Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi, pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe wakimkabidhi rasmi kadi ya uanachama wa CHADEMA mwanachama mpya ambaye ni mwana mitindo Linda Bezuidenhout (LB) katika ofisi ya tawi la Chadema Washington DC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2012

    sawa kabisa linda kuwa chedema maana matusi na mdomo mchafu unafaa kabisa karibu chadema

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2012

    Wadau!
    Mwanachama mpya wa CDM Linda anaonekana ameshawishika kuingia uanachama wa CDM kutokana na ama Sera za CHADEMA au kuna ushawishi mwingine alioupata kutokana na ziara ya Waheshimiwa Wabunge wa Chadema ambao walikuwa wametembelea Marekani hivi karibuni, hii inaonesha ni jinsi gani Watanzania walio nyumbani na ughaibuni walivyo na mtizamo tofauti katika itikadi za kisiasa, na hali hii inatishia mustakabali wa CCM kwa siku zijazo, anyway! Hongera Sana Linda Bezuidenhout! Inawezekana umefanya uamuzi wa busara lakini nakumbuka kuwa ulisomeshwa na fedha za Serikali ya CCM pale Vituka Technical Secondary School katika miaka ya 1986 hadi 1989 "O" Level kama sikosei! Najaribu kuvuta kumbukumbu! Utashi ni wako na pia tunakukaribisha Bongoland!!

    Shark_ham@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2012

    Kwa hiyo sare hata mimi naomba kadi.Lol. Kweli wewe mwana mititndo. Huyo anayesema kasomeshwa na ela za serikali what has it got to do with uanachama wake wa CHADEMA; kwani ela za serikali ni za CCM?????

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2012

    Watu mna mambo kwani kusomeshwa na serikali ndo ukubali kuburuzwa hata kama wapelekwa shimoni? Kama ameamua kwenda Chadema ni kwa hiari yake na utashi wake acheni chuki binafsi. Hongera mdada mwaya na nimependa hlo gwanda lako nami nahitaji kama hilo kwavile wewe mwanamitindo basi utudizainie nasisi wadada wa kibongo mitindo ya kuvaa sare ya chadema. Hata mimi nikirudi bongo natafuta kadi kabisa
    Mdau kutoka Ujerumani

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2012

    Ukisomeshwa na Serikali ndio lazima ubaki CCM?? Hata kama chama kinaboronga lazima tulipe fadhila kwa kuking'ang'ania, au sio??

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2012

    Linda sasa ndoa yako iko hatarini au mashakani. Subiri tutasikia umeteuliwa mbunge wa viti maalum au ka cheo chochote utapata. Chezea chama cha kuvunja ndoa!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2012

    "How an intelligent man can subscribe to a political party I find a complete mystery. Loyalty to a party means surrendering some independence of thought." - Albert Einstein

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2012

    Huyu aje kugombea ubunge 2015. Kama atagombea jimbo ninaloishi atapata kura yangu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2012

    Linda na mimi nataka hilo gwandaaa lol!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 07, 2012

    Kombati lako tu dada Linda.....kwa kweli na mie naomba kadi!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 07, 2012

    Mimi ninapenda sera za CHADEMA na nipo tayari kabisa kujiunga na chama hicho. Kwa taarifa ya mchangiaji hapo juu, mimi nimesomeshwa na pesa za wananchi wa Tanzania kuanzia darasa la kwanza mpaka kiwango cha Masters degree. CHADEMA ni chama cha Watanzania wote. Usidhani kuwa Tanzania ni mali ya CCM, bali inahitajika kuwajibika kwa Watanzania. Kama haiwajibiki, Watanzania tuna uhuru wa kukitosa wakati wowote na kujiunga na chama kingine!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 07, 2012

    Mdau hapo juu umenena. Ni wale wenye mawazo yaliyopitwa na wakati wanadhani shule za serikali ni za CCM. Asilimia kubwa ya watanzania tumesomea shule za serikali ambazo ni shule za wananchi wakulima, wafanyakazi n.k. Ni hii confusion kwamba cha Serikali ni cha CCM ndio kinafanya watu wabaki nyuma kifikra. Siwalaumu tumekuwa na chama kimoja muda mrefu sana.
    NCHI HII NI YETU SIO YA CCM.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 07, 2012

    Dada mwisho mwampamba huyu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 07, 2012

    Shark_han huna sera, hela za serikali ya CCM ni za EPA au ni za ufisadi gani? Navyoelewa mimi hela zinazosomesha watu ni za serikali ya Tanzania na sio za serikali ya CCM. Unachotaka tu kuonyesha ni kwamba unamfahamu huyo mwana mitindo.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 07, 2012

    Ela za SERIKALI sio za MAGAMBA kaka hapo juu,hili ndio tatizo letu wa TZ wengi,uelewa wa KUCHAMBUA mambo ni mdogo sana,dada ake RICHARD (BBA winner) tupo pamoja,na GWANDA hiloooooo daaah,,yaaan yaaaan yaaan lazima CHICHIEM yatasema,we need changes no way bana,ka MBWAI acha tu na iwe MBWAI aishee oshieeee.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 07, 2012

