Dkt Arnold Chiwalala akivalishwa kofia maalumu ya Nondozzzz ya udaktari katika Mahafali ya 3 ya kimataifa (Conferment Ceremony 2012) yaliyo andaliwa na chuo kikuu maarufu kinachoitwa Sibelius Academy, Finland leo. Msomi huyu ni mmoja wa wadau wakubwa wa Globu ya Jamii wa Finland, ambako ndiko ilikoanzishwa Septemba mwaka 2005.
Katika tukio hili waliofuzu shahada ya udaktari walivishwa kofia maalumu, pia wateule wachache kutoka mataifa mbalimbali walitunukiwa heshima ya udakatari na kuvishwa kofia. Mwaka 1997 mtanzania Dkt Hukwe Zawose (marehemu) alikuwa miongoni mwa wachache waliotunukiwa heshima ya udaktari na kuvishwa kofia hiyo. Dkt Chiwalala ni mtanzania/mwafrika wa kwanza kusoma na kufikia ngazi ya udaktari (2009) katika historia ya chuo hicho- Sibelius Academy.

Mbali ya kubobea katika ubunifu wa sanaa, Dkt Chiwalala ana uzoefu mkubwa wa kuongoza, kufundisha na kutoa mihadhara. Pia ni mtaalamu na mshauri katika nyanja za utamaduni. Mfano, 2010 alikuwa mtaalamu na mshauri wa utamaduni katika bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa, Finland.
Mradi unaoendelea sasa: Dkt Chiwalala ni mtaalamu na mmoja wa waanzilishi wa urafiki kati ya mji wa Bagamoyo, Tanzania, na Mji wa Haapavesi, Finland. Urafiki/ushirikiano unalenga utamaduni na elimu.
Ukaribisho kwenye tafrija Dkt Chiwalala akiwa na mama Chiwalala (mai waifu)
hadhira: wakuu, maprofesa, wasom n.k
Maandamano kuelekea kanisani kwa ibada maalumu kabla ya mdau Dkt Chiwalala na wenzake kula nondozzz zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...