Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Maendeleo hapa nchini(UNDP) kesho Jumatatu tarehe 23 April, 2012 watazindua mradi wa makubaliano wa kuwajengea uwezo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na watumishi wa Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mradi huu ujulikanao kwa lugha ya kiingereza kama Legislatures Support Project ulisainiwa kwa pamoja kati ya Serikali na UNDP na ni mradi wa miaka minne yaani 2011-2015. Mradi unagharimu Dola za Kimarekani Million 7.8
Lengo kuu la mradi huu ni kuwawezesha Wabunge na watumishi wa Ofisi ya Bunge kufanyakazi kwa ufanisi zaidi katika shughuli za Kamati hasa masuala yanayohusu uchambuzi wa miswada, uchambuzi wa bajeti, utendaji kazi wa Serikali na changamoto zinazowakabili wapiga kura katika majimbo.
Aidha kwa upande wa watumishi mradi huu umelenga kuwajengea uwezo ili waweze kuwasaidia waheshimiwa wabunge kufanya kazi zao kwa ufanisi katika Kamati na ndani ya Bunge.
Wadau wakubwa ambao watashirikishwa katika mradi huu ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watumishi wa Bunge, Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP), taasisi mbalimbali zinazotoa mafunzo katika masuala ya Kibunge, Mabunge ya Kikanda na Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA). Wengine ni Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, Public Procurement Regulatory Authority, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika.
Mradi huu wa miaka mine ni ukombozi kwa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania katika kutoa mafunzo na uboreshaji katika utendaji kazi na shughuli zote zinazohusiana na Bunge, hususani katika namna bora ya kuisimamia Serikali na uwakilishi. Hadi hivi sasa, wafadhiri wakuu wa mradi huu ni UNDP, DFID, Ubalozi wa Ireland, Ubalozi wa Norway, Bank ya Maendeleo ya Afrika, Ubalozi wa Afrika Kusini, Ubalozi wa India, Ubalozi wa Marekani na USAID.
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma,
na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge
DODOMA
22 Aprili, 2012
HIKI NI CHANZO KINGINE CHA ULAJI WA FEDHA ZA UMMA TU.HUKU NIKUPOTEZA MUDA,KUNA HAJA GANI YA KUWAJENGEA UWEZO KAMA UWEZO WALIONAO WANAPOUTUMIA UNAKANDAMIZWA NA SPIKA?KILA KITU HAKIENDI NCHII HII WABUNGE WANACHANGIA NA KUELEZA NINI CHA KUFANYA LAKINI HATUA ZINAZOCHUKULIWA HAKUNA.HATA MUWEKE MRADI WA KUWAANZISHA DARASA LA KWANZA KABISA WABUNGE WOTE BADO HAITA SAIDIA KWANI SHIDA SI UTENDAJI ILA UTEKELEZAJI
ReplyDeleteMsalaba mwingine kwa watanzania
ReplyDeleteNakuunga mkono wewe namba moja..Sikio la kufa...
ReplyDeleteDavid V
Mdau naomba moja umemaliza kazi. Chanzo kingine cha ulaji hicho.
ReplyDeletendio maana nasema wanaosoma na kutoa hoja humu globuni wana mawazo finyu. Elimu haina mwisho, na ukilisoma tangazo anaebeba mzigo huu ni UNDP na ndio matakwa ya mwezeshaji sasa unataka UNDP iwagaie watanzania pesa za bure bila ya kuzifanyia kazi. Tutakua wajinga maisha. Tungojee hao chadema wakishika hiyo serikali wasitumie chochote. Watanzania sisi ni wa mwisho hapa duniani. Mimi wala sio CCM ninakerwa tu na umbumbumbu wetu sisi kila kitu madhali kinafanywa na serikali iliopo madarakani basi mtakiponda.
ReplyDeleteSio tu ni ulaji kwa Wabunge bali hata ulaji kwa hao jamaa wa UNDP. Hivi kweli si aibu kuesema Bunge letu linahitajijkujengewa uwezo? Miaka hamsini baada ya uhuru! Tuliwachaguaje? Aibu tupu. Watu wa Umoja wa mataifa na hizo serikali shirikishi wanatafuta posho zao na wabunge wanaona mteremko. Kwanini hizo fedha wasijenge shule na hospitali vitu tunavyoviona?
ReplyDeleteMdau namba moja umeongea ukweli kabisa, wanawajengea uwezo wa nini wakati yanaelezwa mengi na wabunge lakini wakubwa wanalindana?? Zitawatokea puani siku moja hizi hela za jasho la wanyonge.!!
ReplyDelete