Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo (pili kulia) akimfuatilia kwa makini Mwalimu wa somo la Baolojia wa Shule ya Sekondari Lupanga, January Maziku,wakati akiandika maneno makuu ya muhimu katika ufundishaji wanafunzi wa masomo ya sayansi , hisabati na kiingereza kwa njia ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ( TEHAMA) hivi karibuni mjini Morogoro, Wizara hiyo kwa kushirikiana na Serikali ya Sweden kupitia SIDA wameanzisha mradi wa majaribio kwa njia hiyo uliojumuisha shule 21 za Halmashauri saba za Wilaya na Manispaa nchini,mafunzo hayo yameendeshwa kwa muda wa wiki mbili katika Vyuo saba vya Ualimu nchini.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo (kushoto) akimsikiliza kwa makini mwalimu wa masomo ya sayansi wa Shule ya Sekondari Lupanga , Manispaa ya Morogoro, January Maziku,anayefundisha somo la Baolojia katika shule hiyo akionesha uelewa wake baada ya kupata mafunzo ya matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika kufundisha masomo ya sayansi , hisabati na Kiingereza ‘English’,mradi huo wa majaribio umejumuisha shule 21 kutoka Halmashauri saba za Wilaya na Manispaa nchini, ambapo mafunzo hayo yameendeshwa kwenye Vyuo saba vya Ualimu nchini.picha na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...