Watuhumiwa wanne wa Uwindaji haramu kwenye Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha ambao wote ni wakazi wa kijiji cha Kambi ya Simba,Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu wakiwa na maboga yaliyowekwa sumu kwa lengo la kuwaua Tembo ili kujipatia Meno yake baada ya kukamatwa na askari wa Mamlaka hiyo,watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2012

    Bila kuwakamata wafanyabiashara husika ni kazi bure. Kesha watawatuma walalahoi wengine, na kuliendeleza kama kawaida!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2012

    Ni vidagaa tu hawa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2012

    Watu wa namna hii kuanzia Wawindaji na Mtandao mzima hadi hao Matajiri wao wawataje ni watu wa kufungwa maisha!

    Nchi yetu ipo hoi Kiuchumi, masuala ya misaada ya nje ni utata mtupu kilichobaki ni kujitegemea kwa vitu kama Mali asili zetu na Sekta ya Utalii kwa kuwahifadhi na kuwatunza wanyama wetu kama hawa Tembo !

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2012

    Hawa jamaa watandikwe ili akili ya kizalendo iwarudie.......kwasaabu kama mtu una akili ya kizalendo hutakubali jangili akutumie

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2012

    Nyie mnaongea tuu... hamjui maisha yalivyo magumu bongo. Wewe unafikiri wanapenda kufanya hivyo? Nani afe? Tembo au Wao kwa njaa!!!! Kila kukicha maisha yanazidikua magumu... Hawana access ya elimu, chakula, maladhi wala kazi za kueleweka. Hao mafisadi mbona wao wasifungwe maisha.... ?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 14, 2012

    Mtandao ni mkubwa... hawa wamechoka mbaya. kuna matajiri wamewatuma kazi. Tafuta kwanza matajiri wao. Kwanza mnapoteza muda wenu kukamata watu wa namna hii , mtafukuzwa kazi bure kwa kuingilia maisha ya vigogog

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 15, 2012

    Kama wana njaa wale hayo maboga badala ya kuwauwa Tembo ili wapate hela ya kula. Kuna mdau hapo juu anatia kichefuchefu kutetea watu kama hawa. Unajua hata jambazi ukimkamata atakuambia hali ngumu.. Hali ngumu ni changamoto tuu binadamu hakuumbwa kukaa tuu na kupata mahitaji kirahisi rahisi. Hali ngumu ni kuzidisha juhudi na sio kufanya uhalifu, kama kila mtu angekuwa na mawazo kama yao nani angebaki?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...