Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), 
Dkt. Willibrod Peter Slaa 
--
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Peter Slaa amealikwa kuwa mmoja wa wanajopo (panelists) wanne, kutoka Mabara ya Afrika, Asia, Amerika Kusini na Ulaya, watakaojadili mada isemayo “Demokrasia Shinikizoni (democracy under pressure)” nchini Ujerumani.
 Katibu Mkuu Dkt. Slaa ambaye amesafiri jana jioni kuelekea Ujerumani, atakuwa pamoja na wanajopo wenzake wengine ambao ni Prof. Dr. Kyaw Yin Hlaing (Academic Director Myanmar Egress; kutoka Rangum/Myanmar), Dkt. Aliaksandr Milinkiewitsch (Chairman, Movement for Freedom; kutoka Minsk/ Belarus), Gavana Henrique Capriles Radonski (Leader of the Opposition Movement Mesa de la Unidad Democratica; kutoka Carcas/ Venezuela).
  Mjadala wa mada hiyo ya Demokrasia Shinikizoni, itakuwa ni sehemu ya sherehe za miaka 50 za Siku ya Shirika la Konrad-Adenauer-Stiftung (KAS Day) katika mahusiano yake ya kimataifa na wadau wake mbalimbali kutoka nchi 80 duniani.
Mwenyekiti wa wanajopo katika kuendesha mjadala huo ni Christoph Lanz (Director of Global Content; Deutsche Welle, Berlin/ Germany)
 Sherehe hizo pia zitahudhuriwa na Kansela wa Ujerumani, Dr. Angela Merkel, Rais Mstaafu wa Chile, Seneta Eduardo Frei Ruiz-Tangle na Rais Mstaafu wa Bunge la Ulaya ambaye pia ni Mwenyekiti wa KAS, Dr. Hans-Gert Pottering.
 Shirika la KAS linatimiza miaka 50 tangu lilipoanza rasmi kujihusisha na ukuzaji wa demokrasia, uhuru, amani maendeleo na haki. Kwa muda wote huo limekuwa likifanya kazi na wadau katika nchi mbalimbali duniani kutimiza malengo hayo tajwa.

Mpaka sasa KAS ina ofisi 80 sehemu mbalimbali duniani (pamoja na Tanzania), ikishirikiana na wadau wake katika kuendesha miradi inayohusiana na malengo hayo katika nchi 120.

Katika kusherehekea Jubilee ya Miaka 50 ya Siku ya KAS itakayofanyika Juni 27, 2012, shirika hilo limeamua kukutana na wadau na marafiki zake ambao pia wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika utendaji kazi wa KAS katika shughuli za kupigania demokrasia na maendeleo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa nchi husika.

Katika mada ya “Demokrasia Shinikizoni”, wanajopo watajadili changamoto zinazowakabili watetezi wa demokrasia katika tawala mbalimbali zinazotumia njia dhalimu zinazobana upanukaji wa demokakrasia ambayo ni msingi muhimu wa maendeleo ya watu.

Imetolewa jana Juni 25, 2012, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Afisa Habari CHADEMA  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2012

    Ooooh kule kwa wafadhili wao,...sasa mbona inaonekana kama alikwenda tu kwenye sherehe ya jubilee...JK akisafiri kikazi kwa manufaa ya taifa ni kosa lakini Slaa poa kabisa

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2012

    aende tu; kibaraka wa wachaga !

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2012

    Amekwenda kupewa fedha na wale jamaa wa herufi tatu? Maana wao hawana raha mpaka waone chokocho katika nchi zenye amani, angalia tu profile ya nchi wanazozifadhili Belorusia, Venezuela na (Chadema) Tanzania? tena bahati mbaya sana jamaa wa herufi tatu wanapitisha fedha hizo kupitia KAS ili kuwe na invisible hand! kweli tunakazi kubwa.

    Unahitajika uzalendo wa hali ya juu siyo uchu wa kutawala:-(

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 26, 2012

    Acheni Kasumba Jamani..Mambo ya Uchaga yanaingiaje hapa. Mbona wewe mpogoro na Mmatumbi hatusemi? Watu tunataka changes bana..Sio Mayowe tu alafu unaenda kupigania daladala ya kwenda kwenu pale Posta Mpya. Tubadilikeni jamani

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 27, 2012

    Wote mliocomment hapo juu mna chuki binafsi na chadema. Ukweli utabaki kuwa ukweli chedema ndio chama pekee kitakachotutoa hapa tulipo.

    ReplyDelete
  6. ROGERS LEMAJune 27, 2012

    Am Proud to Be A Chagga

    Kumbe mnatuogopa sana Wachagga...sikuwahi kutegemea
    na bado nawaambie msipo jipanga vizuri na Makabila yetu mtakomaaa
    sio CHADEMA wala huyo mjinga wenu Silaa the Chaggas Stand Alone kama wachaga bila masaada wowote tunauwezo wa kufanya wenyewe

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 27, 2012

    Mambo ya uchaga hatasijui yanaingiaje hapa kwa kweli, huyu baba sio mchaga kwanza lakini kuwa anaenda kwa wafadhali wao wakubwa Christian Democratic Union, ni kielelezo tosha kwa vile, amealikwa na chama cha Angela Merkel CDU. CDU ni Christian Democratic Union ambacho misingi yake inaendeshwa kwa mfumo wa demokrasia ya Kikristo na msisitizo wa uelewa wa Kikatoliki wa majukumu ya binadamu kwa Mungu. Sera zake zinatokana na Siasa za Kikatoliki, elimu ya jamii ya Kikatoliki na siasa za Kiprotestanti.
    Ingawa wanasema wanakaribisha wanachama wa madhehebu mengine lakini msingi na sera zao ndio kama hizo. Na Chadema tunajua haswa ni CDM Christian Democratic Movement hii ingine danganya toto.
    Sasa wanakataa nini kuambiwa kuwa ni chama cha kidini………….wengine wanaongeze kikabila CDM ChagaDemocraticMovement.
    Huo ndio ukweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...