Kaka michuzi,
Naomba wanaohusika na masuala ya rekodi za mambo yasiyo ya kawaida wamtafute huyu Mama Vilet, mjini Dodoma. Hana mikono. Ana umri wa miaka 41 na anao watoto wawili; mkubwa akiwa na umri wa miaka 18 na anasoma kidato cha nne. Mama huyu ni mnyenyekevu na ndiyo maana alikubali nipige picha naye Mnadani, Dodoma. Nimekutana na wafupi, lakini huyu mama kwa kweli nimemvulia kofia!

Mdau Manyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2012

    niliwahi kuona mtu mfupi kwenye TV ya CNN ana miaka 71 nafikiri alikuwa na urefu wa nchi 14 kwa hapa sikumbuki vizuri na anatokea nchi ya Pakistani-lakini hata huyu wa kwetu ,jamani naye yumo kwenye rekodi ,please wanaojua anga za mabook ya gueness ,njooni na bongo. Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2012

    huruma hamna, badala ya kumsaidia wanakimbilia kumpa mizigo ya watoto.

    hata hivyo inaonekana anajitahidi kupigana na maisha na hakati tamaa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2012

    Na yeye anayo haki ya kupata watoto. Nadhani wakiwa na elimu na wakajitambua watamsaidia vizuri mbeleni.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2012

    Huyu mchangiaji wa Sun Jul 08, 12:52:00 PM 2012, kuwa na hali yake haimaanishi amekosa haki ya kuwa na familia, unataka asaidiwe umesikia anaomba msaada.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2012

    Aliyeko kwenye Guiness urefu wake ni robo tu ya huyo unayemuita mfupi wa Dodoma!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2012

    Mdau una matatizo mazito, kwani akiwa mlemavu ndio asizae? Kila mwaanamke anafurahi kuitwa mama, na nina uhakika ukimwuliza mwenyewe atakuambia faraja yake ya pekee ni hao watoto wake. Watanzania wengi hawajui haki za msingi za binadamu. Nakushangaa unaposema hawamwonei huruma. Yeye pia ana feelings kama wewe, na ndio maana akashiriki kikamilifu na kupata hao watoto wake. Au alikuambia amebakwa?! Tafakari kabla ya kutoa comment zisizo na maana!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 08, 2012

    She is a victim of phocomelia, and extremely rare congenital disorder involving limbs,there are several causes for this, the most common ones are the use of the drug Thalidomide in the 60s and from genetic inheritance.
    Just for the information, shortly after Thalidomide was made available as over the conter drug (In W.Germany) to treat morning sickness in pregnancy, about 7,000 children were born with phocomelia in West Germany.
    Whatever the cause to this lovely lady`s case, she seems happy and was also blessed with two children, she is a tough woman,it must have been hard to go through pregancy, child birth and looking after her children, well done to Mama vilet.
    Thalidomide was taken out use in 1996, it is still used in treatin Erythema Nodosum Leprosum.
    Dr Gangwe Bitozi

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 08, 2012

    Hivi unawezaje kufanya mapenzi na mtu kama huyu. Si kama unafanya na mtoto? Nina wasiwasi mtu aliyelala naye hata watoto anabaka.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 08, 2012

    Asante sana anonym hapo juu kwa kimombo safi na kutuelemisha juu ya hili tatizo; lakini k.m binadamu wa kawaida naye anahitaji kuwa na familia; naamini hao watoto wake ndiyo watakuwa msaada kwake, wakiongozwa na Baba yetu aliye mbinguni

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 08, 2012

    Sorry, Thalidomide was taken out of use (Ughaibuni) in 1961.
    Dr G.Bitozi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 08, 2012

    Manyerere; unasema umemvulia kofia wakati bado tunaona umeivaa???, HA HAAAAAA, HA HAAAAA.

    Jamani, huyu naye ni binadamu kama ww unayetoa maoni hapo juu. Ana haki ya kuzaa, kuishi na kuthaminiwa.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 09, 2012

    Kwanza Tunamshukuru Mungu kwa miujiza hii ya kumfanya mama huyu aweze kuzaa bila matatizo, kwasababu kama siyo miujiza mambo yafuatayo yangemtokea kwani najua aliyelala naye ni mtu wa kawaida yaani mkubwa,
    Tatizo la kwanza, angeweza kupata "uterus rapture" kwasababu ya overextension ya tumbo lake dogo,
    pili, angeweza kupata "Distockia" yaani mtoto kukwama kwenye njia ya kizazi, kwa vyovyote anamaumbile madogo proportional to her size.
    Lakini bwana akasema mimi ndiye muumbaji na maumbile nayajua mimi, naye binti yake hakupata shida,
    akamsaidia bure.
    Asante Mungu.

    ReplyDelete
  13. Wewe Anon. uliyesema:-

    "Hivi unawezaje kufanya mapenzi na mtu kama huyu. Si kama unafanya na mtoto? Nina wasiwasi mtu aliyelala naye hata watoto anabaka."

    Nadhani umejisahau na kuanza kumkufuru Muumba. Hujuwi kwamba AKIKUPA KILEMA HUKUPA NA MWENDOWE? Basi ukiutafakari huo msemo, utapata jibu fasaha na hapo ulipo kumbuka ungali hujafa basi bado hujaumbika. Mapenzi upofu, kibaya kwako, lakini chema kwa mwenzako. Dunia hii wawili wawili, pengine alijaaliwa kuwa na mwenza wake na yote yakawezekana, tuache kufuru tukijidhania tumekamilika na kutowa maneno ya kejeli au kashfa kwa wengine. Mwenyeez Mungu akulinde na azidi kukupa nguvu na uwezo Mama Vilet, ili uweze kuitunza familia yako na muishi kwa salama na amani raha mustarehe.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 09, 2012

    sio kweli huyo siyo mfupi.nipe mail yako nikutumie mtu mfupi zaidi duniani kulingana na guiness book of records. au kwa kukusaidia anatoka singapore

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 09, 2012

    Mapenzi hayana adabu!

    Wadau hamjaona watu wanawazalisha Vichaa,Vipofu, Mabubu na Mataahira ije kuwa huyu mtu ingawa ni Mlemavu wa kuwa na umbile fupi lakini ana akili zake timamu?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 09, 2012

    Watu wengi wanaustaarabu wa kuazima, usiotoka moyoni na wakibinafs! Nao na ndoo huzaa kujipendelea na kusahau wengine, huo ni ufisadi.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 09, 2012

    Nahisi huyu mama akisoma comments za baadh ya wachangiaji hapa atajisikia vibaya sana na atatokwa na machozi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...