Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake  Malindi Mjini Zanzibar-Picha na Nafisa Madai-Maelezo Zanzibar
--
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 
            Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar imezifutia rasmi hati ya kufanya kazi Meli ya Mv.Kalama, Mv.Seagul na Mv.Sepideh kutokana na meli hizo kutokukidhi hali ya usalama wa abiria katika meli hizo. 
Aidha meli hizo zimepewa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo kuhakikisha zimeondoka katika maeneo ya Zanzibar kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya wamiliki wa Meli hizo.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake kuhusu hali ya usafiri wa baharini na usalama Zanzibar. 
Amesema Mamlaka hiyo imefanya tathmini na uhakiki wa kutosha na kujiridhisha kuwa Meli hizo hazifai kufanya kazi katika maeneo ya Zanzibar jambo ambalo limepelekea kuchukua hatua za kufuta hati za kufanyia kazi meli hizo.
Amefahamisha kuwa sababu kuu zilizopelekea Mamlaka kufanya maamuzi hayo ni pamoja na uchakavu,umri wa meli hizo kuwa mrefu na kupata matatizo mara kwa mara katika safari zao. Kombo amefahamisha kuwa Sheria ya Mamlaka ya Usafiri na Bandari Zanzibar ya mwaka 2006 kifungu cha 17.1 inampa mamlaka Msajili wa Meli kuifuta meli yoyote ambayo itakuwa haikidhi usalama wa abiria.
Kufuatia sheria hiyo Kombo amesema watawataka wamiliki wa Meli hizo kuzirudisha hati za kufanyia kazi meli hizo ili waende kutafuta sehemu nyengine za usajili kinyume na maeneo ya Zanzibar.  
Akizungumzia Meli ya Mv.Serengeti Kombo amesema wamelazimika kuiagiza meli hiyo kupunguza idadi ya abiria kutoka watu 800 hadi 350 na tani za mizigo kutoka 100 hadi 50  hadi pale ambapo watajiridhisha kutokana na hali ya meli hiyo ilivyo.
Aidha amegusia kuwa Kampuni ya Bakhresa italeta Meli kubwa ya abiria itakayofanya kazi zake Zanzibar ambapo pia Serikali ya Mapinduzi nayo iko mbioni kuhakikisha wanaleta meli inayokidhi mahitaji ya wananchi wa Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2012

    siku zote mlikuwa wapi mpaka watu wateketee

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2012

    Sasa ndio wanaaamka usingizini!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2012

    sheikh abdulla, mimi nakuaminia sana hii wizara sasa hivi ilikuwa wewe ndio waziri

    kwani uchapakazi wako tunaufahamu endelea na majukumu na tunaamini kuwa mambo yatakuwa mazuri tu chini ya uongozi wako mzee
    kutoka mikocheni b.....shuleni pale

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2012

    kwahiyo meli zisizofaa ni hizo tu au kwakuwa zinahusiana na meli iliyopata ajali?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2012

    Hii ndio hatua inayostahili!

    Tuache kuendesha mambo kwa kutazamana usoni tufuate kanuni, vigezo na mashariti.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2012

    Baada ya Kisa mkasa....

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2012

    sasa wangetoa na picha za meli hizo ili watu wazijue, manake mtu saa zingine anaenda gatini tuu na kutafuta ticket ya boti bila kufahamu ni ipi au ikoje ikoje!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2012

    mnakumbuka shuka wakati kumekucha..POOR

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 27, 2012

    maamuzi ya jazba, mara zote hayana busara, mmefanya hivyo ili kujiosha na si kwa ajili ya kufanyakazi yenu kikamilifu!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...