
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Dkt. Willibrod Peter Slaa
--

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Peter Slaa amealikwa kuwa mmoja wa wanajopo (panelists) wanne, kutoka Mabara ya Afrika, Asia, Amerika Kusini na Ulaya, watakaojadili mada isemayo “Demokrasia Shinikizoni (democracy under pressure)” nchini Ujerumani.
Mwenyekiti wa wanajopo katika kuendesha mjadala huo ni Christoph Lanz (Director of Global Content; Deutsche Welle, Berlin/ Germany)
Mpaka sasa KAS ina ofisi 80 sehemu mbalimbali duniani (pamoja na Tanzania), ikishirikiana na wadau wake katika kuendesha miradi inayohusiana na malengo hayo katika nchi 120.
Katika kusherehekea Jubilee ya Miaka 50 ya Siku ya KAS itakayofanyika Juni 27, 2012, shirika hilo limeamua kukutana na wadau na marafiki zake ambao pia wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika utendaji kazi wa KAS katika shughuli za kupigania demokrasia na maendeleo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa nchi husika.
Katika mada ya “Demokrasia Shinikizoni”, wanajopo watajadili changamoto zinazowakabili watetezi wa demokrasia katika tawala mbalimbali zinazotumia njia dhalimu zinazobana upanukaji wa demokakrasia ambayo ni msingi muhimu wa maendeleo ya watu.
Imetolewa jana Juni 25, 2012, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Afisa Habari CHADEMA


Ooooh kule kwa wafadhili wao,...sasa mbona inaonekana kama alikwenda tu kwenye sherehe ya jubilee...JK akisafiri kikazi kwa manufaa ya taifa ni kosa lakini Slaa poa kabisa
ReplyDeleteaende tu; kibaraka wa wachaga !
ReplyDeleteAmekwenda kupewa fedha na wale jamaa wa herufi tatu? Maana wao hawana raha mpaka waone chokocho katika nchi zenye amani, angalia tu profile ya nchi wanazozifadhili Belorusia, Venezuela na (Chadema) Tanzania? tena bahati mbaya sana jamaa wa herufi tatu wanapitisha fedha hizo kupitia KAS ili kuwe na invisible hand! kweli tunakazi kubwa.
ReplyDeleteUnahitajika uzalendo wa hali ya juu siyo uchu wa kutawala:-(
Acheni Kasumba Jamani..Mambo ya Uchaga yanaingiaje hapa. Mbona wewe mpogoro na Mmatumbi hatusemi? Watu tunataka changes bana..Sio Mayowe tu alafu unaenda kupigania daladala ya kwenda kwenu pale Posta Mpya. Tubadilikeni jamani
ReplyDeleteWote mliocomment hapo juu mna chuki binafsi na chadema. Ukweli utabaki kuwa ukweli chedema ndio chama pekee kitakachotutoa hapa tulipo.
ReplyDeleteAm Proud to Be A Chagga
ReplyDeleteKumbe mnatuogopa sana Wachagga...sikuwahi kutegemea
na bado nawaambie msipo jipanga vizuri na Makabila yetu mtakomaaa
sio CHADEMA wala huyo mjinga wenu Silaa the Chaggas Stand Alone kama wachaga bila masaada wowote tunauwezo wa kufanya wenyewe
Mambo ya uchaga hatasijui yanaingiaje hapa kwa kweli, huyu baba sio mchaga kwanza lakini kuwa anaenda kwa wafadhali wao wakubwa Christian Democratic Union, ni kielelezo tosha kwa vile, amealikwa na chama cha Angela Merkel CDU. CDU ni Christian Democratic Union ambacho misingi yake inaendeshwa kwa mfumo wa demokrasia ya Kikristo na msisitizo wa uelewa wa Kikatoliki wa majukumu ya binadamu kwa Mungu. Sera zake zinatokana na Siasa za Kikatoliki, elimu ya jamii ya Kikatoliki na siasa za Kiprotestanti.
ReplyDeleteIngawa wanasema wanakaribisha wanachama wa madhehebu mengine lakini msingi na sera zao ndio kama hizo. Na Chadema tunajua haswa ni CDM Christian Democratic Movement hii ingine danganya toto.
Sasa wanakataa nini kuambiwa kuwa ni chama cha kidini………….wengine wanaongeze kikabila CDM ChagaDemocraticMovement.
Huo ndio ukweli