Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi  ameanzisha rasmi safari ya kupanda mlima kilimanjaro kwa mwaka huu inayoratibiwa kila mwaka na kampuni ya Geita Gold Mining LTD.  Kampeni hiyo ya mapambano dhidi ya Ukimwi na maambukizi ya Ukimwi  aliyoanza nayo Mzee Mwinyi tangu mwaka 2002 na inafahamika kama Kilimanjaro Climb against HIV/AIDS 2012 
Mzee Mwinyi alifanya uzinduzi huo katika lango la Machame lililoko wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.
-Kilichovutia zaidi ni kwa Mzee Ruksa kuwa fit kwa kipande alichotembea na leo kwa kiasi fulani alipunguza ule umbali anaopanda ambapo kila mwaka usababisha kati ya kundi lake la wapambe robo tatu kuishia njiani
Pichani Mzee Mwinyi pamoja na Mkewe Mama Siti Mwinyi wakiongozana na mwenyeji wao mkuu wa wilaya ya Hai Mhe.  Novatus Makunga pamoja na kundi la Wapanda Mlima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2012

    Hajapata kuonja pombe huyu ndio maana. Chakula mafuta hali, wake wawili wanamtosheleza. Zaidi ya hapo Mungu hakunyimi afya njema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...