Shirika la Umeme Tanzania Tanesco limepatwa na tatizo la kuanguka kwa nguzo 22 za umeme eneo la Kipawa – uwanja wa ndege jijini  DSM kulikosababishwa na upepo mkali uliovuma kutoka eneo linalojengwa uwanja wa ndege wa Mwl, J.K.  Nyerere.

Tatizo hilo la dharura litasababisha baadhi ya maeneo yote ya kipawa – Tandika na maeneo ya Temeke kukosa umeme wakati mafundi wa TANESCO  wakifanya kazi usiku kucha.
Njia hiyo ya msongo wa kilovolti 33 unatarajiwa kurudishwa kwenye hali ya kawaida mapema iwezekanavyo.

Shirika linawaomba wateja wake wote kuwa watulivu wakati mafundi wanahangaika na linatoa tahadhari kwa mtu yeyote kutogusa waya uliodondoka chini.
Uongozi wa Shirika uanaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kwa raia na wateja wake kwa ujumla.


Wakazi wa Jiji  wakiangalia daladala namba T 195 BRV, lililopata ajali ya kuangukiwa na nguzo ya umeme maeneo ya Kipawa, Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam leo. Katika ajali hiyo iliyohusisha daladala zingine mbili namba  T 808 AEZ na T 403 BSH,  watu wanne walijeruhiwa na nguzo 22 zilianguka kuanzia JET hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kutokana na  upepo mkali


                                           Daladala zikiwa zimezingirwa na nya za umeme

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. duh bongo kweli tambalare

    ReplyDelete
  2. siyo bongo peke yake, huo upepo mkali (tornado) hata huku marekani (kansas) umetokea week iliyopita..nguzo nyingi zilianguka, miti iling'olewa na baadhi ya nyumba zilivunjika..na kuna baadhi ya watu walirudishiwa umeme siku ya nne... tatizo hapo hamna usalama, huku barabara kama hizo zilifungwa na kuachia mafundi wamefanya kazi yao na kwasababu ya usalama wa raia bt hapo naona ndo kwanza watu wapo karibu na hizo waya.

    ReplyDelete
  3. Bongo vingumu sana kuhepuka kifo ,usipokufa na hiki lazima ufe na hili duuu washukuru mungu naona umeme hakuwa kwenye nguzo hizo ingekuwa duuu ,mungu anajua

    ReplyDelete
  4. mmh jamani, upepo au nguzo zimeoza?

    ReplyDelete
  5. Hee hee hii ilikuwa balaa.Siku nyingine hali kama hii abiria msiwe mnashuka kwenye gari..Kwenye gari ndiko kuna usalama zaidi kuliko kuruka chini!!!!...Hii ingekuwa balaa baya kuliko maelezo

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...