Home
Unlabelled
Tawi la CHADEMA Washington DC lapata mwanachama mpya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
sawa kabisa linda kuwa chedema maana matusi na mdomo mchafu unafaa kabisa karibu chadema
ReplyDeleteWadau!
ReplyDeleteMwanachama mpya wa CDM Linda anaonekana ameshawishika kuingia uanachama wa CDM kutokana na ama Sera za CHADEMA au kuna ushawishi mwingine alioupata kutokana na ziara ya Waheshimiwa Wabunge wa Chadema ambao walikuwa wametembelea Marekani hivi karibuni, hii inaonesha ni jinsi gani Watanzania walio nyumbani na ughaibuni walivyo na mtizamo tofauti katika itikadi za kisiasa, na hali hii inatishia mustakabali wa CCM kwa siku zijazo, anyway! Hongera Sana Linda Bezuidenhout! Inawezekana umefanya uamuzi wa busara lakini nakumbuka kuwa ulisomeshwa na fedha za Serikali ya CCM pale Vituka Technical Secondary School katika miaka ya 1986 hadi 1989 "O" Level kama sikosei! Najaribu kuvuta kumbukumbu! Utashi ni wako na pia tunakukaribisha Bongoland!!
Shark_ham@yahoo.co.uk
Kwa hiyo sare hata mimi naomba kadi.Lol. Kweli wewe mwana mititndo. Huyo anayesema kasomeshwa na ela za serikali what has it got to do with uanachama wake wa CHADEMA; kwani ela za serikali ni za CCM?????
ReplyDeleteWatu mna mambo kwani kusomeshwa na serikali ndo ukubali kuburuzwa hata kama wapelekwa shimoni? Kama ameamua kwenda Chadema ni kwa hiari yake na utashi wake acheni chuki binafsi. Hongera mdada mwaya na nimependa hlo gwanda lako nami nahitaji kama hilo kwavile wewe mwanamitindo basi utudizainie nasisi wadada wa kibongo mitindo ya kuvaa sare ya chadema. Hata mimi nikirudi bongo natafuta kadi kabisa
ReplyDeleteMdau kutoka Ujerumani
Ukisomeshwa na Serikali ndio lazima ubaki CCM?? Hata kama chama kinaboronga lazima tulipe fadhila kwa kuking'ang'ania, au sio??
ReplyDeleteLinda sasa ndoa yako iko hatarini au mashakani. Subiri tutasikia umeteuliwa mbunge wa viti maalum au ka cheo chochote utapata. Chezea chama cha kuvunja ndoa!!!
ReplyDelete"How an intelligent man can subscribe to a political party I find a complete mystery. Loyalty to a party means surrendering some independence of thought." - Albert Einstein
ReplyDeleteHuyu aje kugombea ubunge 2015. Kama atagombea jimbo ninaloishi atapata kura yangu.
ReplyDeleteLinda na mimi nataka hilo gwandaaa lol!
ReplyDeleteKombati lako tu dada Linda.....kwa kweli na mie naomba kadi!
ReplyDeleteMimi ninapenda sera za CHADEMA na nipo tayari kabisa kujiunga na chama hicho. Kwa taarifa ya mchangiaji hapo juu, mimi nimesomeshwa na pesa za wananchi wa Tanzania kuanzia darasa la kwanza mpaka kiwango cha Masters degree. CHADEMA ni chama cha Watanzania wote. Usidhani kuwa Tanzania ni mali ya CCM, bali inahitajika kuwajibika kwa Watanzania. Kama haiwajibiki, Watanzania tuna uhuru wa kukitosa wakati wowote na kujiunga na chama kingine!!
ReplyDeleteMdau hapo juu umenena. Ni wale wenye mawazo yaliyopitwa na wakati wanadhani shule za serikali ni za CCM. Asilimia kubwa ya watanzania tumesomea shule za serikali ambazo ni shule za wananchi wakulima, wafanyakazi n.k. Ni hii confusion kwamba cha Serikali ni cha CCM ndio kinafanya watu wabaki nyuma kifikra. Siwalaumu tumekuwa na chama kimoja muda mrefu sana.
ReplyDeleteNCHI HII NI YETU SIO YA CCM.
Dada mwisho mwampamba huyu
ReplyDeleteShark_han huna sera, hela za serikali ya CCM ni za EPA au ni za ufisadi gani? Navyoelewa mimi hela zinazosomesha watu ni za serikali ya Tanzania na sio za serikali ya CCM. Unachotaka tu kuonyesha ni kwamba unamfahamu huyo mwana mitindo.
ReplyDeleteEla za SERIKALI sio za MAGAMBA kaka hapo juu,hili ndio tatizo letu wa TZ wengi,uelewa wa KUCHAMBUA mambo ni mdogo sana,dada ake RICHARD (BBA winner) tupo pamoja,na GWANDA hiloooooo daaah,,yaaan yaaaan yaaan lazima CHICHIEM yatasema,we need changes no way bana,ka MBWAI acha tu na iwe MBWAI aishee oshieeee.
