Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake Malindi Mjini Zanzibar-Picha na Nafisa Madai-Maelezo Zanzibar
--
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar imezifutia rasmi hati ya kufanya kazi Meli ya Mv.Kalama, Mv.Seagul na Mv.Sepideh kutokana na meli hizo kutokukidhi hali ya usalama wa abiria katika meli hizo.
Aidha meli hizo zimepewa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo kuhakikisha zimeondoka katika maeneo ya Zanzibar kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya wamiliki wa Meli hizo.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake kuhusu hali ya usafiri wa baharini na usalama Zanzibar.
Amesema Mamlaka hiyo imefanya tathmini na uhakiki wa kutosha na kujiridhisha kuwa Meli hizo hazifai kufanya kazi katika maeneo ya Zanzibar jambo ambalo limepelekea kuchukua hatua za kufuta hati za kufanyia kazi meli hizo.
Amefahamisha kuwa sababu kuu zilizopelekea Mamlaka kufanya maamuzi hayo ni pamoja na uchakavu,umri wa meli hizo kuwa mrefu na kupata matatizo mara kwa mara katika safari zao. Kombo amefahamisha kuwa Sheria ya Mamlaka ya Usafiri na Bandari Zanzibar ya mwaka 2006 kifungu cha 17.1 inampa mamlaka Msajili wa Meli kuifuta meli yoyote ambayo itakuwa haikidhi usalama wa abiria.
Kufuatia sheria hiyo Kombo amesema watawataka wamiliki wa Meli hizo kuzirudisha hati za kufanyia kazi meli hizo ili waende kutafuta sehemu nyengine za usajili kinyume na maeneo ya Zanzibar.
Akizungumzia Meli ya Mv.Serengeti Kombo amesema wamelazimika kuiagiza meli hiyo kupunguza idadi ya abiria kutoka watu 800 hadi 350 na tani za mizigo kutoka 100 hadi 50 hadi pale ambapo watajiridhisha kutokana na hali ya meli hiyo ilivyo.
Aidha amegusia kuwa Kampuni ya Bakhresa italeta Meli kubwa ya abiria itakayofanya kazi zake Zanzibar ambapo pia Serikali ya Mapinduzi nayo iko mbioni kuhakikisha wanaleta meli inayokidhi mahitaji ya wananchi wa Zanzibar.


siku zote mlikuwa wapi mpaka watu wateketee
ReplyDeleteSasa ndio wanaaamka usingizini!
ReplyDeletesheikh abdulla, mimi nakuaminia sana hii wizara sasa hivi ilikuwa wewe ndio waziri
ReplyDeletekwani uchapakazi wako tunaufahamu endelea na majukumu na tunaamini kuwa mambo yatakuwa mazuri tu chini ya uongozi wako mzee
kutoka mikocheni b.....shuleni pale
kwahiyo meli zisizofaa ni hizo tu au kwakuwa zinahusiana na meli iliyopata ajali?
ReplyDeleteHii ndio hatua inayostahili!
ReplyDeleteTuache kuendesha mambo kwa kutazamana usoni tufuate kanuni, vigezo na mashariti.
Baada ya Kisa mkasa....
ReplyDeletesasa wangetoa na picha za meli hizo ili watu wazijue, manake mtu saa zingine anaenda gatini tuu na kutafuta ticket ya boti bila kufahamu ni ipi au ikoje ikoje!
ReplyDeletemnakumbuka shuka wakati kumekucha..POOR
ReplyDeletemaamuzi ya jazba, mara zote hayana busara, mmefanya hivyo ili kujiosha na si kwa ajili ya kufanyakazi yenu kikamilifu!!!
ReplyDelete