Shirika la Umeme Tanzania Tanesco limepatwa na tatizo la kuanguka kwa nguzo 22 za umeme eneo la Kipawa – uwanja wa ndege jijini DSM kulikosababishwa na upepo mkali uliovuma kutoka eneo linalojengwa uwanja wa ndege wa Mwl, J.K. Nyerere.
Tatizo hilo la dharura litasababisha baadhi ya maeneo yote ya kipawa – Tandika na maeneo ya Temeke kukosa umeme wakati mafundi wa TANESCO wakifanya kazi usiku kucha.
Njia hiyo ya msongo wa kilovolti 33 unatarajiwa kurudishwa kwenye hali ya kawaida mapema iwezekanavyo.
Shirika linawaomba wateja wake wote kuwa watulivu wakati mafundi wanahangaika na linatoa tahadhari kwa mtu yeyote kutogusa waya uliodondoka chini.
Uongozi wa Shirika uanaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kwa raia na wateja wake kwa ujumla.
duh bongo kweli tambalare
ReplyDeletesiyo bongo peke yake, huo upepo mkali (tornado) hata huku marekani (kansas) umetokea week iliyopita..nguzo nyingi zilianguka, miti iling'olewa na baadhi ya nyumba zilivunjika..na kuna baadhi ya watu walirudishiwa umeme siku ya nne... tatizo hapo hamna usalama, huku barabara kama hizo zilifungwa na kuachia mafundi wamefanya kazi yao na kwasababu ya usalama wa raia bt hapo naona ndo kwanza watu wapo karibu na hizo waya.
ReplyDeleteBongo vingumu sana kuhepuka kifo ,usipokufa na hiki lazima ufe na hili duuu washukuru mungu naona umeme hakuwa kwenye nguzo hizo ingekuwa duuu ,mungu anajua
ReplyDeletemmh jamani, upepo au nguzo zimeoza?
ReplyDeleteHee hee hii ilikuwa balaa.Siku nyingine hali kama hii abiria msiwe mnashuka kwenye gari..Kwenye gari ndiko kuna usalama zaidi kuliko kuruka chini!!!!...Hii ingekuwa balaa baya kuliko maelezo
ReplyDeleteDavid V