ReplyDeleteHIZI MISHEMISHE ZA VYAMA VYA SIASA BONGO KUFUNGUA OFISI UGHAIBUNI NI UTAMADUNI MPYA KIDOGO, SIONI KASI HII HAPA KWETU JAPOKUWA WAPO WAGENI WENGI WA NJE WAKIFANYA KAMA TUFANYAVYO. AU NI MOJA YA TACTICS ZA OMBAOMBA?
ReplyDeletewewe unaesema kuwa huyo mwanachama mpya eti kashawishika kwani ulitaka afanye nini? eti umeshawishika na viongozi waliokuja hivi karibuni sasa ulitaka iweje ?
ReplyDeletealafu umerudi kwa huyo Bezuidenhuut Kuwa alisomeshwa na hela za ccm sasa hata kama alizomeshwa na hela za ccm tatizo lipo wapi?
ni nani anaechukua kodi kwa wananchi kama sio serikali ya ccm? sasa ulitaka asomeshwe na nani tena miaka ya 90?
wewe inaonekana ndio wale wenye chuki kali sana na vyama vingine wewe una uccm kwenye damu waachie wenzio wajiunge kwenye vyama wanavyotaka
wacha kuwachambua watu eti alikuwa sijui nini nini kwani kina mrema walikuwa wapi zamani?
au hujui kuna viongozi wangapi wametoka ccm na kujiunga na vyama pinzani hali ya kuwa walikuwa wanakula mihela ya serikali ya ccm kabla ya hapo?
kuingia chama ukipendacho ni jukumu na maamuzi ya mtu na sio eti sababu alikuwa ccm na wale wanaotoka vyama vingine na kuingia ccm tuseme nini?
wacha zako wewe
karibu sana dada kwenye chama cha vijana wanaotaka maendeleo waliochoka kubuluzwa
hongera sana kwa maamuzi mazuri
mdau uholanzi.
Duh Linda (LB) umesha uvaa mkenge!
ReplyDeleteUtachemsha mawe bibie,
Sasa hao jamaa CDM hadi waje wapate ni lini ?
Ungeenda CCM ndio ungepiga bao inawezekana hata Viti Maalum, U-DC ,ama Uafisa wowote ungepata!
Linda hahitaji vyeo vya kupewa,miaka yote ninayomfahamu hajawahi kusema anataka cheo cha kuteuliwa.
ReplyDelete.Acha mawazo mgando wewe.
mimi sijawahi sikia vyama vya conservative na labour vya uk, au republican na democrat vya us wakawa na matawi tz au popote nje ya nchi zao. linda amekuja hapo kutafuta publicity tu, she has no clue when it comes to politics.
ReplyDeleteBinti mitindo umeolewa? he leo michuzi utaua watu umeanza kwa dj fetty sasa kwa linda asalaleee na kweli pandukizi analo binti mitindo si mchezo ijaokua picha ni nusu
ReplyDeleteKwani lazima vyama vyetu vifanye kila kitu wafanyacho republic na democrat? Watu wengine mna mitazamo finyu!
ReplyDeleteWadauuuuu!!! Anon!!!
ReplyDeleteAnkal!!
Watanzania tunasifika kwa umoja na upendo wetu! jana nilijaribu kuchangia hoja kuhusu kujiunga kwa watanzania na vyama vya siasa ughaibuni, nilijaribu kuelezea hisia zangu kuhusu Dada Linda kujiunga na CHADEMA tawi la Marekani, Mrusho nyumba (feedback) niliyoipata kutoka kwa wachangiaji mada hiyo katika blog yako ankal imenifanya nifikiri mara tatu kuhusu mustakabali wa nchi yetu siku zijazo. Wadau hawana hoja za msingi zaidi ya kusifia gwanda alilovaa huyu modo Linda!! vitu vya ajabu!! Mwingine anakuambia wewe mdau huna jipya kwani ukisomeshwa na CCM basi hutakiwi kuhama Chama? Hawa watu karibu wengi wapo Ughaibuni lakini hawana upeo wa kufanya upembuzi yakinifu kwa kujibu hoja za msingi wa mjadala huu. Na inawezekana unajaribu kutwanga maji kwenye kinu kwa kujaribu kuelimisha jamii kupitia blog yako ya jamii!! Chuki za dhahiri zisizo na kipimo kwa Chama Tawala zitawafikisha wapi enyi vijana mliopo ughaibuni!! hatukatai kukosolewa lakini pia jifunzeni kupitia majadiliano ya kiungwana, Hongera Linda kwa kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo!!! Chama ambacho kila Mjomba, Binamu, Shangazi, Wifi na Shemeji anapewa Ubunge wa Viti Maalum!! Chama ambacho ukitaka kugombea Uenyekiti wa Taifa! Mwenyekiti Mstaafu na Muasisi anakwambia wewe ni nani? hufai kuwa kiongozi mkuu wa chama hiki! Mkwe wangu Freeman awe nani ikiwa wewe unautaka uenyekiti wa chama!! Hongereni CDM! Hongera Linda! Hongereni Wadau mnaopiga box abroad!!
shark_ham@yahoo.co.uk