Mratibu wa kampeni ya Elimu yao Jukumu letu Rebeca Gyumi akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda jinsi harambee ya uchangiaji mabweni inavyoendeshwa na makusudio ya harambee hii. TEA inakusudia kuchangisha jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 2.3 zitakazotumika kujengea hosteli 30 katika mikoa minane nchini.
Mheshimiwa Deo Filikunjombe, Mbunge wa Ludewa akitoa mchango wake kuchangia ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike kupitia kampeni ya Elimu yao Wajibu wetu, kampeni inayoendeshwa na mabalozi wa Mamlaka ya Elimu (TEA).
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii na Mbunge wa viti maalumu(CCM) Mh. Margreth Sitta akitoa mchango wake kwa TEA katika kuchangia harakati za Mamlaka ya Elimu Tanzania kuhakikisha wanafunzi wa kike wanakuwa na makazi salama.
Mheshimiwa Vicky Kamata (MB)(Katikati) akijaribu moja ya huduma ya kuchangia kampeni hii ya ujenzi wa mabweni kulia kwake ni Nancy Sumari Miss Tanzania 2005 na kulia kwake ni Faraja Nyalandu Miss Tanzania 2006 ambao ni mabalozi wa kampeni hii.
Mh. Sophia Simba Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na Watoto akitoa mchango wake kuchangia kampeni hii bungeni. Ili kuchangia pia unaweza kutuma neno CHANGIA TOFALI kwenda namba 15564 ambapo utakatwa shilingi 250 tu za kitanzania.
Mbunge wa Kilosa Mh. Mustapha Mkulo (MB) akitoa mchango wake kuchangia kampeni hii. Mabalozi wa harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za watoto wa kike waliamua kwenda bungeni kuwaomba wabunge wachangie kampeni hiyo.








TEA mna akili kweli...mmeamua kuwafuata wenye nazo. Hapo lazima watoe (ingawa kimoyo moyo watakuwa wanalaani)
ReplyDeleteTEA wamelenga sana!
ReplyDeleteKwenda Bungeni mmechagua, mkitoka Dodoma sasa ni Dar Ofisi hadi Ofisi za Idara Wizara na Mashirika kwa Mabosi wote nchini!
Lazima mabinti walale ktk mabweni.