Moja ya Bajaj zifanyazo shughuli ya kubeba abiria jijini Dar ikiwa imekula vichwa pamoja na mizigo zaidi ya uwezo wake na inaendelea safari zake kama kawaida.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ili kuongeza usalama kwa abiria wa bajaji wengeweka alau vyuma vitatu kila upande ili abiria wasianguke.

    ReplyDelete
  2. vitu vingine tunajitakia wenyewe. Mimi nilishauri zamani kwa wahusika, bajaji zote zinazobeba abiria ziwe registered na kupewa namba ya ubavuni kama taksi za kawaida. Dereva wake lazima aweke certified copy ya leseni yake ining'inie kati yake na abiria ili abiria awe ana uhakika nani ni dereva wake na kama ana leseni. Kila bajaji lazima iorodheshe kituo chake cha kazi na hicho kituo kiwe kimesajiliwa. Process yote hio ni mapato kwa Halmashauri/ TRA/ Polisi. Siwezi amini bajaji zimezuka miaka mitano tu iliopita lakini tunashindwa kuzidhibiti. Similar process ifanywe kwa bodaboda.

    Che

    ReplyDelete
  3. Hapo ndipo tunapokosea. Trafiki wanaona huyo anavunja sheria lakini wanawaachia tu mpaka itakapotokea ajali ndipo wataanza kupiga kelele.

    Mbona taxi hazibebi abiria wengi sana hapo mjini?

    Na nyinyi abiria munaoburuzwa namna hiyo inakuwaje? Munasubiri mpaka mupate ajali halafu ndiyo museme ooooh alikuwa amejaza kupita kiasi.

    Si usubiri bajaji nyengine?

    ReplyDelete
  4. Mara nyingi wakipakia lumbesa kama hii hawapiti maeneo walipo trafiki polisi. Na issue ya kupakia watu watatu pia a.k.a Mshkaki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...