    HIZI MISHEMISHE ZA VYAMA VYA SIASA BONGO KUFUNGUA OFISI UGHAIBUNI NI UTAMADUNI MPYA KIDOGO, SIONI KASI HII HAPA KWETU JAPOKUWA WAPO WAGENI WENGI WA NJE WAKIFANYA KAMA TUFANYAVYO. AU NI MOJA YA TACTICS ZA OMBAOMBA?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 07, 2012

    wewe unaesema kuwa huyo mwanachama mpya eti kashawishika kwani ulitaka afanye nini? eti umeshawishika na viongozi waliokuja hivi karibuni sasa ulitaka iweje ?

    alafu umerudi kwa huyo Bezuidenhuut Kuwa alisomeshwa na hela za ccm sasa hata kama alizomeshwa na hela za ccm tatizo lipo wapi?

    ni nani anaechukua kodi kwa wananchi kama sio serikali ya ccm? sasa ulitaka asomeshwe na nani tena miaka ya 90?

    wewe inaonekana ndio wale wenye chuki kali sana na vyama vingine wewe una uccm kwenye damu waachie wenzio wajiunge kwenye vyama wanavyotaka

    wacha kuwachambua watu eti alikuwa sijui nini nini kwani kina mrema walikuwa wapi zamani?

    au hujui kuna viongozi wangapi wametoka ccm na kujiunga na vyama pinzani hali ya kuwa walikuwa wanakula mihela ya serikali ya ccm kabla ya hapo?

    kuingia chama ukipendacho ni jukumu na maamuzi ya mtu na sio eti sababu alikuwa ccm na wale wanaotoka vyama vingine na kuingia ccm tuseme nini?

    wacha zako wewe
    karibu sana dada kwenye chama cha vijana wanaotaka maendeleo waliochoka kubuluzwa

    hongera sana kwa maamuzi mazuri

    mdau uholanzi.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 07, 2012

    Duh Linda (LB) umesha uvaa mkenge!

    Utachemsha mawe bibie,

    Sasa hao jamaa CDM hadi waje wapate ni lini ?

    Ungeenda CCM ndio ungepiga bao inawezekana hata Viti Maalum, U-DC ,ama Uafisa wowote ungepata!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 07, 2012

    Linda hahitaji vyeo vya kupewa,miaka yote ninayomfahamu hajawahi kusema anataka cheo cha kuteuliwa.
    .Acha mawazo mgando wewe.

    ReplyDelete
  20. mimi sijawahi sikia vyama vya conservative na labour vya uk, au republican na democrat vya us wakawa na matawi tz au popote nje ya nchi zao. linda amekuja hapo kutafuta publicity tu, she has no clue when it comes to politics.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 08, 2012

    Binti mitindo umeolewa? he leo michuzi utaua watu umeanza kwa dj fetty sasa kwa linda asalaleee na kweli pandukizi analo binti mitindo si mchezo ijaokua picha ni nusu

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 08, 2012

    Kwani lazima vyama vyetu vifanye kila kitu wafanyacho republic na democrat? Watu wengine mna mitazamo finyu!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 08, 2012

    Wadauuuuu!!! Anon!!!
    Ankal!!
    Watanzania tunasifika kwa umoja na upendo wetu! jana nilijaribu kuchangia hoja kuhusu kujiunga kwa watanzania na vyama vya siasa ughaibuni, nilijaribu kuelezea hisia zangu kuhusu Dada Linda kujiunga na CHADEMA tawi la Marekani, Mrusho nyumba (feedback) niliyoipata kutoka kwa wachangiaji mada hiyo katika blog yako ankal imenifanya nifikiri mara tatu kuhusu mustakabali wa nchi yetu siku zijazo. Wadau hawana hoja za msingi zaidi ya kusifia gwanda alilovaa huyu modo Linda!! vitu vya ajabu!! Mwingine anakuambia wewe mdau huna jipya kwani ukisomeshwa na CCM basi hutakiwi kuhama Chama? Hawa watu karibu wengi wapo Ughaibuni lakini hawana upeo wa kufanya upembuzi yakinifu kwa kujibu hoja za msingi wa mjadala huu. Na inawezekana unajaribu kutwanga maji kwenye kinu kwa kujaribu kuelimisha jamii kupitia blog yako ya jamii!! Chuki za dhahiri zisizo na kipimo kwa Chama Tawala zitawafikisha wapi enyi vijana mliopo ughaibuni!! hatukatai kukosolewa lakini pia jifunzeni kupitia majadiliano ya kiungwana, Hongera Linda kwa kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo!!! Chama ambacho kila Mjomba, Binamu, Shangazi, Wifi na Shemeji anapewa Ubunge wa Viti Maalum!! Chama ambacho ukitaka kugombea Uenyekiti wa Taifa! Mwenyekiti Mstaafu na Muasisi anakwambia wewe ni nani? hufai kuwa kiongozi mkuu wa chama hiki! Mkwe wangu Freeman awe nani ikiwa wewe unautaka uenyekiti wa chama!! Hongereni CDM! Hongera Linda! Hongereni Wadau mnaopiga box abroad!!

    shark_ham@yahoo.co.uk

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...