Leeds Swahili Culture Community ina furaha kuwakaribisheni Ndugu wote kuhudhuria Mihadhara ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani iliyoandaliwa hapa Leeds U.K. kama ifuatavyo;
Tarehe: 28.07.2012; siku ya Jumamosi , muhadhara kuanzia saa 12 jioni ikifuatiwa na futari kwa wote.
Tarehe: 11.08.2012; siku ya Jumamosi, muhadhara kuanzia saa 12 jioni
Ikifuatiwa na futari kwa wote.
Mihadhara na kufutari vyote vitafanyika kwenye ukumbi
wa Erbo Garden Hall- Leeds.
Kwa upendo na Baraka za Allah, Wote mnakaribishwa na tafadhali mfahamishe na mwenzio.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na mwenyekiti (LSCC) kwa namba
+447946724908 au +447575464698.



Wanazuoni nina swali,je ukifuturishwa na watu wasio ma fardhi(sio waislamu),je saumu inaswihi? Tuelimishane please
ReplyDeleteJamaa zangu walipokuwa wanasoma Dover College UK miaka ya 90, walikuwa wanatengewa futari. Mimi si mwanazuoni kwa hivyo sina jibu lakini nina hakika kabisa kuwa kama anayekufuturisha (awe Mwislamu au si Mwislamu)anafanya biashara ya pombe, ukahaba. nguruwe, kamari au madawa ya kulevya basi utakuwa huna swaumu kabbisa.
ReplyDeleteKama si mwanazuoni unajibu ya nini maana hujajibu spesific za swali,in general rule ukiacha hizo tabia ulizotaja(ulevi etc.),mtu wa dini nyingine akijitolea kufuturisha,je saumu inashwhi? Please kama huna jibu kaa kimya maana serious people needed.
ReplyDelete