, hii iwe changamoto kwetu sote, kama tunataka siku moja tuongoze mashirika makubwa ambayo kwa sasa yanaongozwa na wageni, lazima tufanye kazi kiuadilifu, kiuvumilivu, tujenge uzoefu wa miaka ya kutosha. Hapo tutawaondoa Wakenya na wengine wengi katika nafasi nyeti..!
ReplyDeleteUtadumu huko kweli Tido, au utakubaliana na upishi wa habari na picha kwa manufaa ya kisiasa? Mie nikupe tu pole, maana sioni ni jinsi gani unaweza ku keep ethical integrity na kufanya kazi Mwananchi kwa wakati mmoja!
ReplyDeleteAtaweza kufanya kazi chini ya mafisadi!!
ReplyDeleteHongera Tido.
ReplyDeleteYou are a rare breed in Tanzania, i.e a principled proffessional who does not get swayed by political pressure. We all know what you went through at TBC.
Maintain same ethical and proffessional standards at Mwananchi.
Hongera tena.
Huyu bwana ni mtu mahiri sana angalia alivyofanya mageuzi makubwa TVT na sasa TBC Moja mimi sikuwa na wazo la kufungulia runinga ya TVT kipindi kile lakini baada ya huyu bwana (TIDO) kufanya mabadiliko hayo imekuwa television mama na yakuangaliwa na watu lukuki tanzania na a/mashariki, ongera mwananchi kwa kumuona ila TBC mtabaki hapo hapo na hakuna jipya litakalo ongezeka baada ya Tido Haibu yenu kwa waliomfanyia ufitini
ReplyDeleteHongera tido ukweli uta kuweka huru. Umekuwa mkweli ukiwa tbc, pamoja na yote ulibaki huru na mwenye heshima kwa kuwa ulikuwa mkweli. Taifa la tanzania linakutegemea sana.
ReplyDelete