Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongazana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana Agosti 8, 2012 kuhudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki hiyo na kufutari pamoja na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) akiwaongoza baadhi ya Viongozi wa dini na Serikali ‘kujisevia’ futari wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na kufuturu pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Bilal na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa katika hafla hiyo, jana Agosti 8, 2012.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour, akizungumza machache kuhusu kazi na utendaji wa kazi za Benki hiyo ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na malengo yake wakati wa hafla hiyo ya futari iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakipata futari wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakishiriki kuomba dua ya pamoja wakati wa hafla hiyo, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam jana Agosti 8, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, na baadhi ya waumini wa dini ya kiislam baada ya hafla hiyo ya futari iliyoandaiwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) jana, Agosti 8, 2012 katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh, Abdulla Tarib Abdulla na baadhi ya waumini wa dini ya kiislam baada ya hafla hiyo ya futari iliyoandaiwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) jana katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Hii imekaa kiexecutive zaidi, no Mikekaaaa. Safi sana!inawezekana pia
ReplyDeletelakini brother Michu Hii ni benki ya watu wa Zanzibar nafikiri. Benki ya kiislam ni division tu ndani ya benki hiyo(PBZ). naomba kuwekwa sawa katika hili.
ReplyDeleteMimi Mdau kutoka Magu district
hivi huo ukumbi huwa hauuzi pombe kweli? manake wazanzibari wamesusia shughuli ya Chadema kwasababu imefanyika kwenye ukumbi wa bar. sasa hii imekaaje? Serena hotel hawauzi pombe??
ReplyDeleteI Pray God to reveal HIMSElF to each and everyone's heart so that we can see and know the truth.
ReplyDeleteMimi pia muislam lakini hawa kama wanaonekana matapeli. Mbona sheikh hana ndevu?.waislam tusome dini tusitapeliwe
ReplyDeleteUnafiki ni dhambi moja mbaya sana! hatutaki pombe Znz kwani Mungu hataki lakini ukija UASHERATI NDIO WENYEWE!
ReplyDeleteBenki ya Watu wa Zanzibar, ndivyo tunavyoifahamu sie. Banki ya Kiislamu ya Watu wa Zanzibar aidha ni kitu chengine na sio PBZ au labda imebadilika kipindi hiki cha Ramadhani kwa sababu zile zile zinazowafanya makampuni hata ya bia nayo yafuturishe watu! Uchanganyaji huu wa biashara katika mambo ya kidini utatutokea puani siku moja!
ReplyDelete