Mkurugenzi Mtendaji na Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Ecobank nchini Tanzania,Samuel Ayim (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kuchezeshwa kwa Droo ya kwanza ya Bahati Nasibu ya promosheni ya Shinda Babkubwa na Ecobank iliyofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Benki hiyo,Jijini Dar.Kulia ni Msimamizi Mkuu wa Bidhaa na Masoko wa Benki hiyo,Andrew Lyimo na Kushoto ni Mkuu wa Benki za Ndani wa Benki hiyo,Joyce Malai.
Msimamizi Mkuu wa Bidhaa na Masoko wa Benki ya Ecobank,Andrew Lyimo (katikati) akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Promosheni hiyo.
Mdau Julio Batali wa Selcom na Humud Abdul wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha wakiichezesha droo hiyo.
Droo ikiendelea kuchezeshwa.
Wateja 15 wakiwepo wateja binafsi na wajasiriamali waliibuka washindi katika promosheni ya shindababkubwa na Ecobank. Benki ya Ecobank ni benki halisi ya KiAfrika inayojivunia uwepo wake katika nchi 32 Afrika nzima. Siku zote za uwepo wetu katika soko hili tunahamasika zaidi kushirikiana na jamii katika kujenga uchumi wa Tanzania.
Akiongea Jijini Dar es salaam leo katika uzinduzi wa droo ya kwanza Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Bw Samuel Ayim alisema promosheni hii kabambe ni ya miezi sita ikiwa na lengo la kuhamasisha umma wa Watanzania kuwa na utamaduni wa kuweka amana kwa malengo ya baadae au dharura zitakazotokea.
Aliendelea kusema ahadi ya benki ilikuwa ni kuboresha maisha ya watanzania pitia zawadi mbalimbali na vilevile kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba kwa malengo ya baadae au dharura zitakapotokea.
Hii promosheni ni njia mojawapo ya jitihada zetu za kushirikiana na jamii kwasababu dhumuni hasa ni kuona watanzania wengi zaidi wakiwekeza kwa ajili ya malengo ya badae na dharura. Ecobank iko madhubuti katika kuwasaidia wajasiriamali katika kukua biashara zao. Tunahamasika zaidi kushirikiana na jamii ya kitanzania katika kujenga uchumi wa Tanzania.
Washindi 15 wa leo wameshinda zawadi mbalimbali ambazo ni kama ifuatavyo; Washindi watano (5) watapata Ipad au Laptop kutegemeana na mteja atapenda kipi. Washindi 9 watapata zawadi za vocha kwa ajili ya kununua nguo, samani za ndani, na za kieletroniki kutoka maduka yafuatayo at Mariedo, Home Shopping Centre, Unique & Clock. Na mteja 1 amejishindia tiketi ya mapumziko kwa siku moja visiwani Zanzibar ikiwa imelipiwa gharama zote.
Mkurugenzi mtendaji alisema huu ni mwanzo tuu zawadi zaidi zitazidi kushindaniwa kila mwezi ambapo washindi 15 watabahatika kujinyakulia zawadi mbalimbali. Droo ya mwisho kutakua na zawadi kubwa ya gari aina ya Hyundi Tucson mpya kabisa (thamani Tshs65m) itanyakuliwa kwa mteja atakae bahatika kuwa mshindi siku hiyo.
Kila mtanzania ana nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwepo ya gari mpya kabisa, chukua uamuzi leo na fungua akaunti na Ecobank na anza kuweka amana yako. “Utajiri huja kupitia utamaduni wa kuwekeza na haikulazimu kuwa na kiasi kikubwa ili uanze, kwahiyo anza sasa na Ecobank”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...