Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mama Maria Nyerere Tuzo ya Juu ya Heshima ya Taifa la Burundi aliyotunukiwa Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Burundi yaliyofanyika mjini Bujumbura wiki iliyopita.Mwalimu Nyerere alitunukiwa tuzo hiyo kwa mchango wake wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Burundi ambapo alikuwa mshauri wa karibu wa Waziri Mkuu wa Kwanza wa nchi hiyo Prince Louis Rwagasore. Rais Kikwete alimkabidhi Mama Maria tuzo hiyo leo asubuhi ikulu jijini Dar es Salaam. (picha Freddy Maro).
Home
Unlabelled
Rais Kikwete amkabidhi Mama Maria Tuzo ya Heshima ya Juu ya Taifa la Burundi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
prince luis rwagasore hakua waziri mkuu wa burundi alikua prince mwanae king.
ReplyDeleteHongera mama yetu wa Taifa,unastahili kupata tuzo hizo kwa niaba ya mzee wetu kipenzi chetu, baba wa Taifa letu Mwalimu J.K Nyerere. Zamani hukuwahi kupata chochote kama mke wa Rais,enzi zile zilikuwa ngumu kwa sababu ulikuwa ndiyo unamsaidia mumeo kulijenga Taifa lilokuwa maskini hadi kufikia hapa lilipo unazeeka mama yetu,unastahili kula kidogo kilichopo sasa.Manufaa haya ya sasa ni yako na mwalimu, ''sisi wa MISENYI,MINZIRO,TUNGETAMANI KULA NA WEWE CHOCHOTE KIZURI, UNASTAHILI KUPEWA DUA TU''Hususani mimi binafsi sina cha kumlipa mwalimu ila dua tu;na wewe kukutakia maisha marefu. Mimi na Familia yangu tunakutakia afya na siha iliyo njema.M/Mungu akupe baraka. ameen
ReplyDelete