Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,Fimbo Butallah akimkabidhi zawadi Mtoto Abou Makame alieibuka mshindi wa kwanza wa kuimba nyimbo za muziki wa kufoka foka (Hip Hop) katika hitimisho la Tamasha la Wazi la Filamu nchini lililokuwa limedhaminiwa na Kampuni hiyo kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha Grand Malt.Tamasha hilo limemalizika mwishoni mwa wiki hii.Kulia ni Mkurugenzi wa Sofia Productions ambao ndio walioandaa Tamasha hilo la Wazi la Filamu,Mussa Kisoky.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,Fimbo Butallah na Mkurugenzi wa Kampuni ya Sofia Productions ambao ndio walioandaa Tamasha hilo la Wazi la Filamu,Mussa Kisoky wakiwa pamoja na Watoto waliotinga nne bora ya kusakata Dansi kwa watoto.
Wakazi wa Jiji la Tanga wakifatilia Burudani iliyokuwa ikitolewa na vijana wa Ice Cream Dances muda mfupi kabla ya kutangazwa kumalizika kwa Tamasha hilo la Wazi la Filamu nchini,lililokuwa likifanyika kwenye viwanja vya Tangamano,jijini Tanga.
Grand Malt wapigwe faini kubwa, kutumia watoto ni aibu and it is a criminal offence.
ReplyDeleteHii grand malt ni kilevi ghafi, na sio kama si kilevi. Ni kama bia za kijarumani ambazo zao ni kama maji hazileweshi ukila kiasi. Ila ukifakamamia baadae zinalewesha.
ReplyDelete