Dear Michuzi,
Habari za Jumatatu,
Jana jumapili ya tar 17 May, wanachama wa Baraza la CHADEMA (BAVICHA) tawi la Arusha walipata Muda wakumtembelea mjane wa Marehemu Msafiri Mbwambo aliyekua Mwenyekiti wa Chadema kata USA-River wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha.
Walipata fursa yakukaa na familia hiyo nakujumuika nayo pamoja kupeleka mahitaji kiasi kwa familia hiyo. Walipata nafasi pia yakufanya shughuli za nyumbani hapo na baadae kurudi Arusah.
Wakiwa hapo pia walipata kuijua vizuri familia hiyo wakiwemo mabinti watatu wa marehemu ambao waliwatia majonzi vijana hao na pia BaVICHA walifurahishwa na ujasiri wa Mjane na watoto hao.
Siku Njema
Emmanuel
Friend of CHADEMA Arusha
Wanachama wa BAVICHA wakiwasili nyumbani kwa mjane huyo
Wanachama wa BAVICHA wakiwa na familia ya marehemu Msafiri Mbwambo
Kila nikikumbuka ishu ya Msafiri chozi linanidondoka
ReplyDelete