NA VERONICA KAZIMOTO – MAELEZO

Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Mawasiliano Tanzania (TEWUTA) kimeitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kupunguza tozo inayolipwa na makampuni ya simu nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dare s Salaam leo, Katibu Mkuu wa chama hicho Junus Ndaro amesema TCRA imeshindwa kusimamia na kuhakikisha gharama za huduma za mawasiliano ya simu zinapungua na kuwa na uwiano sawa kwa tozo za makampuni yote Tanzania.

“Mamlaka imeshindwa kuwaeleza watanzania kwa uwazi na huku ikitambua kuwa moja ya jukumu lake ni kupanga bei elekezi kwa makampuni ya simu, kitendo ambacho hakijafanyika toka mamlaka hiyo iundwe na kutangazwa kwenye vyombo vya habari”, amesema Ndaro.

Ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine chombo hiki kiliundwa kwa madhumuni ya kumsaidia mteja kupata bei nafuu kila anapotumia mtandao wowote wa simu.

“Ni ukweli kuwa watanzania wamechoka kutembea na simu zaidi ya moja za mitandao tofauti kwa sababu ya kutafuta punguzo kwa mtandao husika, hivyo ni wajibu wa TCRA kusimamia mitandao yote ya simu nchini kuwa na bei zenye uwiano wa karibu” amesisitiza Ndaro.

Ndaro amesema kuwa serikali imeleta Mtandao wa Mkongo (FIBRE) ambao gharama zake za uendeshaji ni mdogo sana na unafanya kazi vizuri kwa haraka zaidi hivyo kuna uwezekano mkubwa kwa TCRA kupunguza gharama wanazotoza kutoka kwenye makampuni ya simu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. MPAKA LINIApril 24, 2012

    HIVI...hawa wafanyakazi wa TEWUTA...wamatumwa au ni wanafiki...kwamba WAGENI kwetu tuwalegezee KWAO watukazie...hii migao ya maji, umeme, huduma mbovu za afya na elimu zitaisha lini..HUKU MADINI NA GESI YOTE WANACHUKUA...SASA NA MAWASILIANO...baada wa mwezeshe mtanzania kufungua kampuni za mawasiliono...ndo kwanzaaa hawaelewi hata mipango yao baada ya miaka 20...tuwe na kampuni la kitanzania kama ya hao wawekezaji wa nje!!!

    ReplyDelete
  2. Kwa hili sidhani kama TCRA itasikia kilio cha wananchi kwani kwa TOZO kuwa juu ndio mgao wao unavyokuwa juu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...