Judith G. Habash a.k.a Komando Binti Machozi Lady Jay Dee akiwasili na Familia yake katika Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo maeneo ya Kinondoni Hananasifu.
Vijana wa Familia ya Jay Dee wakishusha msosi ulioandaliwa Nyumbani Lounge kwa ajili ya watoto yatima wa Kituo cha Maunga Centre.
Baadhi ya zawadi zilizopekwa na Jay Dee Family katika kituo cha kuelea watoto yatima cha Maunga Centre.
Mlezi wa kituo cha Maunga Centre Bi. Zainabu Bakari akionyesha chumba wanacholala watoto wa kiume katika kituo hicho.
Hiki ni choo wanachotumia yatima hao ambacho hakijaezekwa na bati.
Mtoto Khadija Mussa akisoma Risala kwa mgeni rasmi Komando Lady Jay Dee na Familia yake (hawapo pichani) ambapo amezungumzia changamoto ya mahali wanapoishi haparidhishi na kuwataka wadau kujitokeza kuwasaidia kuboresha eneo lao ikiwemo Choo, Sehemu ya kulala pamoja na ada za twisheni kwa watoto hao.
Lady Jay Dee akipokea risala kutoka kwa mtoto Khadija Mussa.
Lady Jay Dee akikabidhi msaada uliotolewa na Familia yake vikiwemo Mchele, Maharage, Mafuta ya Kupikia, Sabuni za Kufulia, Nguo, Juisi pamoja na vingine vingi. Anayepokea msaada huo ni Mlezi wa Kituo hicho Bi. Zainabu Bakari (kushoto) pamoja na mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho Khadija Mussa.
Jay Dee Family inawakaribisha wadau wote watakaoguswa kutoa mchango chcochote walichonacho kupitia Jay Dee Family. Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Judyjaydee@yahoo.com.
Lady Jay Dee akibadilishana mawazo na walezi wa kituo hicho baada ya kukabidhi msaaada huo.
Watoto wa kituo cha Maunga Centre wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Jay Dee Family.
Vijana wa Jay Dee Family wakiwajibika kuhudumia chakula kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre.
Mlezi wa kituo cha Maunga Centre Bi Zainabu Bakari ambapo amezungumzia changamoto zinazowakabili ni sehemu ya kuishi wahudumu wa kituo hicho, mishahara ya kuwalipa wahudumu na makazi ya wahudumu wa kituo hicho.
Bi. Zuhuru Bakari alisema kituo hicho kinalea watoto 30 ambapo watoto 20 wanalelewa nje ya kituo kwa baadhi ya walezi waliowachagua wao kutokana na ufinyu wa eneo jumla yake inatengeneza idadi ya watoto 50.
Baadhi ya wanafamilia katika pozi na walezi wa kituo hicho.
Wanafamilia katika picha ya pamoja na walezi wa kituo hicho pamoja na watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2012

    shukran lady jay dee. mungu azidi kukupa na akulinde. watanzania wangekuwa na upendo kama wewe wange pungukiwa wivu na chuki. watanzania wengi wamejaa chuki rohoni na ndio maana wanazidi kuwa maskini. wale wenye roho nzuri kama lady jay ndio mungu anazidi kuwajalia. roho nzuri na kazi kwa bidii siku zote utakua rewarded by the mighty god.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2012

    Hongera JayDee, mwenyezi mungu akuzidishie na uendelee na moyo huo. Amen

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2012

    Watanzania ni nani? ifike mahali tutoe pongezi kwa mazuri ambayo mtu anafanya bila kutaja kwamba kuna watz ambao wana chuki. Kwa kufanya hivyo nina imani wale wenye chuki watabadilika. Lakini ukitoa pongezi huku unawaponda wale wenye chuki maana yake hata comment yako wataiona inaonyesha ina chuki na wataendelea kuwa na chuki wakati kinachotakiwa wenye chuki wapungue wabaki wengi wenye upendo mdau wa Sun Jul 01, 01:13:00 AM 2012 nadhani umesikia kilio changu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2012

    HONGERA SANA, ALLAH ATAKULIPA MAALIPO MAKUBWA INSHAALLAH.

    ReplyDelete
  5. Jay Dee kupongeza, hongera 'Binti Machozi',
    Mola atakuongeza, kunyima katu hawezi,
    Kila jema unofanza, ng'ara kama mbalamwezi,
    "Jaza" kesho takutunza, ILAHI MOLA MWENYEZI.

    Hongera sana Lady Jay Dee and your family kwa moyo wenu wa upendo na huruma. You really put a smile on their faces. INSHA ALLAH, Mwenyeez Mungu awajaaliye kila jema na malipo yenu mtayakuta kesho usoni twendako. Keep it up!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2012

    Safi sana jideeee u really comando keep it up god bless u

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2012

    umefanya vizuri. hicho ulichotoa kwa yatima hao ndio chako umejiwekea akiba kwa mwenyezimungu utakikuta.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 02, 2012

    Hii inaitwa ''Self-Actualization'' Kwa stage iliyofikia sasa hivi soon tutasikia unadhamini Football Team. Aminia JD uko juu sana

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 02, 2012

    Hongera sana Lady JD na Familia yako!

    Tuwe na moyo wa kujali kama huu tutafanikiwa sana.

    Mwenyezi Mungu akufungulie zaidi!

    ReplyDelete
  10. andy andrew diq labanAugust 16, 2012

    be blessed

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...